Zitto kugombea urais 2015?

Status
Not open for further replies.

kweli mkuu hii ni kweli watz wengi kazi kulalamika tuuuuuuuuuuu lakini ukimwambia toa option hana kabisa ..pale cdm kuna watu kibao wanamuona zitto ni tisho kwao wanakaa wanazusha tuu inakera sana
 
umeongea kweli ndugu huu ni mkakati ambao una mgongo wa vizito wa chadema nia yao kumuundosha zitto katika duru ya siasa lkn kamwe wakimuuondosha kwa hila yyte ile na wao wajichimbie kaburi lao

umeandika uzushi
 
Nahic mwisho wa Zitto hautakuwa tofauti sana na Warid Kaburu kisiasa lets wait...
 
Kuna wastani wa thread moja au zaidi mpya kila siku inayomhusu Zitto Kabwe, tunavitu vingi kujadiliana tofauti hizi habari zinazojurudia tena za mtu mmoja kila mara. Je? ni kweli hatuna kitu kizuri tunachoweza sema kuhusu Zitto ? Zaidi ya hizi personal attacks..??

 
Nimefanya utafiti humu JF members, wengi wanaumwa hili gonjwa.
ZITTOPHOBIASIS, kupona kazi sana
 

Lakini lisemalo lipo.Zitto kabadirika sana kuna kitu kipo mbele yake.
 
Tatizo la Zitto ni kulewa kushabikiwa, halafu fedha za kuwafadhili akina Kafulila alizitoa wapi? au naye na kati ya mafisadi watakaojivua gamba Chadema?
 
Tunapungukiwa watu makini(Great thinkers) hapa JF, sidhani kama mtu makini ukishapitia thread kama hii na reply zake utaona haja ya kuweka mchango wowote, coz kinachoendelea hapa ni mipasho na majungu yasiyo na tija. Ningeomba ingawa tuna uhuru wa kuanzisha na kuchangia mijadala mbalimbali, mods mngekuwa mnaangalia thread zisizo na tija mziondoe!
 
Tunapungukiwa na watu makini(Great thinkers) hapa JF, sidhani kama mtu makini ukishapitia thread kama hii na reply zake utaona haja ya kuweka mchango wowote, coz kinachoendelea hapa ni mipasho na majungu yasiyo na tija. Ningeomba ingawa tuna uhuru wa kuanzisha na kuchangia mijadala mbalimbali, mods mngekuwa mnaangalia thread zisizo na tija kuziondoa.
 
Duh! Hivi ma-great thinkers ni wepesi kutolewa na kuhamishwa kwenye hoja namna hii?
Tuanze kujadili matatizo yetu ya msingi na halisi, nini kifanyike ili kusambaza huduma za maji safi na salama katika mikoa ya kati kusini na magharibi mwa Tanzania? Mkishindwe jipatieni wenyewe mji.
 
Jamani mbona MAgufuli katangaza nia kwenye facebook hasemwi? Zitto Kama katangaza mwache CDM iache wananchi watakachosema na kuamua..
 
Zitto ni ndumila kuwili kwa sababu ya tamaa zake ya madaraka na fedha wakati uongozi hawezi bali mpenda sifa tu.Chadema wala msimfukuze mwacheni ajikaange kwa mafuta yake mwenyewe ili mumdhibiti asiiletee chama kashfa kwa tamaa zake.
 
Zitto is done politically and there is no coming back. It's good to see he got his sense back and be Chadema one more time. The issue is "Trust and Credibility" Zitto had lost all and I will never forget all the spy and dirty works he did for ccm. Something still itch me that Zitto still work for Kikwete, just a thought. I think Zitto should be happy where he is and continue to represent his constituents thats it, but if he want to pursue something large i.e. presidential bid, the man is done for good. No one destroyed Zitto he did to himself thats end of the story. Guys lets move away from Zitto discussions.
 
kweli mkuu hii ni kweli watz wengi kazi kulalamika tuuuuuuuuuuu lakini ukimwambia toa option hana kabisa ..pale cdm kuna watu kibao wanamuona zitto ni tisho kwao wanakaa wanazusha tuu inakera sana
Anazushiwa yapi mkuu.watu hapa wanajadili maneno na vitendo vyake na si mambo ya nyuma ya pazia,utaje huo uzushi basi.mbona akitoa hoja za msingi bungeni kila mtu humu anamsifia?bado naamini Zitto ana move aliyopania kuifanikisha and time will tell kwasababu hawezi kuikimbia cdm kwa mazingira ya sasa ya kisiasa.Nyerere alikuwa Kichwa lakini daima mnyenyekevu na hiyo hata ukimwangalia unaona inatoka moyoni na penye mgongano wa mawazo alitumia nguvu ya hoja na watu wote kumuunga mkono na hatujawahi sikia kuwa aliwahi kushawishi watu kwa hila ili aungwe mkono.
 
