Mkuu Shardcole. Hakuna anayepinga Zitto kurudi kundini iwapo atatubu (hata mwana mpotevu katika biblia alijitathmini na kugundua alipomkosea baba yake, aliporudi alijinyenyekeza na kuomba kufanywa mmoja wa watumishi wake,=hakutoa mashart= lakini baba yake akamkumbatia kwa upendo na kumpa nafasi ya juu katika wanae hadi wanae wengine wakaanza kumuonea wivu). hatuhitaji kurudia kumjulisha makosa yake ili aombe radhi, kwa sababu yapo wazi kabisa na yeye anayajua. Na kama anadai hayajui hakuna haja ya kumrudisha kundini maana atatutibua tena. Kutujia na mbwembwe za mashart ni upuuzi ambao nitashangaa sana kama chama kitaintatain. By now Zitto anatakiwa awe ameshajua kosa lake lilikuwa nini na yeye ndiye anayepaswa kukieleza chama na kueleza kwa nini anadhani sasa chama kimpokee. Akifanya hivyo nitakuwa wa kwanza kukisihi chama kimkumbatie na ikiwezekana kimpe mahala pa juu kama ilivyokuwa kwa mwana mpotevu. Kuendelea kujiinua kwa kukipa chama mashart ni muendelezo uleule wa kujiona yeye ni zaidi ya chama. Huo ni utoto - CHADEMA ni zaidi ya mtu yeyote na imebeba dhamana kubwa kuikomboa Tanzania. Yeyote atakayejiona wa maana zaidi ya CHADEMA hatumuhitaji. Hilo ndilo Zitto and the likes wanalopaswa kulijua.