Najua ni kuishutumu serikali ila wangetaka kumuua huyo anatiliwa sumu kwenye mike anayozungumza nayo, anatiliwa sumu kwenye kinywaji anachokitumia. Inammaliza taratibu anakuja kufa kwa ugonjwa wengine hawajui. hakuna serikali inayotaka kukuua kinamna ambayo itajulikana haraka hivyo, nyingine kiki hizo.
Hata Lissu naye angekuwa auawe na serikali basi eneo lile la tukio asingetoka mzima, risasi moja ama mbili tu ndiyo zingetumika. Hata angepona na kuingia kile chumba upasuaji Dodoma, na jinsi hospital za serikali zilivyojaa vibaraka. Asingetoka hai, na hakuna ambaye angejua kauawa. Si wanakuwekea tu damu ambayo si kundi lako, nani atajua?
Ule uhuni umefanywa na wahuni tu.
Hizi ni Sympathy vote kwenye ulingo wa siasa ndiyo zinatafutwa, kumfanya mwanasiasa awe juu na jina lake lisotoke midomoni mwa watu. Kunatumika mbinu nyingi mno, zenye ubaya na uzuri. Watawalaghai wengine.
"Mwanasiasa yupo kwenye kampeni muda wote, hata kama hakuna uchaguzi"