Leo imeripotiwa kuwa Zitto Kabwe amesema kuwa ana sharti moja ili kurudi CHADEMA. Sharti lenyewe ni kuambiwa kosa lake ili ikibidi aombe msamaha hadharani. Habari hii na zinazofanana nayo ni upotofu mtupu.
Mosi,Zitto bado ni mwanachama wa CHADEMA. Hajawahi kuvuliwa au kufukuzwa uanachama wake. Alichopokwa ni uongozi ndani ya Chama chake na Bungeni,yaani Waziri Kivuli na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Mtu ambaye yuko CHADEMA anawezaje kutaka kurudi CHADEMA?
Pili,uongozi wa CHADEMA haujawahi kuutaarifu umma juu ya kumrejesha Zitto kundini. Angeombwa ndipo angekuwa na uwezo na nguvu ya kutoa masharti. Jambo hilo la kuombwa au kubembelezwa halipo.
Kwanini kuna upotofu kama huu? Nani mhusika? Kwa faida ya nani?