Zitto: Nina sharti moja tu kurudi CHADEMA

Zitto: Nina sharti moja tu kurudi CHADEMA

Hata Mama mzazi wa Zitto - Marehemu Mama Shida Salum alisikika akisema kuwa mwanae anatumika kuhujumu chama.

November 19, 2009 Gazeti la M W A N A H A L I S I

SHIDA Salum, mama mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Zitto Kabwe, ameibuka na kusema mwanaye anatumiwa kukivuruga chama chake.
Akizungumzia taarifa zinazoandikwa na baadhi ya magazeti kuhusu kinachoitwa mgogoro wa uongozi katika CHADEMA, kati ya Zitto na viongozi wenzake, Shida alisema, "hakuna mgogoro pale, kuna kikundi cha watu wanaotaka kumtumia mwanangu kufanikisha mambo yao."
Akizungumza na gazeti hili juzi jijini Dar es Salaam, alidai kuna watu walio nje ya CHADEMA wanakula njama za kumgombanisha mwanawe na viongozi wenzake.
Alisisitiza, "kuna baadhi ya wanasiasa ndani ya CHADEMA wanaotumiwa na walio nje kugombanisha viongozi."
Akaongeza, "Mambo ya uchaguzi yalikwisha kitambo na Zitto kwa moyo mmoja alikubali kumaliza tofauti zake na Mbowe (Freeman Mbowe) ndiyo maana akamuacha Mbowe kuwa mgombee pekee wa uenyekiti."
Shida aliwatuhumu watu walio nje ya CHADEMA akisema ndio wanaopandikiza mbegu za chuki kwa lengo la kuwavuruga. Hata hivyo, hakuwataja.
Alisema kila mwenye akili timamu anajua kinachotafutwa, na nani mkweli na yupi anasingiziwa.
"Angalia wanaoandika haya. Kweli Zitto anaweza kutetewa na magazeti ya Habari Corporation yanayomilikiwa na Rostam Aziz halafu ukaamini kile kinachoandikwa?" alihoji.
Aliongeza, "Rostam yupi? Ni huyu tunayemjua au mwingine? Kwa wema upi alionao kwa chama chetu."
Wiki iliyopita magazeti ya Rai na Mtanzania yalinukuu taarifa zikidai kuwa zimetolewa na Shida, kwamba anataka mwanawe aondoke kwenye chama hicho kwa kile ilichoeleza kuwa "kumwepuesha na yaliyomkuta Chacha Wangwe."
Katika kujibu hilo, Shida anasema, "Mimi na Zitto tunajua katiba ya chama chetu. Tunafahamu taratibu za kuendesha chama. Yeye ni naibu katibu mkuu, mimi ni mjumbe wa Kamati Kuu. Tunajua nini maana ya uongozi, hivyo hatuwezi kukurupuka barabarani.
"Kwamba kama kuna malalamiko au tuhuma mathalani juu ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum, basi sote ni sehemu ya hicho kinacholalamikiwa. Kutokana na hali hiyo, hatuwezi kujifanya hatuhusiki na tukatuhumu kupitia vyombo vya habari, tena magazeti yanayomilikiwa na mwanachama wa CCM."
Shida alisema anajua kwa mapana chanzo cha yote yanayoandikwa na jitihada za kutaka kumgombanisha Zitto na viongozi wenzake, hasa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa na mwenyekiti wake, Freeman Mbowe.
"Yote haya tunafahamu chazo chake. Si uchaguzi wa ndani ya chama. Uchaguzi ulishakwisha na Zitto kwa moyo mmoja alikubali kumuachia Mbowe uenyekiti ili kulinda maslahi ya chama," alisema.
Alisema kuwa yeye kama mlezi, hawezi kuruhusu hali hiyo, hivyo atatumia nafasi yake ya mjumbe wa CC kuhakikisha kwamba tabia hiyo ya kugombanisha viongozi inakoma.
"Nikiwa mzazi, mlezi na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, siwezi kuruhusu Zitto kutumika kuingiza chama katika mgogoro. Nitasimama imara kuhakikisha kwamba CHADEMA inakuwa salama," alisema.
Wiki iliyopita, Dk. Slaa aliwaondoa katika nafasi za utendaji David Kafulila aliyekuwa Afisa Habari na Danda Juju aliyekuwa Afisa anayeshughulika na Halmashauri na Bunge kwa kile kinachoelezwa kuwa utovu wa nidhamu kwa chama na viongozi wake.
Kafulila alinukuliwa na baadhi ya magazeti kuwa alibeza kikao cha viongozi wa juu wa chama hicho kilichofanyika Dodoma ambapo Mbowe na Dk. Slaa walikutana katika kikao cha kawaida na wabunge wa chama hicho na baadhi ya wakurugenzi.
Kafulila alisema mkutano huo wa viongozi haukuwa na maana; na alifika mbali zaidi kwa kuufananisha na vikao vya geto. Ni matamshi hayo na mengine yaliyomfanya Dk. Slaa kutumia mamlaka yake ya kikatiba kumuondoa Kafulila katika wadhifa huo.
Taarifa zinasema hoja ya kumuondoa Kafulila katika kikao ilitolewa na Msafiri Mtemelwa, mmoja wa viongozi wake na ambaye alikuwa meneja wa kampeni za Zitto wakati wa kuwania uenyekiti wa CHADEMA.
Kwa nini Zitto hakukanusha habari hizo zilizokuwa zikiandikwa kwenye magazeti ya Rostam Aziz?
 
