Zitto: Nina sharti moja tu kurudi CHADEMA

Zitto: Nina sharti moja tu kurudi CHADEMA

unaweza uthibitisha usalit wa ZZK au n maneno tu

RIPOTI YA SIRI JUU YA ZITTO KABWE
KWA
CHADEMA
UCHUNGUZI WA MWENENDO WA KISIASA WA ZITTO Z. KABWE
NDANI NA NJE YA CHADEMA.
UTANGULIZI:
Tangu mwaka 2008 mwenendo wa kisiasa wa Zitto Zuber Kabwe
ulianza kutiliwa shaka na wanachama wa CHADEMA ndani na nje
ya chama, Hili lilipelekea kuibuka maneno ya chini kwa chini kuwa
anakisaliti chama.
Hilo liliilazimu timu ya kijasusi ya chama kuanza kufuatilia nyendo
zake kwa ukaribu zaidi usiku na mchana ili kujiridhisha pasipo
kuacha chembe ya mashaka. Ifahamike kuwa chama kina idara ya
ulinzi na usalama wa chama na viongozi wake yenye uwezo wa
kufuatilia nyendo za majasusi wa nje na viongozi na wanachama
wake popote walipo kwa masaa 24. Baada ya kujiridhisha kuwa
mwenendo wake ni wa mashaka, bila kusita timu ya ujasusi ilianza
kazi rasmi ya ujasusi dhidi ya nyendo zote za Zitto Zuberi Kabwe
MAMBO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI DHIDI YA ZITTO KABWE.
Kumfuatilia yeye binafsi nyendo zake.
Kufuatilia mawasiliano yake ya simu.
Kufuatilia mawasiliano yake ya barua pepe.
Kufuatilia pato lake nje ya kazi zake halali za kibunge.
SEHEMU YA KWANZA 2008
Chombo chetu cha ujasusi tulichokipandikiza kwa siri katika
nyendo zote za Zitto Kabwe na ndani ya vikao vya mwanzo kabisa
vya Zitto na viongozi serikalini, nahata vile vikao muhimu vya
idara ya ujasusi ya chama cha mapinduzi (ccm), kinatupa fursa ya
kuweka msingi wa kuimarisha chama cha CHADEMA na kutenda
haki kidemokrasia kwa maslahi ya chama na Taifa kwa ujumla:
Mnamo Jumatatu ya tarehe 16/6/2008 saa 09:46 asubuhi, Mh
Zitto Kabwe kupitia simu yake ya kiganjani namba +2557547...50
alipokea simu kutoka kwa xxxxxxx mwenye namba
+255717...473 ambaye ni afisa Usalama wa Taifa anayefanya kazi
ikulu hivi sasa. Alijitambulisha kuwa yeye ni Usalama wa Taifa
ametumwa na mkuu wake wa kazi aje aongee na Zitto, Maelezo ya
msingi katika simu hii ilikuwa ni bwana xxxxxxx kuomba miadi ya
kuonana kutokana na agizo la mkuu wake wa kazi.
Siku sita baadae yaani Jumatatu ya tarehe 23/6/2008 saa 07:52
asubuhi, Zitto alipigiwa tena simu na xxxxxxx akimkumbusha
maongezi yao waliyo fanya siku 6 zilizopita na kumuomba siku
hiyo jioni waonane, ingawa Zitto alionekana kusita kidogo lakini
baadae alikubali, Walikubaliana wakutane Sea Cliff Hotel, ilipofika
jioni ya siku hiyo Zitto akiwa na marafiki zake wawili Omar Lyasa
na Abdalah Said walifika Sea Cliff Hotel wakaketi na kuagiza
vinywaji, Baada ya kama dakika kumi hivi Zitto alipokea simu
ikimuelekeza alipo bwana xxxxxxx kisha Zitto akawaambia
marafiki zake wamsubiri kidogo, akaondoka kuelekea aliko
elekezwa…..
Mashariki mwa lango kuu la kuingilia Sea Cliff Hotel mita kama
tatu tu kuna mlango mdogo unaoelekea kwenye vyumba maalumu
(VIP), chumba namba 8 ndicho Zitto alichokuwa anaelekezwa kwa
simu kuingia, chumba hiki kina meza moja na sofa zilizo zunguka
meza ile zenye uwezo wakukaliwa na watu watano hadi sita,
Ndani ya chumba kile Zitto anakutana na watu watatu ambao ni
Steven Wasira, xxxxxxx na Abdalla Punja.
Mazungumzo yao ndani ya chumba hiki yalianza maramoja,
akianza Mr xxxxxxx kueleza sababu za wao kumuita Zitto, kikubwa
ilikuwa ni "bwana Zitto, serikali (ikulu) inakutaka uache kuibana
na kuishurutisha hasa kwa hili suala la Buzwagi". Tunaomba
kujua shida yako kubwa ni nini?" xxxxxxx alihoji, Katika majibu
yake Zitto anajibu, "Mimi napigania haki za watanzania,
nimechaguliwa na wanakigoma na watanzania wameniamini ni
wawakilishe hivyo", Lakini mashambulizi ya ushawishi yalipozidi
Zitto alilegeza msimamo wake.
Katika kikao hiki kilichochukua masaa mawili, Zitto anaonekana
kusita sana na anaomba apewe muda akafikirie aliyoitiwa, wote
wanaafiki na kukubali ombi la Zitto na kikao kinaahirishwa.
Siku tatu tu baada ya kikao cha Hotel ya Sea Cliff, yaani tarehe
27/6/2008 Zitto anakutana na Naibu Mkurugenzi wa TISS Ndugu
Jack Zoka jijini Arusha, hiki sio kikao chao maalumu bali
wamekutana kwa mara ya kwanza wote wakiwa kwenye shughuli
za kitaifa, Katika mazungumzo yao wanaonekana ni watu
wanaofahamiana japo si kwa undani, Baada ya maongezi ya
dakika kadhaa wakiwa wamesimama, Mr Zoka alimuuliza "Vipi
vijana wangu walikupa ujumbe, umefikia wapi?" Zitto aliitikia kwa
kucheka na kusema "yap nipo tayari, lakini nihakikishieni usalama
wangu" Katika maongezi haya, Zoka anasikika akisema "Ondoa
shaka" Kisha Mr Zoka anamuagiza Zitto kuwa kesho kutwa yake
aende kwa Charles Kimei (Mkurugenzi CRDB Benki) pale Makao
makuu, atayakuta maagizo yake huko.
Tarehe 30/6/2008 majira ya saa 12:22 za alasiri, Zitto akiwa
ameongozana na kijana mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Rajabu
Abdala anaingia eneo la CRDB Benki mtaa wa Azikiwe, na kwenda
moja kwamoja kuonana na Bw Kimei, baada ya salamu
haikuchukua muda mrefu, Zitto akapelekwa katika moja ya
vyumba maalumu vya bank hiyo kwenye jengo hilohilo la Azikiwe,
baada ya kufika katika chumba hicho Zitto alihamaki kuwakuta
watu wawili katika chumba hicho, mmoja alikuwa ni mfanyakazi
wa bank hiyo aliyetambuliwa kwa jina la Maselina K. Kombe na
mwingine hakuwa mgeni machoni mwa Zitto, alikuwa ni xxxxxxx
yule wa TISS waliyekuwa naye kwenye kikao cha awali kule Sea
Cliff Hotel wiki chache zilizopita, Zitto alikabidhiwa Briefcase
nyekundu iliyokuwa imesheheni pesa halali za kitanzania kiasi
cha Shilingi milioni 250.
Wakati hayo yakitendeka yule kijana aliyekuja na Zitto alikuwa
kwenye gari aina ya Toyota Mark 11 No T 134 AAB yenye rangi
nyeupe na vioo vyeusi (Tinted). Baada ya makabidhiano
yaliyochukua kama dakika 10 tu, Mr xxxxxxx alimwambia Zitto,
"tunataka utulivu, mengi mazuri yanakuja utafurahia kijana," Na
kisha Zitto akatoka na begi lake (Briefcase) na kuingia nalo katiga
gari ile na kutokomea.
Uchunguzi umeonyesha kuwa pesa ile aliyokabidhiwa ndugu
Zitto, ilitoka katika akaunti Namba 0J56708968923 yenye jina la
Shani Maya, ambapo inaonyesha kuwa akaunti hii ilifunguliwa
CRDB tawi la azikiwe tarehe 25/6/2008 saa 10:14 asubuhi, kisha
tarehe 27/6/2008 iliingizwa kiasi cha pesa za kitanzania milioni
400. Na tarehe 30/6/2008 pesa hizo zilitolewa zote na akaunti hii
ilifungwa. Madhumuni ya pesa hii kutoka CRDB kwenda kwa Zitto
yanathibitishwa na kikao cha 23/6/2008 pale Hotel ya Sea Cliff
kuwa ni kupunguza kasi ya Zitto kuibana serikali hasa anapo
kuwa bungeni. Na kweli kasi yake iliyozoeleka kwenye kuibana
serikali akiwa bungeni ikapungua na kuweka msingi wa ujenzi wa
mashaka juu ya mwenendo wake wa kibunge.
SEHEMU YA PILI 2009
Mnamo Jumatatu ya tarehe 30/11/2009 saa 04:30 asuhuhi
wakati wa maandalizi ya uchaguzi wa mkuu wa 2010, idara ya
ujasusi ya ccm ilikutana kwa siri pale Moven Pick/SERENA Hotel,
ndani ya idara hii wakiwamo Jack Zoka, Wilson Mkama, Kingunge
Ngombale Mwiru, Jakaya Kikwete, Nape Nnauye, Fred Kimati,
Steven Wasira, xxxxxxx, Martin Palakyo, Mwigulu Nchemba,
Ahamed Msangi na Abdalla Punja. Katika kikao hiki yalijadiliwa
mengi sana, lakini kubwa lilikuwa nikukabiliana na vyama vya
upinzani hususani CHADEMA, zilipangwa mbinu nyingi sana juu
ya Chadema, Mbinu hizo ni kama ifuatavyo:
Kuwanunua wagombea ubunge na Udiwani (Mtakumbuka
wagombea wetu kadhaa walikuja kununuliwa na chama kina
ushahidi kwenye hili).
Kuwanunua VIONGOZI wajuu wa CHADEMA.
Kutumia TISS kutisha wagombea na wanachama wa Chadema (Hii
ilikuwa ni kuwakamata au kuvuruga mikutano).
Kuwaua baadhi ya wafuasi wa Chadema, viongozi wa Chadema na
wabunge.
Lakini walitilia mkazo zaidi njia ya kwanza ,ya pili na ya tatu
ambapo kikao kilijiridhisha kuwa mmoja wa VIONGOZI wa
Chadema ambae ni Zitto Kabwe ni mtu wao ambaye wamesha
anza kumtumia, kikubwa liandaliwe fungu tu kwa ajili yakuanza
mikakati yao, Waliafikiana mambo mengi kwaajili ya uchaguzi wa
mwaka ambao ungefuata, na wakakubaliana mambo kadhaa
ambayo walimuagiza Mr Zoka akamwambie Zitto nini cha kufanya
ili kupunguza nguvu ya upinzani.
Kwa upande wake Zoka alikiambia kikao kuwa Zitto
amemthibitishia kuwa yeye anawafuasi wakutosha ndani ya
chama ambapo watamuunga mkono kwa lolote hivyo kikubwa ni
pesa tu. Lakini kwanza kikao hicho kilimtaka Mr Zoka amwambie
Zitto kuwa taarifa zote zinazoihusu Chadema na za kila vikao vya
ndani vya chama zinatakiwa pia ziifikie timu hiyo ya kijasusi ya
ccm, pili walitaka Zitto apunguze ushiriki katika majukwaa ya
chama na shughuli nyingine za chama. Baada ya kikao sasa
ulikuwa ni utekelezwaji wa maadhimio yao.
Zoezi la kikao cha tarehe 30/11/2009 linaonyesha kuzaa
matunda hasa baada ya kubainika mawasiliano ya karibu sana
kati ya Zitto na Jack Zoka, Kwamfano: Jumamosi ya tarehe
6/12/2009 saa 03:43 asubuhi Zoka kupitia namba yake ya simu
+255756....35 alimpigia simu Zitto kupitia simu yake ya kiganjani
ambayo ni +2557547...50, wakati wa mawasiliano yao haya ya
simu Zitto alikuwa Tabata na maongezi yao yalihusu kikao cha
30/11/2009 na kile walichoamua timu ya kijasusi ya chama
(ccm) na matakwa yao kwa Zitto. Ndani ya maongezi yao
yaliyochukua dakika 68, Zitto anasema, "Mr kazi hii ni nzito, vipi
mmeongeza hela? Isije kuwa kama ile ya mwaka jana." Anajibiwa
na Zoka kuwa "ondoa shaka una dili na Jamhuri, hela sio tatizo"
Lakini zaidi Zitto anamshauri bwana Zoka kuwa utaratibu wa
uchukuaji wa pesa ubadilike, "Mr Jack ile staili ya uchukuaji pesa
kule CRDB mwaka jana ilinitisha kidogo halafu hii isije
ikabumburuka vyombo vya habari vipo makini kweli sasa hivi"
Anajibiwa na Bwana Zoka kuwa "Tunazo njia nyingi sana ambazo
si TAKUKURU wala polisi wanaoweza kubaini, tusikilize sisi,
tutakacho kuambia ujue ni salama, Haya Mr (Zitto) wewe
unayajua mazingira vizuri katika nchi moja ya Ulaya?, au unaweza
kutafuta mtu unae mwamini huko ili atumiwe yeye hiyo pesa na
awe wa kuaminika ili tumtumie kwa vipindi hivi vyote, kisha
uifuate huko au uangalie mwenyewe njia sahihi ya kuichukua
huko" Suala la kumpata mtu Ulaya lilionekana kama zito kidogo
kwa Zitto, kwani aliomba wawasiliane kesho yake ili awe na jibu la
uhakika.
Tarehe hiyo hiyo 6/12/2009 ya Jumamosi saaa 23:05 usiku, Zitto
kupitia simu yake ya mkononi namba +255754....50 , alipiga
namba +49157.....853, kimaongezi walionekana ni watu
wanafahamiana sana, alikuwa anaongea na
mwanamke ,waliongea mengi lakini kubwa lilikuwa ni Zitto
kuomba kupitisha hela yake kwenye akaunti ya huyu mtu.
Mwanamke huyu alihoji kama pesa hiyo ni nyingi na haina
madhara? Lakini alijbiwa sio nyingi na haina madhara kwakuwa
inatoka serikalini na chama tawala, Mwanamke huyo alizidi kuhoji
zaidi, "sasa vyombo vya dola vya hapa Berlin vikinihoji nitasema
nimepata wapi?" Anajibiwa kuwa "Darling huniamini? Nimesoma
na wewe na nimefanya kazi na wewe, lakini huniamini? Utasema
umelipwa nchini Tanzania kwa kazi yako", kisha katika maongezi
ya hapa na pale dada akakubali na baada ya dakika kumi
akamtumia akaunti namba 033B 33093101 Berliner Bank German.
Baada ya kuipata akaunti hii Zitto hakuchelewa, akaipeleka kwa
Mr Zoka kwa njia ya ujumbe wa maandishi (sms), baada ya dakika
5, Zoka akampigia simu Zitto kupitia namba +255756...535 nae
Zitto akapokea kupitia namba +255754....50, na mazungumzo
yao yaliyochukua dakika 6 yakaendelea, Zoka aliuliza swali kuwa
"Mwenye akaunti hiyo huko Ujerumani unamwamini na unamjua
vema?" Majibu ya Zitto yalikuwa "Ondoa shaka Mr Jack nafanya
kazi ya hatari na wewe , siwezi kukuangusha au kujiangamiza,
huyu mtu nimesoma nae na ninamfahamu in and out" Zoka
akajibu "ok".
Jumatano ya tarehe 16/12/2009 majira ya saa 13:12 za mchana
kwa Ujerumani akaunti namba 033B 33093101 Berliner Bank ,
ziliingizwa dola za kimarekani 266,000 pesa hizi katika
uchunguzi zimebainika kuwa zilitoka Tanzania katika Benki ya
NMB tawi la NMB House jiji Dar katika akaunti namba
2231604658 yenye jina la TSA, hii ni moja ya akaunti za siri za
TISS, ambapo wao ndio huzisimamia akaunti zao zote kwa
kutumia mawakala (TISS) walio ndani ya benki hiyo.
Kujiridhisha kuwa pesa hiyo ilifika Ujerumani, kunabainishwa na
mawasiliano ya barua pepe kati ya Zitto Kabwe na yule mwanamke
wa kijerumani aliyemtumia akaunti ya benki, anafahamika kwa jina
la Andrea Cordes, mawasiliano yaliyofanywa tarehe 17 alhamisi
saa 20:34 usiku ambapo Andrea kupitia barua pepe yake
acodes@gmail.com anamwandikia Zitto kupitia barua pepe ya
Zitto iitwayo zittokabwe@gmail.com , Andea anasema "Hey sweet,
mzigo yako imefika, can we talk?" Ujumbe huu unajibiwa na Zitto
saa 21:03 usiku huo kwakusema, "I'm so sorry my darling,
nimechelewa kukujibu, I will call you soon"
Saa 23:23 Zitto Kabwe kupitia simu yake ya kiganjani namba
+255754....50, alimpiga Andrea Codes kupitia namba
+491573...853, akimweleza kuwa anashukuru kwa mzigo
kumfikia, lakini anataka kumpa utaratibu wa kuichukua hiyo pesa,
ambapo alimweleza kuwa atakuwa anaichukua kidogo kidogo kila
mwezi kwa njia ya Western Union kuanzia dola 20,000 hadi dola
50,000, wakati huo Andea Codes atakula kamisheni ya dola
25,000.
Uchunguzi wa ndani umebaini pesa hiyo ilitumwa kwa Zitto ndani
ya miezi 8 kwa vipindi tofauti kupitia Western Union kama
alivyoomba, na alikuwa anachukulia maeneo tofauti tofauti hapa
jijini Dar, vilevile uchunguzi umebaini kuwa mwanamke huyu ni
Mjerumani aliyewahi kuishi Tanzania na amezaa mtoto mmoja
hapa Tanzania, Mwanamke huyu anaitwa Andrea Cordes, anaishi
Mechernich Ujerumani, mtaa namba 134, nyumba namba 141,
anafanya kazi UN Women Nationales Komitee Deutschland e.V.
Shirika ambalo shughuli zake huendeshea pia Tanzania. Katika
uchunguzi zaidi imebainika kuwa akaunti aliyomtumia Zitto ni ya
kwake binafsi, katika ushahidi tuliobaini kupitia benki iitwayo
Berliner Bank yenye Code No Hardenbergstraße 32, 10623 iliyopo
mjini Berlin nchini Ujerumani.
SEHEMU YA TATU 2010
Uhusiano usio wa kawaida na wa karibu wa Zitto na viongozi wa
ccm, serikali na wale wa Usalama wa Taifa uliendelea kushamiri
hasa kipindi cha kampeni na kipindi cha uchaguzi mkuu wa 2010,
Mfano tarehe 7/9/2010 siku ya jumanne saa 11:21 asubuhi,
Ahmed Msangi kupitia namba yake ya simu ya kiganjani
+2557842....4, alimpigia Zitto kupitia simu ya kiganjani namba
+255754....50 waliongea mambo mengi japo kwa muda mfupi, na
jambo kubwa lilikuwa ni "vipi kuna kipya ndani ya Chadema?"
Zitto alijibu "yapo mengi lakini hayana impact kwa ccm" Msangi
anajibu "Ok mr nikutakie siku njema"
Lakini mawasiliano ya simu yaliyochukua mda mrefu zaidi
yalikuwa kati ya Zitto na Zoka yaliyofanywa tarehe 10/9/2010
siku ya ijumaa saa 07:04 jioni na mazungumzo yao yalichukua
dakika 71, Mazungumzo haya yalifanywa wakati huo Zitto akiwa
katika hoteli ya Blue Pearl Ubungo, Mr Zoka alitaka kujua mambo
kadhaa kuelekea Uchaguzi mkuu, kwanza alimuuliza "Mr Zitto
umejiandaaje, una timu ya kazi?" Zitto akajibu "nipo fiti kiakili na
kimwili na nina timu ya kutosha, ondoa shaka juu yangu, kama ipo
hiyo hela tumeni tu Ujerumani kwenye ile akaunti, na ningeomba
kukutana na mwenyeti wenu (rais JK)" Zoka lijibu "hilo halina
tabu nitalifikisha sehemu husika bwana Zitto",
Uchunguzi umebainisha kuwa akaunti namba 033B 33093101
Berliner Bank ya German iliendelea kuingizwa pesa kwa nyakati
tofauti kutoka Tanzania kupitia NMB akaunti namba 2231604658
yenye jina la TSA ambayo ni moja ya akaunti za siri za .........
.................
............. ..............
 
Eti CCM mnaishauri Chadema Mtasubiri sana..
Twaweza wamtabiri Laaaabda 2015 wanaweza sogea kwenye Mawaziri
Lakini km itakuwa ni hii ya Wachagga na saccos yao (bila ya Zitto) HAWAPATI KITU alishatuasa JK Nyerere
 
Zitto kama hajui kosa lake ni tatizo.kama kweli ni mkomavu wa kisiasa awe tayari kuadmit makosa yake.chadema hakuna anayemchukia zitto yeye mwenyewe anajua ndio maana wote waliungana nae katika sakata la escrow.Chama kumuomba msamaha zitto ni kuwakatisha taamaa wale wote waliofanya kazi usiku na mchana kufichua mbinu chafu za zitto na wezanke katika kuharibu chama.nafikiri yeye anakihitaji zaid chama kuliko chama kinavyomuhitaji yeye
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    10.6 KB · Views: 226
Kauli yako ngumu ndugu.


Na kama atarudi, basi, ijulikane kuwa, walio mhukumu hawana upeo wa kuona umbali zaidi ya pua zao, haiwezekani ndani ya mda huu mfupi mkamrudisha mtu ambaye mmemchunguza kwa miaka isiyo pungua mitano na kuona hafai, na leo ghafla bin vu mseme arudi?

Kamati iliyo fanya maamuzi, kama ikimrudisha Zitto, basi inabidi ijipime uwezo wake kimtazamo.
 
Kwa kauli hiyo sioni nafasi ya muafaka. Upande mmoja lazima ukubali kuwa wenyewe ni wahifidhina, wabadhirifu na wana siasa za majitaka...

Anyway ndio wanasiasa wetu na siasa zao.


Duuu! Haya maneno yatakuwa yameeditiwa na hilo gazeti si maneno ya Zitto
 
Naomba kuweka wazi...

Hakuna aliye juu ya chama.Kuna watu wanatafuta kutaka kuwa maarufu kuliko chama.

Zitto akitaka kurudi Chadema anapaswa kuomba radhi ajutie makosa yake na huu ndiyo msimamo rasmi.

Katiba ya chama iko wazi.Kukipeleka chama mahakamani ni kujifukuzisha mwenyewe ndani ya chama.

Umenena sawa mkuu, chama kitaombaje ardhi? Kama anataka kurudi árudi bila agarró hata moja, hawezi, abajo huko huko.
 
hivi kweli mbowe na slaa watamruhusu zito agombee urais?? sidhani..bora zito uendelee kubaki huko huko
 
Siongelei haki ya mwanachama ndani ya CHADEMA.

Why should I do that? I am not CHADEMA.

Naongelea haki ya mwanachama kama

Kwa hiyo unadhani mahakama inaweza kulazimishia mtu abaki Chadema? Mahakama unaweza kuchagulia Chadema viongozi? Mahakama inaweza kututeulia wagombea Ubunge?

Mtasubiri sana..
 
Sioni muafaka kwa kauli hizi. Yeye aliitwa mamluki, msaliti na mengine mengi na yeye kaamua kuwaita wahifidhina, wabadhirifu na watukuzao siasa za maji taka.

Nadhani kwa sasa wangekaa kimya tu watu wameshaanza kusahau haya mambo


Tehe teh amewapa WAHAFIDHINA masharti ya kumuomba radhi, tusubiri tuone.
 
Kauli yako ngumu ndugu.


Na kama atarudi, basi, ijulikane kuwa, walio mhukumu hawana upeo wa kuona umbali zaidi ya pua zao, haiwezekani ndani ya mda huu mfupi mkamrudisha mtu ambaye mmemchunguza kwa miaka isiyo pungua mitano na kuona hafai, na leo ghafla bin vu mseme arudi?

Kamati iliyo fanya maamuzi, kama ikimrudisha Zitto, basi inabidi ijipime uwezo wake kimtazamo.

Naelewa hisia zako umeongea vyema...
 
Zitto kama hajui kosa lake ni tatizo.kama kweli ni mkomavu wa kisiasa awe tayari kuadmit makosa yake.chadema hakuna anayemchukia zitto yeye mwenyewe anajua ndio maana wote waliungana nae katika sakata la escrow.Chama kumuomba msamaha zitto ni kuwakatisha taamaa wale wote waliofanya kazi usiku na mchana kufichua mbinu chafu za zitto na wezanke katika kuharibu chama.nafikiri yeye anakihitaji zaid chama kuliko chama kinavyomuhitaji yeye

Nikuhakikishie hata siku moja Chadema haitamwomba radhi mwanachama wake yeyote mwenye hatia ya utovu wa nidhamu...

Hilo nikuhakikishie...
 
Naongelea haki ya mwanachama kama

Kwa hiyo unadhani mahakama inaweza kulazimishia mtu abaki Chadema? Mahakama unaweza kuchagulia Chadema viongozi? Mahakama inaweza kututeulia wagombea Ubunge?

Mtasubiri sana..

Mahakama inaweza kutoa hukumu kwamba fulani kafukuzwa chama bila haki.

CHADEMA haiko juu ya mahakama.

Au unafikiri CHADEMA iko juu ya mahakama?

Hayo ya kuchagua viongozi na kupeana ubunge mtajijua wenyewe.

Kama mfuasi wa chama kinachojinadi kuwa cha demokrasia na maendeleo unatakiwa kujua the basic tenets of the rule of law.
 
Ni kama mwanamke asiye na akili,aliyemsaliti mumewe kwa dharau na kejeli kisa hana pesa na kuhamia kwa mwanaume mwingine,huko mambo yamebuma ndiyo anamkumbuka mume wa awali.
"baby,nimekumic na ninakupenda sana,tuombane msamaha tuyamalize"
Ovyoooo!!
 
hivi kweli mbowe na slaa watamruhusu zito agombee urais?? sidhani..bora zito uendelee kubaki huko huko
acha umbea kwani zitto alikuambia anataka kugombea uraisi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom