Zitto: Nitafanya uamuzi mgumu

Zitto: Nitafanya uamuzi mgumu

Status
Not open for further replies.
"Mfa maji haishi kutapatapa" ACT ipo aende na tunamtakia heri ya kuwatoa ccm madarakani teh teh!
Kupokewa!walipokewa wakina mboga za m 10,joka la makengeza etc sembuse yeye!MATANZANIA NDO MAJITU YENYE IQ NDOGO DUNIANI,NDO MAANA YANAAMBIWA "PIGA TU"
 
Kwa nini nyie chadema msieandae mazingira chanya yatayomshawishi Zitto aombe msamaha badala yake mnafanya maamuzi kwa mihemko ya kisiasa na sifa kwa public.Hii ni mbaya hasa kwa sasa ambako tunaelekea kwenye uchaguzi na tunahitaji nguvu moja iliyoimara,sisi wananchi tunaamini kwama Ukawa inaweza chukua nchi vizuri tu(tathimini:matokea ya serikali za mitaa ambayo ndo msingi wa ushindi wa ccm) ila nashangaa tena Zitto yupo na kiongozi mkubwa wa Ukawa huko kigoma alishawahi kwenda mtwara na Pro Lipumba. Je hii inaashiria nini kwa Uhai wa Ukawa?.Jamani Zitto anahitaji kufanya maamuzi sio magumu bali sahii basi Chadema mlioshika upini fanyeni na nyie kwa nafasi yenu maamuzi yatakayomfanya Zitto aone pia kwamba kuna uhalisia kwa kufanya 1 na 2 kwa maslahi ya chama na wana kigoma,kwani wazee wa chama si wapo,vijana wenzake wa chadema(halima mdee,mnyika,sugu na hata kafulila chini ya ukawa) hamuwezi watumia hawa kwa manufaa ya chadema jaman.Kumpuuza Zito ni kupuuza kura za kigoma kwa na watu wengine makusudi kabisaa,kama tumeweza kuwarudisha wakina Kafulila chini ya mwavuli wa ukawa Zitto ni nani hasa na kwa sababu gani hasa asirudishwe hata sio chamani ila ilimradi kura zisiende ccm wananchi tunataka mapinduzi halisia na visible ila hizi propaganda zinaturudisha nyuma kabisaa.

stanlthecreator,

Nimekusoma sana.Siko mbali na mtazamo wako...
 
Last edited by a moderator:
Inasemekana Atagombea Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT.
Lakini Zitto ni mtu kigeugeu sana, moja ya kauli zake tata ni hizi hapa.
1/Wakati wa uchaguzi mkuu wa 2010 akiwa kigoma hapo hapo alitangaza kuwa mwaka 2015 atagombea Urais.
2/Aliwahi kusema mara kadhaa kuwa atakuwa mtu wa mwisho kuondoka CHADEMA.
3/Mara kadhaa amewahi kusema kuwa kipindi hiki ndio cha mwisho kuwa mbunge, baada ya hapo 2015 ataachana na siasa na kwenda chuo kikuu kwenda kufundisha.

*Kwa sasa amekuwa akiimba chorus "Mwezi March nitafanya maamuzi magumu juu ya hatma yangu ndani ya CHADEMA" lakini karibu kila mtu anajua atahamia ACT, bahati mbaya sana CHADEMA wamemuwahi kwa kumvua uanachama.

Nimetokea kumdharau sana Zitto.
 
Zitto umewafanyia watanzania kazi kubwa. Umefichua ufisadi mkubwa

Hata wakutukane wakutemee mate ila kazi Umefanya.
ufisadi gani ameibua zito?

Au mnadhani ripoti za CAG ni ripoti zake
 
Last edited by a moderator:
Zito kajimaliza mwenyewe, yeye aangalie utaratibu mwingine wa maisha na si vinginevyo.
 
Taasisi yeyote ili iaminike ni lazima iwe na utamaduni wa kuamua!! Ikulu ya JK imeshindwa mtihani huu!! CDM isiyumbishwe na wahuni wanaolelewa na kunufaika na mfumu uliokufa wa CCM na IKULU yake.

CDM mkirudi nyuma katika maamuzi yenu mtawakwaza Watanzania ambao wamewapa Vitongoji na Mitaa mingi kwa sababu mbalimbali; Sababu kubwa ikiwa Mkakati wenu mliouanza wa kuwajibishana Mamluki bila uwoga. Endeleeni hivyo hivyo mpaka hapo CCM nao watakapogutuka na kuiga mfano wenu!

Mkuu kwa kuwa mkweli, Nimejiunga na Chadema juzi baada ya kujuwa hakuna Mambo ya kulindana.
 
Kwa mtu yeyote makini, atagundua kuwa huyu jamaa, anatafuta kuhurumiwa, sisi watu wa MARA, tunaamini, tumezaliwa Siku Moja, na tutakufa siku moja, ukitaka kufanya jambo lolote huhitaji kutangazia watu, kama ni uamuzi amua ijulikane.
Zito hana tofauti na mtu anayetaka kujiua kwa sumu, ananunua sumu na kusubiri chenji. Very STUPID.

Ama kwa hakika unatoka mara.. Hahahahahhah.... kwahiyo mkuu ukinunua sumu ni nduki kali kwenda kukoroga na kumeza!! Umeniacha hoi ndugu yangu Urgent..... kunamwingine alidai ni sawa na mtu aliyekwenda msituni kujinyonga, akakutana na Simba na kutimua mbio kali huku akipiga mayowe mamaweeeeee na kamba yake mkononi huku akiwa na karatasi la wosia lililoandikwa tayari......!!!!!!

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Taasisi yeyote ili iaminike ni lazima iwe na utamaduni wa kuamua!! Ikulu ya JK imeshindwa mtihani huu!! CDM isiyumbishwe na wahuni wanaolelewa na kunufaika na mfumu uliokufa wa CCM na IKULU yake.

CDM mkirudi nyuma katika maamuzi yenu mtawakwaza Watanzania ambao wamewapa Vitongoji na Mitaa mingi kwa sababu mbalimbali; Sababu kubwa ikiwa Mkakati wenu mliouanza wa kuwajibishana Mamluki bila uwoga. Endeleeni hivyo hivyo mpaka hapo CCM nao watakapogutuka na kuiga mfano wenu!



Kwa akili yako unafikiri viti ilivyopata Chadema ni kwa sababu ya kufikuzana?
UKAWA ndiyo iliyokua imeipaisha Chadema .
tena ni kwa sababu CUF ina viongozi waliokomaa kisiasa na wasioa na papara lakini kushirikiana na chama kama CHADEMA ni kazi sana.
 
nasikia amewaambiwa wananchi hatogombea ubunge safari hii lakini bado hajabainisha atafanya nini kama hagombei

mna ushabiki wa kishamba ninyi mnashidwa hata kutumia akili zetu yaani watakacho kisema viongozi wa chadema ninyi kazi yenu ni kusema ndio mzee hamwezi hata ku argue
 
Hakuna Uamuzi Mwingine Mgumu ambao ni makini anaopaswa kufanya zaidi ya Kuomba Radhi kwa wapenzi na wanachama wa CHADEMA na kusonga mbele

Kwenda chama Kingine itakua uamuzi mgumu lakini sio makini

Acha unafiki wewe si ndo chanzo cha zito kufukuzwa
 
Habari za ndani kabisa kutoka kwenye vyanzo vyetu vya uhakika ni kuwa mwanasiasa mahiri zitto Zuberi Kabwe yu mbioni kujiunga chama cha wanainchi Cuf, na ndie atakae simama kugombea jimbo la kigoma mjini kwa tiketi ya ukawa, na baadaye kukabidhiwa nafasi ya uenyekiti ambapo mwenyekiti wa cuf prof Lipumba hatogombea tena nafasi hiyo, ambapo kipindi hiki cha miaka 3 kitakuwa ni kipindi cha kumuandaa kuelekea kushika uenyekiti wa chama hicho, ni hivi punde tu ambapo mh zitto na prof Lipumba walifanya ziara mkoani mtwara baada ya kumaliza mazungumzo na viongozi wa kitaifa wa Cuf.
 
Too late and too low.
Maamuzi ya nini tena wakati ameshafukuzwa CHADEMA? Kama kumwaga, CHADEMA walianza kumwaga mboga, Zitto akaendelea kusita kumwaga Ugali, CHADEMA juzi wamemwaga na ugali kabisa. Sasa hakuna msosi tena. Zitto kwisha habari yake kabisa.

CHADEMA juzi walifanya nini? mmeambiwa Lisu aliueleza umma kilichomo katika katiba ya chama chao. Hakuna kikao wala tamko rasmi la chama kuhusiana na uanachama wa ZZK zaidi ya maelezo juu ya katiba kuwa jamaa ni sawa na kuwa ameshajifukuza uanachama. Mpka sasa kwa mujibu wa katiba ya chama cha Zito hatambuliki kama mwanachama
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom