Kamanda kwenye maisha na siasa sio kila kitu kitapata majibu kama tutakavyo. Kama unaona unaweza kurudi kufanya kazi na CDM ni bora kurejea kwenye meza ya maridhiano bila masharti yeyote.
Mgogoro wa Israel na Palestina unashindwa kupata suluhisho la kudumu kwani pande zote hazikubali kwenda kwenye maridhiano bila masharti yasiyotekelezeka.
Mchawi hayupo zaidi ya wakati. Chama ni watu ambao wanakuja na kutoweka, kufa, kustaafu, kuhama, nk ukitaka majibu yote itakuwa ngumu.
Mtaji mkubwa wa mwanasiasa ni watu. Rudi fanyeni maridhiano , piga kazi andika kitabu weka ukweli wako wazi wacha tusome. Tutaamua. Ila ukitaka chama kikuombe msamaha, sasa mimi niliyeko huku ndandahimba nimekufanya nini? Wewe sema baadhi ya watu muombane msamha kwani kuna watu mlikoseana kibinafsi kwenye ule mgomvi. Ndio maana nakubaliana na msemo wa bakiza na akiba.
vuta pumzi rudi kazini. Ama unataka kuwa kama mandela bila sisulu hurudi?