Moto wawaka Chadema, NI VITA YA KAMBI ZA MBOWE, ZITTO


Sunday, 01 May 2011 22:56
Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Zitto Kabwe
Ramadhan Semtawa
VITA vya makundi vimezidi kuviandama vyama vikubwa vya siasa nchini, ambapo sasa hali si shwari ndani Chadema, ambako kunadaiwa kuwepo mkakati wa kumng'oa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe.
Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, anadaiwa kuponzwa na msimamo wake kupinga ununuzi wa magari mitumba yenye thamani ya Sh480 milioni ya Chadema.
Hali hiyo ilijitokeza katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichoketi juzi Jumamosi chini ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, kikao ambacho pia kilimg'oa John Shibuda katika nafasi ya kukaimu uenyekiti mkoa wa Shinyanga.Shibuda ambaye ni mbunge wa Maswa Magharibi ameondolewa baada ya kukalia nafasi hiyo takriban kwa siku nne tu tangu ateuliwe, kufuatia kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Shinyanga Philip Shelembi ambaye alizikwa April 27, 2011.

Chanzo cha mvutano


Habari kutoka ndani ya kikao hicho cha Kamati Kuu na kuthibitishwa na baadhi ya wajumbe wa kikao hicho zinasema kuwa mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, ndiye alianzisha mvutano wa kutaka Zitto ang'olewe kutokana na kupinga wazo la kununua magari chakavu kutoka India.

Chanzo chetu cha uhakika kilidokeza kuwa mashambulizi dhidi ya Zitto yalianza pale alipounga mkono hoja ya Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo ambao walinukuliwa wakisema kwamba, isingekuwa sahihi kwa chama hicho kinachopinga ufisadi kufanya ufisadi kwa kununua magari chakavu wakati wamekuwa wakiibana serikali isifanye hivyo.

Baada ya Zitto kuunga mkono hoja hiyo, vyanzo hivyo nifafanua kuwa ndipo vurugu zilipoanza kwani Lema alianza kumrushia vijembe akisema kwamba Zitto ni tatizo na kwamba amekuwa akimtetea Shibuda.

Habari zinasema baadhi ya wajumbe walisema hoja ya Lema haikuwa na nguvu ya kumshutumu Zitto kwani Shibuda ni mbunge halali wa Chadema.

Duru zaidi za kisiasa kutoka ndani ya kikao hicho zinasema wakati mvutano huo ukiendelea, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alikuwa kimya huku kwa mara ya kwanza Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akiwa mmoja wa wajumbe waliomtetea Zitto.

"Wakati Lema akisema hivyo, Dk Slaa wakati wote alikuwa kimya na hakusema chochote. Mnyika alisimama na kumtetea Zitto kwa mara ya kwanza, na katika utetezi pia alikuwepo Grace Kiwelu," kiliweka bayana chanzo hicho.

Katika majibizano hayo inadaiwa ulifika wakati Zitto alisimama na kumwambia mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kwamba mpango mkakati wake huo wa kujenga mtandao utakuja kumgharimu katika siku za usoni."Zitto alimwambia Mbowe mpango wake huo wa kujenga mtandao ungekuja kumletea matatizo hapo baadaye, "kilisema chanzo hicho kikimnukuu Zitto ndani ya kikao.

Kung'olewa kwa Shibuda


Mbali ya Zitto, Kamati Kuu hiyo pia iliazimia kutengua nafasi ya Shibuda, kukaimu nafasi ya uenyekiti ya Chadema mkoa wa Shinyanga.Vyanzo hivyo viliongeza kwamba, kabla ya mpango huo genge linalompinga Zitto lilimshutumu kwamba alikwenda Shinyanga na kushirikiana na baadhi ya wanachama kumweka Shibuda ili kutimiza ajenda zao.

Mvutano huo unaondelea ndani ya Chadema unazidi kukiweka chama hicho kinachokua na kuwa na malengo ya kukamata dola katika wakati mgumu kutokana na makundi mawili, huku moja likimuunga mkono Zitto na jingine Mbowe.

Zitto na Shibuda ni viongozi ambao wamekuwa wakikumbwa na misukosuko ndani ya Chadema na mara kadhaa Zitto amenusurika kung'olewa katika nafasi zake za uongozi kutokana na kile kinachodaiwa ni hulka yake ya kutofautina na wenzake hata katika mambo yenye maslahi kwa chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

Kauli za Zitto, Shibuda


Zitto alipoulizwa na Mwananchi jana jioni kuhusu tafrani hiyo alisema "….tafadhali sana, naomba nisiongee chochote kwa sasa, hiki ni kipindi cha kukijenga chama, si kipindi cha kuonyesha umma kwamba Chadema kuna mgogoro".

Pale mwandishi alipomhoji zaidi alisema "…tafadhali naomba nikupigie baadaye" kisha kukata simuKwa upande wake Shibuda alikiri kusikia taarifa hizo na kuongeza kwamba, anasubiri apate taarifa rasmi kwani yeye alipewa heshima hiyo na wanachama wa Shinyanga kupitia vyombo vyao vya maamuzi.
 
Wewe mama mtu mzima unasubuliwa na upenzi au maslahi kwa Zito. Huyu si wakumwani kabisa. Mtoa mada ameleza vizuri kabisa kama hujaelewa, basi toa hayo maslahi yako binafsi usome tena. Mimi sina imani na huyu mtu mpaka mwisho wa dunia.
 
U knw wt?mimi cioni umuhimu wa malumbano ya wana cdm kwa upande wangu zito yuko sahihi kabisa chama hakiwezi kununua magari chakavu kutoka india kwa sh 486 milions wakati cdm wenyewe wanaipiga ccm kufanya hivyo mbowe anamfwata lema aliyemchanga kwenye siasa mpashkuna huyu mi nashauri zito aendendelee na msimamo wake kabisa
 

Kwa mtazamo wangu Mh ZItto arudi kundini ashirikiane na wenzake kwa ajili ya kukiimarisha chama. Mh Zitto kumbuka wanaokushabikia wengi ni watu wa CCM na unajua wanalengo gani na CHADEMA. CHADEMA ikishavurugika hutamwona hata mtu mmoja watawakimbia wanawaacha mkiwa njia panda. CHADEMA hapa mlipofikia ni mahali pazuri ila panahitaji uvumilivu na kuvumiliana. Tunamdharau kamanda LEMA lakini anajitahidi sana kuwa kwenye ukweli.
 
Kwa maoni yangu kamanda Lema anatisha kisiasa kuliko Zitto, siku akikatiwa uzi anaweza kusema yasiyotarajiwa. Kifupi sidhani kama ni mwanasiasa mzuri kwani anaropoka sana.
 

Jiweke katika nafasi yake na uone utakuwa wapi!
Kila mwanasiasa ana ndoto ya kuwa step moja au zaidi ya alipo sasa, Zitto alitaka kugombea umwenyekiti wa chama chake anachokipenda. Na kwa kujua kwamba atashinda, wazee wa chama kina Mtei (Baba Mkwe wa Mbowe) walikaa naye chini kwa lazima na kumlazimisha aondoe jina, hii ni baada ya dikteta Mbowe kukataa kumsemesha Zitto, hatimaye Zitto akatii na tokea hapo hakuna siku Zitto kasemwa vizuri. Magazeti hasa gazeti la Mwana Halisi liliandika vitu vingi vibaya kuhusu Zitto mpaka ikafikia Zitto kuwataja wamililki wa gazeti hilo (Kubenea na Kiongozi Mkubwa Chadema-Finance and Administration Manager) akiwalalamikia. Toka hapo Mwanahalisi wakajivua gamba na hawakumwandika tena Zitto.

Ninachokiona Chadema; Zitto ni tishio na ana mipango ya kugombea nafasi kubwa kwenye chama sasa wenye chama (Wakaskazini) wanahaha na wameleta ngumi mkononi (Lema) kwenye chama ili amnyamazishe Zitto kwa sababu wanajua kwa hoja hawamwezi na atawashinda. Chezeni demokrasia ya kweli, CHADEMA (Chama cha Demokrasia na Maendeleo) tunautegemea mfano kutoka kwenu sio manguvu bali hoja.

Na tukiendelea hivi hiki kizazi kitakufa kabla hatujaitoa CCM madarakani, tunazungumzia mabanzi ndani ya macho ya maadui bila kuangalia mabolt machoni kwetu. Tuache demokrasia ichukue mkondo wake.

Nawasilisha.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…