Thanx to the ALMIGHTY.....
ZZK tulimtetea tukaishia kutukanwa. Kuleni matapishi na uharo wenu. Tulipowaambia nguvu ya kiakili ya zzk ni zaidi ya MARA 1000000 YA MBOWE NA WAFUASI WAKE WAKICHANGANYWA mkatubishia.
Masharti ya zzk ni ya msingi sana lakini utekelezaji wake ni majuto kwa vibaraka.
Maana anaposema"""waliomtuhumu kuwa anatumiwa na ccm walete uthibitisho na wakishindwa wachukuliwe hatua"""
Hii ina maana LISU,LEMA, MNYIKA,BEN SAANANE, MNAFIKI YERICKO NYERERE na vifaranga wengine watafute kimbilio.
.......acha movie iendelee..........
 
Ni lazima Mhe. Zitto arudi CDM. Huyu ni muhimu ktk mageuzi ya kisiasa hapa Tanzania. Ni muhimu sana kuwa ndani ya UKAWA ndani ya CDM.

hata mageuzi anaweza kuyafanya akiwa ACT na kukiingiza chama chake hicho kwenye umoja wa UKAWA, haishindikani mbona NLD wapo.

opportunist wa hali ya juu kiasi hiki akitumia hoja ya mbunge Kafulila na uenyekiti wa PAC kumhuisha kisiasa anachostahili ni chama chake mwenyewe
 
Thanx to the ALMIGHTY.....
ZZK tulimtetea tukaishia kutukanwa. Kuleni matapishi na uharo wenu. Tulipowaambia nguvu ya kiakili ya zzk ni zaidi ya MARA 1000000 YA MBOWE NA WAFUASI WAKE WAKICHANGANYWA mkatubishia.
Masharti ya zzk ni ya msingi sana lakini utekelezaji wake ni majuto kwa vibaraka.
Maana anaposema"""waliomtuhumu kuwa anatumiwa na ccm walete uthibitisho na wakishindwa wachukuliwe hatua"""
Hii ina maana LISU,LEMA, MNYIKA,BEN SAANANE, MNAFIKI YERICKO NYERERE na vifaranga wengine watafute kimbilio.
.......acha movie iendelee..........

Hujui ukisemacho wewe..

Unadhani Chadema ni sawa na banda lako la kuku..
 
hata mageuzi anaweza kuyafanya akiwa ACT na kukiingiza chama chake hicho kwenye umoja wa UKAWA, haishindikani mbona NLD wapo.

opportunist wa hali ya juu kiasi hiki akitumia hoja ya mbunge Kafulila na uenyekiti wa PAC kumhuisha kisiasa anachostahili ni chama chake mwenyewe

Nimekusoma katikati ya mstari Kamanda..

Unaonekana una uchungu mkubwa na chama chako.
 
Thanx to the ALMIGHTY.....
ZZK tulimtetea tukaishia kutukanwa. Kuleni matapishi na uharo wenu. Tulipowaambia nguvu ya kiakili ya zzk ni zaidi ya MARA 1000000 YA MBOWE NA WAFUASI WAKE WAKICHANGANYWA mkatubishia.
Masharti ya zzk ni ya msingi sana lakini utekelezaji wake ni majuto kwa vibaraka.
Maana anaposema"""waliomtuhumu kuwa anatumiwa na ccm walete uthibitisho na wakishindwa wachukuliwe hatua"""
Hii ina maana LISU,LEMA, MNYIKA,BEN SAANANE, MNAFIKI YERICKO NYERERE na vifaranga wengine watafute kimbilio.
.......acha movie iendelee..........
Kwa hili Zitto hatafutwi na CHADEMA ili arudishwe. CHADEMA haimhitaji Zitto, na imekabili changamoto zilizosababishwa na Zitto vizuri tu na imepita salama.

Zitto ndio anatafuta kurudi CHADEMA kwa kuwa amekosa platform ya kutafutia umaarufu wake.

Hakuna hata kiongozi mmoja wa CHADEMA aliyeongelea kumhitaji Zitto, bali ni viongozi wa CCM wanashinikiza Zitto arudi CHADEMA kwa kuwa his mission is not yet accomplished....

Zitto is motivated by selfishness and personal motives!
 
Na ndiyo maana huwa ninawashangaa wendawazimu wanaodhani Chadema inaweza kumpigia magoti mtu yeyote na kulamba miguu yake

Watu hawaelewi mfumo ndani ya Chadema jinsi ulivyo.Wanafananisha Chadema na baadhi ya vyama vikaragosi vya CCM
 
[h=2]Re: Zitto: Nina sharti moja tu kurudi CHADEMA [/h]
chadema bila zitto hawawezi kujiendesha kabisa hata iweje tulisema kitambo kwamba watampigia magoti tu.

kumbe si hata muhongo mnasema wizara haiengi bila yeye maskini nchi yangu TANGANYIKA
 
Playboy politics of Tanzania,Kasungura kamestukia upepo unapoelekea,yuko radhi kulamba matapishi yake mwenyewe
 
Kwa hili Zitto hatafutwi na CHADEMA ili arudishwe. CHADEMA haimhitaji Zitto, na imekabili changamoto zilizosababishwa na Zitto vizuri tu na imepita salama.

Zitto ndio anatafuta kurudi CHADEMA kwa kuwa amekosa platform ya kutafutia umaarufu wake.

Hakuna hata kiongozi mmoja wa CHADEMA aliyeongelea kumhitaji Zitto, bali ni viongozi wa CCM wanashinikiza Zitto arudi CHADEMA kwa kuwa his mission is not yet accomplished....

Zitto is motivated by selfishness and personal motives!

Bac mapambano yaendelee! tutapata majibu baadae maana huyu ni mwanasiasa mwenye uwezo mkubwa na umri wake bado unamruhusu ku struggle! isilete shida kwenye vichwa vyenu humu mitandaoni tutaifahamu hii sinema mwisho wake!hahahaha acha movie iendelee!
 
Msikie mhafidhina huyu!

Naomba kuweka wazi...

Hakuna aliye juu ya chama.Kuna watu wanatafuta kutaka kuwa maarufu kuliko chama.

Zitto akitaka kurudi Chadema anapaswa kuomba radhi ajutie makosa yake na huu ndiyo msimamo rasmi.

Katiba ya chama iko wazi.Kukipeleka chama mahakamani ni kujifukuzisha mwenyewe ndani ya chama.
 
Baada ya muungano wa ukawa kundwa pale jangwani miezi kadhaa iliyopita, zitto alitoa maoni kuhusu umija huo na mantiki yake na aliufanaisha umoja huo unaoundwa na nld, nccr , cuf an chadema na wasakatonge.toleo la gazeti la ijumaa iliyopitalilimnukuu zitto akieleza jinsi alivyowamiss wana ukawa yaani chadema, nccr, cuf na nld na kwamba anatamani kusuluhisha mgogoro wake ndani ya chamdema ili aweze kushiriki harakati za ukawa ambao awali aliwaita wasakatonge.je?zitto naye anataka kuwa msakatonge?
 
Naona anataka kuungana na wahafidhina
 
Ripoti ya CAG hesabu za ccm cdm zote zina mapungufu. Hebu kupuka kidogo habari ya PAC na hessabu za cdm
 
Tena sio tu pekee Zitto kurudi bali tunataka pia na Kafulila, Moses Machali na Felix Mkosamali wote warudi CHADEMA, Siasa ni pamoja na kusamehana kwa maslai mapana ya taifa.

Naomba viongozi wangu wa CHADEMA taifa, wasikie kilio cha sisi wanachama wao.

Mnatakiwa kwanza mseme sababu za wao kuundiwa zengwe na kuondoka manake chama kimebaki na wapiga kelele wasiojua kujenga hoja wametawaliwa na fujo na matusi wakina Wenje,Sugu,Lema ,Msigwa n.k then ndiyo wao watafikiria na kurudi kwenu,Chama cha watu fulani kwa masilahi ya watu fulani.Mkumbuke maudhuhi ya ule waraka msijifanye mmesahau "Akili ndogo haiwezi kuongoza akili kubwa" sasa sijuhi kama wataweza kukubali kuja kuongozwa na akili ndogo
 
Kwa nini mwenye akili kubwa asiende kwingine ang'ang'anie CHADEMA? Au akili kubwa haiwezi kuanzisha chama na kikafanikiwa?

Kwa nini arudi kwa Wahafidhina? Au wameacha kuwa wahafidhina?

CHADEMA imeendelea kuwepo pamoja na hujuma za wazi za Zitto. Zitto amekosa jukwaa mujarabu la kufanyia siasa ndio maana anataka kurudi.

Kumbuka ni Zitto anayetafuta kurudi CHADEMA na si CHADEMA inayomtafuta Zitto!
 
Watu tuwe serious Zitto anaweza wekea masharti CHADEMA?

Jamani, humu Jf nadhani kuna watu hawaelewi kabisa. Hapa ndani ya statement ya mleta uzi ukiisoma vizuri unagundua kwamba mashaka makubwa yako kwa viongozi dhidi ya zitto. Siya Chadema dhidi ya Zitto. Sasa kama michakato ya kumchafua Zitto ilifanywa na viongozi wetu wa chama basi viongozi hao wanawajibika kumaliza migogoro ili turudi kuwa kama jumuia moja.

Kuendekeza migogoro hakukiendelezi chama hata kidogo, kwa chama kinachokuwa kwa kasi kupoteza hata mjumbe mmoja ni hasara kubwa.

Wakae meza moja na kumaliza mitafaruku.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom