Kwanza na-declare interest: Mimi ni mmoja wa watu niliokuwa nikimshambulia Zitto. Mimi nilitumia sana habari nilizosoma magazetini ambazo kwa kweli zilinishawishi na kuridhika kwamba Zitto alikuwa akitumika kuihujumu CHADEMA.
Lakini mimi ni mtu mwenye kupenda kusamehe na kusameheana. Zitto aliomba Ushahidi tuliokuwa tukimtuhumu nao, lakini mpaka leo hatujaleta Ushahidi. Damn you, Ushahidi, hata kama upo naomba tutupilie mbali mambo hayo tusameheane na tusonge mbele. Sana sana itaturudisha nyuma kwenye mparurano.
Nakumbuka wakati Zitto anafukuzwa alishambuliwa sana na aliumia sana. Jambo moja nililomsifu ni busara: Kukaa kimya na kusubiri ukweli. Aliweka akiba ya maneno kama alivotushauri Mzee Sheikh Thabit Kombo. Big up sana Zitto.
Jaribu kusahau tulivokushambulia na utusamehe. Wapo waliokushambulia binafsi (kama mimi) na wale waliokushambulia kwa niaba ya chama kama Tundu Lissu. Hayo ni mapito huenda ambayo yalipandikizwa na watu wa CCM kuweka mazingira flani kutushawishi kwamba wewe unatumika, ili tukufukuze, tusambaratike. Tulianza na Mungu, na bado aliendelea kutuunganisha. Mungu huyu huyu, ndo akaleta sakata la escrow ambalo umelishughulikia kiume kweli kweli. Nililia machozi uliposema "I missed the movement...". Kubwa zaidi niliona hata kina Mbowe na Lissu ambao najua kimsingi huna ubaya nao, walionyesha kukukubali.
Huu uwe ni mwanzo wa kusameheana. Naomba Zitto urudi nyumbani, najua uliumia sana, lakini samehe, achana na mambo ya Ushahidi. Wasamehe waliokushambulia na urudi tupige kazi tuindoe CCM 2015. WELCOME BACK BUDDY.​