Zitto: Nina sharti moja tu kurudi CHADEMA

Zitto: Nina sharti moja tu kurudi CHADEMA

Kwenye ukweli lazima tuseme,Tangu waondoke akina Zitto CHADEMA imeonekana kupoteza mwelekeo,Kinapoteza mvuto kwa wananchi na viongozi wengi hawana mvuto kwa wananchi,Angalau Dr Slaa wanamsikiliza lakini hawa wengine ni wepesi mno kisiasa.Zitto bado anakubalika na watu wengi hasa maeneo ya mbali na mijini ambapo ndipo kuna wapiga kura wengi ambao wanampenda mtu na sio chama.Zitto arudishwe chamani haraka na wala hili swala haliitaji mjadala.

😱 hii ni amri kutoka mahakamani ama kwako? Mijitu mingine ni maescro jike
 
Ni lazima Mhe. Zitto arudi CDM. Huyu ni muhimu ktk mageuzi ya kisiasa hapa Tanzania. Ni muhimu sana kuwa ndani ya UKAWA ndani ya CDM.
 
Media zitamuharibia Zaidi Zitto asipokuwa makini... Ile Taarifa ya Upelelezi dhidi yake ilikuwa na ukweli mtupu 100%, mikakati yao dhidi ya CHADEMA akiwatumia Shonza, Mwampamba et al unajulikana... Fedha kutoka CRDB hadi Ujerumani na kurejea kwake na kasha kuzitawanya via Mpesa, Tigo Pesa zinajulikana...

Ada ya MJA hunena Uungwana ni vitendo... Aombe msamaha kiutu uzima, then awekwe under probation ... then afanye juhudi za makusudi kukijenga chama ...

akili kama hizi zitatawaliwa na CCM na kuishia vizazi vyenu kutengeneza ma house girl n ma house boys milele!
 
I am not on your level, how could you understand me?

Haswaa!!kweli,mimi si kiwango chako hasa tunapojikita kudadavua dhana susuavu za kitaifa.
Maliza CHEKECHEA kwanza,ndiyo
urudi JF.
JAMBO JAMBO TOTOOOO......??
 
Haswaa!!kweli,mimi si kiwango chako hasa tunapojikita kudadavua dhana susuavu za kitaifa.
Maliza CHEKECHEA kwanza,ndiyo
urudi JF.
JAMBO JAMBO TOTOOOO......??

Kati yangu ninayeongelea a Tanzanians constitutional rights na wewe usiyezielewa hizo rights nani anahitaji kurudi chekechea?
 
Chadema iliwafukuza akina Shonza na Mwampamba ikamwacha Henry Kilewo. Huyu naye ni kirusi kingine ndani ya Chadema. Anatafuta umaarufu kwa kuendesha majungu dhidi ya watu wengine. Kilewo ndiye alisuka mkakati mzima wa kumchafua Zitto Kabwe. Chadema wangejua mbaya wao ni nani, mgogoro usingetokea hata kidogo!
 
Chadema iliwafukuza akina Shonza na Mwampamba ikamwacha Henry Kilewo. Huyu naye ni kirusi kingine ndani ya Chadema. Anatafuta umaarufu kwa kuendesha majungu dhidi ya watu wengine. Kilewo ndiye alisuka mkakati mzima wa kumchafua Zitto Kabwe. Chadema wangejua mbaya wao ni nani, mgogoro usingetokea hata kidogo!

Mchukue zitto kwenye chama chako
 
Mchukue zitto kwenye chama chako

Ili mbaki na mpiga majungu Kilewo siyo?! Alichokifanya kwa Zitto atafanya kwa mwingine pia. Dhambi hiyo haitaishia hapo, itaendelea Itachukua muda CDM kujua ukweli lakini utajulikana tu.
 
Kumbe mahakama ilitoa amri kwa chadema kutomjadili zitto ndio maana mpaka leo ni mbunge! Oooh kumbe mahakama inaheshimika sometimes!
Mahakam Kuu ni chombo cha mwisho kutoa Uamuzi hata Serikali inaogopa Mahakam Kuu hujuwi mambo ya sheria wee nini unanitaka
 
Last edited by a moderator:
Kwani Zitto si aliituhumu CHADEMA kumbagua kwa dini na kanda yake?

Sasa Zitto amebadili dini au amefuta hiyo kauli yake? Je Zitto amekana uzawa wake wa Kigoma na amekuwa wa Kaskazini?

Tusiwe na kumbukumbu fupi.

Daima Zitto ni mwepesi kukanusha mambo yote yanayopotoshwa kumhusu yeye kwenye mitandao ya jamii na hata humu JF, na hatujaona akikanusha haya.

Hatua ya kwanza aanzie kukanusha haya.

My take:
CHADEMA ilifikiriwa itakufa bila Zitto. CHADEMA imeendelea kuwepo na imekabili vema sana changamoto zake.

Zitto bila CHADEMA hajielewi atasimama wapi kisiasa.

Move hii ya Zitto ni kutaka kuifufua nyota yake ya kisiasa na si kwa ajili ya kufanya harakati za kujenga chama kama anavyotuaminisha.

Zitto haaminiki tena.

cc: Ruttashobolwa
 
Last edited by a moderator:
Kwani Zitto si aliituhumu CHADEMA kumbagua kwa dini na kanda yake?

Sasa Zitto amebadili dini au amefuta hiyo kauli yake? Je Zitto amekana uzawa wake wa Kigoma na amekuwa wa Kaskazini?

Tusiwe na kumbukumbu fupi.

Daima Zitto ni mwepesi kukanusha mambo yote yanayopotoshwa kumhusu yeye kwenye mitandao ya jamii na hata humu JF, na hatujaona akikanusha haya.

Hatua ya kwanza aanzie kukanusha haya.

My take:
CHADEMA ilifikiriwa itakufa bila Zitto. CHADEMA imeendelea kuwepo na imekabili vema sana changamoto zake.

Zitto bila CHADEMA hajielewi atasimama wapi kisiasa.

Move hii ya Zitto ni kutaka kuifufua nyota yake ya kisiasa na si kwa ajili ya kufanya harakati za kujenga chama kama anavyotuaminisha.

Zitto haaminiki tena.

cc: Ruttashobolwa

"ukawa ni wasakatonge"zitto kabwe
 
Last edited by a moderator:
hiyo ndio shida. kwa mbowe cdm ni kama kampuni mwenye hisa nyingi ndio kiongozi.
Na Zitto ni lazima awe mwenyekiti wakati anapotaka yeye, na akikosa afanye bidii kuua chama! Kwake subira hamna! Ndio uzalendo ati!!!

Kwangu mimi mwanachama wa hivyo ni hatari mno! Mtu aliye tayari kuua chama pale matakwa yake yasipotimia! Ni nyoka mbaya huyo!
 
Hata Mama mzazi wa Zitto - Marehemu Mama Shida Salum alisikika akisema kuwa mwanae anatumika kuhujumu chama.

November 19, 2009 Gazeti la M W A N A H A L I S I

SHIDA Salum, mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Zitto Kabwe, ameibuka na kusema mwanaye anatumiwa kukivuruga chama chake.
Akizungumzia taarifa zinazoandikwa na baadhi ya magazeti kuhusu kinachoitwa mgogoro wa uongozi katika CHADEMA, kati ya Zitto na viongozi wenzake, Shida alisema, "hakuna mgogoro pale, kuna kikundi cha watu wanaotaka kumtumia mwanangu kufanikisha mambo yao."
Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam, alidai kuna watu walio nje ya CHADEMA wanakula njama za kumgombanisha mwanawe na viongozi wenzake.
Alisisitiza, "kuna baadhi ya wanasiasa ndani ya CHADEMA wanaotumiwa na walio nje kugombanisha viongozi."
Akaongeza, "Mambo ya uchaguzi yalikwisha kitambo na Zitto kwa moyo mmoja alikubali kumaliza tofauti zake na Mbowe (Freeman Mbowe) ndiyo maana akamuacha Mbowe kuwa mgombee pekee wa uenyekiti."
Shida aliwatuhumu watu walio nje ya CHADEMA akisema ndio wanaopandikiza mbegu za chuki kwa lengo la kuwavuruga. Hata hivyo, hakuwataja.
Alisema kila mwenye akili timamu anajua kinachotafutwa, na nani mkweli na yupi anasingiziwa.
"Angalia wanaoandika haya. Kweli Zitto anaweza kutetewa na magazeti ya Habari Corporation yanayomilikiwa na Rostam Aziz halafu ukaamini kile kinachoandikwa?" alihoji.
Aliongeza, "Rostam yupi? Ni huyu tunayemjua au mwingine? Kwa wema upi alionao kwa chama chetu."
Wiki iliyopita magazeti ya Rai na Mtanzania yalinukuu taarifa zikidai kuwa zimetolewa na Shida, kwamba anataka mwanawe aondoke kwenye chama hicho kwa kile ilichoeleza kuwa "kumwepuesha na yaliyomkuta Chacha Wangwe."
Katika kujibu hilo, Shida anasema, "Mimi na Zitto tunajua katiba ya chama chetu. Tunafahamu taratibu za kuendesha chama. Yeye ni naibu katibu mkuu, mimi ni mjumbe wa Kamati Kuu. Tunajua nini maana ya uongozi, hivyo hatuwezi kukurupuka barabarani.
"Kwamba kama kuna malalamiko au tuhuma mathalani juu ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum, basi sote ni sehemu ya hicho kinacholalamikiwa. Kutokana na hali hiyo, hatuwezi kujifanya hatuhusiki na tukatuhumu kupitia vyombo vya habari, tena magazeti yanayomilikiwa na mwanachama wa CCM."
Shida alisema anajua kwa mapana chanzo cha yote yanayoandikwa na jitihada za kutaka kumgombanisha Zitto na viongozi wenzake, hasa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.
"Yote haya tunafahamu chazo chake. Si uchaguzi wa ndani ya chama. Uchaguzi ulishakwisha na Zitto kwa moyo mmoja alikubali kumuachia Mbowe uenyekiti ili kulinda maslahi ya chama," alisema.
Alisema kuwa yeye kama mlezi, hawezi kuruhusu hali hiyo, hivyo atatumia nafasi yake ya mjumbe wa CC kuhakikisha kwamba tabia hiyo ya kugombanisha viongozi inakoma.
"Nikiwa mzazi, mlezi na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, siwezi kuruhusu Zitto kutumika kuingiza chama katika mgogoro. Nitasimama imara kuhakikisha kwamba CHADEMA inakuwa salama," alisema.
Wiki iliyopita, Dk. Slaa aliwaondoa katika nafasi za utendaji David Kafulila aliyekuwa Afisa Habari na Danda Juju aliyekuwa Afisa anayeshughulika na Halmashauri na Bunge kwa kile kinachoelezwa kuwa utovu wa nidhamu kwa chama na viongozi wake.
Kafulila alinukuliwa na baadhi ya magazeti kuwa alibeza kikao cha viongozi wa juu wa chama hicho kilichofanyika Dodoma ambapo Mbowe na Dk. Slaa walikutana katika kikao cha kawaida na wabunge wa chama hicho na baadhi ya wakurugenzi.
Kafulila alisema mkutano huo wa viongozi haukuwa na maana; na alifika mbali zaidi kwa kuufananisha na vikao vya geto. Ni matamshi hayo na mengine yaliyomfanya Dk. Slaa kutumia mamlaka yake ya kikatiba kumuondoa Kafulila katika wadhifa huo.
Taarifa zinasema hoja ya kumuondoa Kafulila katika kikao ilitolewa na Msafiri Mtemelwa, mmoja wa viongozi wake na ambaye alikuwa meneja wa kampeni za Zitto wakati wa kuwania uenyekiti wa CHADEMA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom