Zitto: Nitafanya uamuzi mgumu

Zitto: Nitafanya uamuzi mgumu

Status
Not open for further replies.
Too late and too low.
Maamuzi ya nini tena wakati ameshafukuzwa CHADEMA? Kama kumwaga, CHADEMA walianza kumwaga mboga, Zitto akaendelea kusita kumwaga Ugali, CHADEMA juzi wamemwaga na ugali kabisa. Sasa hakuna msosi tena. Zitto kwisha habari yake kabisa.
Nadhani uamuzi mgumu na muhimu pekee uliobaki kwake ni KUJIUA!!
 
Jamaa huyu anakuwa mbinafsi sana huku akiwa mwanasiasa, sijui angelikuwa daktari au engineer ingekuwaje!
Mnaodhani cdm ni wadini na wakabila na ndio maana 'wanambagua' hebu angalia shughuli anazozifanya na PAC, ni yeye tu anataka aonekane kana kwamba hiyo kamati haina wanachama wengine. CDM ilikuwepo kabla ya 2000 alipokuwa mbunge na maisha ya siasa hayaishii 2015, bado siasa zitaendelea. Kibuli, majigambo na majivuno havijengi na huenda vikambomoa yeye mwenyewe kabla ya hata hiyo cdm.
 
aombe radhi abaki chadema , aepuke maisha ya chuki
Aombe radhi kwa kukataa posho za vikao vya bunge kwa vitendo?? Kweli huko cdm kutakalika, lissu, mnyika, slaa, lema, sugu kutakalika. ?? Na mwenyekiti inawezekana sababu hawajakutana barabarani, ni rahisi kuyajenga sababu wanajuana.
 
which hard decision than joining CCM? that the hardest decision of all
It is unfortunate that ccm will be having a new chairperson probably next year. Na kuna wanaoamini kuwa baada ya uenyekiti wa JK huenda ikashikwa na 'ccm-imani' na sijui kama hilo kundi litakuwa tayari kuwaentertain wasaliti na ndumila kuwili!

 
Zitto amekaririwa na gazeti la Mtanzania la leo Jumamosi ya tarehe 14/03/2015 akisema kuwa atachukua uamuzi mgumu kuhusu hatima yake ndani ya CHADEMA.

Poor Zitto Zuberi Kabwe he does'nt get it as yet!! he is on the recieving end; wa kufanya maamuzi magumu sio yeye; CDM ndio wamefanya maamuzi magumu; yeye ni kuunga foleni na kuchanja mbuga. anachokiita hatima yake ndani ya CDM is already pre-determinned by CDM leadership; WAMEMFUKUZA period. sasa kama yeye anataka kuendelea kung'ang'ania kubaki ndani ya CDM; he is being il-ladvised! na kwa hilo wa kulaumiwa sio wanaomshauri bali yeye mwenyewe anayesikiliza na kuupokea ushauri wa hovyo kama wa Albert Msando ambaye anamshauri very subjectively kwa kuangalia upande mmoja wa shilingi na kujiaminisha kwamba yeye na Zitto ndio wenye akili tu watu wengine wote ni mambwiga tu!
Zitto fuata njia ya Mansour; hutakiwi katika CDM wewe unalazimisha nini kama sio kuendelea kujipotezea muda na kujiongezea stress na msongo wa akili?! Go go Zitto;
Zitto hautakuwa wa kwanza kwa watu waliokuwa na Glittering careers lakini zikabuma kabla ya kuchanua! Maprofesa Anna Tibaijuka na Sospateri Muongo na Edward Lowassa ni baadhi ya watu wachache mtakaoungana nao kuanzisha THINK TANK ya kufanyia utafiti uzoefu wenu mbali mbali! Good riddance Zitto
 
Ikiwa bado sakata la kufukuzwa uanachama kwa mbunge wa kigoma kaskazini (CHADEMA) mh ZITTO KABWE linaendelea kuchukua nafasi katika vichwa vya watanzania na wapenda siasa,mbunge huyo ameanza kufanya ziara ya siku tatu jimboni kwake kuzungumza na watanzania mbalimbali.

Akiwa katika ziara yake MBUNGE wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe(Chadema),amewataka wakazi wa mkoa wa kigoma wasisikitishwe na mambo yanayomkabili kwa sasa kwa kile alichoeleza kuwa asilimia kubwa ya wanasiasa makini walishapitia misuko suko kama yake.

Amewaeleza kuwa jambo la msingi ni kumuunga mkono katika hatua yoyote atakayochukua kwa ajili ya wanakigoma na Taifa kwa ujumla katika kumaliza mgogoro uliopo baina ya Chama chake na yeye.

Zitto ametoa kauli hiyo jana mjini Kigoma alipokutana na viongozi 250 kwenye mkutano wa ndani uliohusisha viongozi kutoka katika kila kijiji kwenye jimbo la Kigoma kaskazini yenye jumla ya vijiji 45.

Aliwataja baadhi ya wanasiasa waliopita katika hatua kama yake na baadae wakageuka washindi kuwa ni Maalim Seif Sharif Hamad(Tanzania),Mahathir Mohamed(Malaysia na Indira Gandhi wa India.

“Msinililie mimi kwa kuwa haya ni mapito ya kila mwanasiasa Makini,wengi walio makini walitofautiana na vyama vyao kwa sababu ya maslahi ya mataifa yao,wapo walioanzisha vyama baada ya hali hiyo na wakashinda na wapo waliopigiwa magoti na vyama vyao baada ya kugundua walichofanya si sahihi, hivyo jukumu kubwa ni kuniunga Mkono”alisema Zitto.

Alisema mpaka sasa hajapewa taarifa yoyote ya kusitishwa kwa Ubunge wake na kama hali hiyo ikijitokeza atarudi kuwafahamisha juu ya hatua atakayochukua.

Zitto yupo mjini Kigoma kwa ziara ya siku tatu,ambapo atawatembelea wakulima wa mradi wa Kahawa walio katika mfuko wa hifadhi ya Jamii(NSSF), pamoja na kukabidhi gari aina ya Ambulance katika kituo cha Afya Nyarubanda na kisha kufanya mikutano miwili ya hadhara.
 
Utamuondoshaje kama hajavunja katiba? Ujue kuna mtu kwa nje unaweza ukaona kama alifaa kuondolewa chamani lkn ukienda kwenye sheria na kanuni unakuta hamna sehemu anakutwa na hatia.Mtu huyo utamfukuzaje?

Chukua taarifa msigwa na wenje ni wachaga wa rombo
 
Tunafahamu wazee wa ukoo wa MTEI walikaa na kuamua kumfukuza.
Chama toka kianzishwe wenyeviti ni wana ukoo,Mtei,Bob makani shemeji yake mtei,Mbowe mkwe wa Mtei,atafatia mtoto wa mbowe ambaye ni mjukuu wa Mtei.Zitto alipotaka kugombea akashauriwa na mtei asigombee,jamani hiki ndo chama kinachojiita cha kimedemokrasia.
 
HAPO ITUMIKE CONFLICTING THEORY. KITU CHA KUWEZA KULETA UGUMU NI KAMA ZITTO ATATUNISHA MISULI YA UBONGO NA KAMA VIONGOZI WA JUU WATATUNISHA MISULI YA UBONGO. SI VEMA KUJENGANA NA KUADABISHANA KWA KUKOMOANA. NAAMIN WEMA NI AKIBA NIKIMANISHA ZITO ANA AKIBA YAKE YA MEMA CHADEMA NA NI AKIBA HIO HIO WAITAZAME KTK HUKUMU YA MWISHO. MAKOSA YAPO NA YANASAMEHEKA KWA KUSEMA TUMEYAMALIZA YAAN TUMESAMEHEANA . Kama kura moja inafaida kubwa sana haina haja ya wadau wa chama kudhalilishana.
Zito Aoneshe nia ya kuomba yaishe kupitia wazee, Chadema wakikataa basi tutajua wana mambo yao Binafsi.
POLE SANA ZITTO, USIFE MOYO UWE NA MATUMAIN . WAPO WENGI USIOWAJUA NA UNAOWAJUA WANAKUOMBEA MEMA NA WANAIOMBEA CHADEMA MEMA NA TAIFA LETU ILI UMOJA UWEPO.
 
Sasa braza aombe radhi kwa kosa gani?? Kutaka mahesabu ya vyama vya siasa yakaguliwe?? Kutaka kugombea uenyekiti chadema. ?? Kuonesha nia ya urais mapema??

Kosa la zitto kufukuzwa chadema sio kudai mahesabu na wala sio kutaka kugombea uenyekiti kosa lake kubwa na kuandika waraka wa kimapinduzi wakutaka kupindua viongozi
 
We zito unadhani Wa tz Ni hovyo kama we we mnafiki name msaliti mkubwa.yuda eskariot.humtishi MTU we sawa name kiriboto au kunguni tu
 
Hakuna Uamuzi Mwingine Mgumu ambao ni makini anaopaswa kufanya zaidi ya Kuomba Radhi kwa wapenzi na wanachama wa CHADEMA na kusonga mbele

Kwenda chama Kingine itakua uamuzi mgumu lakini sio makini
Ben Saanane
===>Maaana yake mko tayari kukaa na Zitto na kuongea sio?Kitila na Mwigamba je?
 
Last edited by a moderator:
Kosa la zitto kufukuzwa chadema sio kudai mahesabu na wala sio kutaka kugombea uenyekiti kosa lake kubwa na kuandika waraka wa kimapinduzi wakutaka kupindua viongozi
Kwani ni dhambi kuaandaa mkakati wowote kuelekea uchaguzi?? Je ni usaliti kuandaa timu ya watu wanaokuunga mkono?? Huhitaji kuwa mwanasheria kujibu tuhuma dhaifu za chadema juu ya zzk
 
Uamuzi mgumu angeufanya kabla ya kauli ya Tundu Lissu.

Kwa sasa uamuzi atakaofikia itaonekana kashafanyiwa na Tundu Lissu, ana react tu.
 
Ben Saanane
===>Maaana yake mko tayari kukaa na Zitto na kuongea sio?Kitila na Mwigamba je?

Ben saanane amekoment kama mwanachama wa CHADEMA. Sio kiongozi na wala hana maamuzi yeyote pia hajui chochote kuhusu maamuzi ya viongozi wa CHADEMA kuhusu Zitto.
 
Last edited by a moderator:
Kama chadema ingekua inaondoa maovu basi shibuda angeondoka kabla ya zitto maana alisaliti tangu sikubya kwanza alipohudhuria kuapishwa kwa JK.zitto n tishio kwa nafasi ya mbowe kama mwenyekiti.undugu,uchaga na ukatoliki ndo umemuondoa zitto CDM

Zitto kasaliti akiwa ndani ya steering comittee mkuu! He knows all corners like ufagio wa zamani
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom