Zitto: Kikwete ni Rais wa ajabu.

Zitto: Kikwete ni Rais wa ajabu.

-Kwenye Sera za Mambo ya Nje hatuangalii matukio ya kutembelewa.Sera yetu ya Mambo ya Nje ambayo tenets zake ni za tangu enzi za Mwl.Nyerere zinatakiwa kufanyiwa overhaul.

Leo hii unashindwa kumtofautisha Rais na Waziri wa Mambo ya Nje.

Ikiwa unawezesha Marais 2 wa Mataifa makubwa ambayo yana ambitions za kuchota raslimali(Ambition za kibeberu) huku mikataba ikiwa ya Siri na huthubutu kuweka wazi ili watanzania wajue kama tumenufaika ama la,does it make you a vibrant leader? Huo ni udhaifu

Hatuwezi kujivunia kutembelewa na Mabeberu ikiwa hatujui na wala hatushirikishwi katika mikataba iliyosainiwa.Hapo wananchi tutakua tumemsaidia Chifu Mangungo.

aka weka mbali na zzk
 
Kikwete angekuwa Rais makini wala hayo ya uhuru yasingetokea. Kinachofanyika hapo ni kufidia udhaifu unaoonekana kwenye taasisi ya urais. A bless in disguise.
 
Huyu kabwe anaongea nn hapo? Ujio wa hao wakuu wawili wana faida gani kwa Tz? Je TZ imenufaika nn na ujio wa Bush? Huenda akaenda magamba kugombea urais hapa pana siri,dalili za mvua ni mawingu.Hz sifa za wakuu wawili wamekuja TZ zina saidia nn wakati nchi ina hali mbaya kiuchumi? Kujipendekeza hakuna faida, kinachohitajika ni maendeleo ya nchi ili unafuu wa maisha uonekane kwa wananchi wote.Nchi nyingine zinaleta wale wazee wasio na uwezo, je kijiji cha wazee kipo wapi?
 
zito Si ndo wale wale tangia siku nyingi?
 
Hayo ni maoni yake hayawezi kufanana na ya mnyika, mdee au hata silaa

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu BEN,hizo chamber za kichwa yako kwa kucheua vito naikubali sana lazima uwasubirishe watu sana.
-Kwenye Sera za Mambo ya Nje hatuangalii matukio ya kutembelewa.Sera yetu ya Mambo ya Nje ambayo tenets zake ni za tangu enzi za Mwl.Nyerere zinatakiwa kufanyiwa overhaul.

Leo hii unashindwa kumtofautisha Rais na Waziri wa Mambo ya Nje.

Ikiwa unawezesha Marais 2 wa Mataifa makubwa ambayo yana ambitions za kuchota raslimali(Ambition za kibeberu) huku mikataba ikiwa ya Siri na huthubutu kuweka wazi ili watanzania wajue kama tumenufaika ama la,does it make you a vibrant leader? Huo ni udhaifu

Hatuwezi kujivunia kutembelewa na Mabeberu ikiwa hatujui na wala hatushirikishwi katika mikataba iliyosainiwa.Hapo wananchi tutakua tumemsaidia Chifu Mangungo.

2:Economic Diplomacy:Hadi sasa sera zetu za mambo ya nje zimeshindwa kwenda kasi na trend ya Dunia.Kenya wamelichukulua hili kwa umakini.Wizara imeshindwa ku-intergrate wizara ya Fedha na uchumi,viwanda na Biashara,Kilimo,Mali asili na Utalii na wizara ya Uwezeshaji.Tumekomalia uzururaji wa Rais kama nguzo kuu ya sera za Mambo ya nje.Tunatekeleza Sera ya Kuomba na Kushukuru

Membe ni msomi mzuri kwenye International Relations na ana uwezo lakini Rais hawezi kukwepa lawama za kuingilia Foreign Affairs.

Katika mamia ya Ziara za Rais nje ya nchi isije kuonekana kuwa ndiyo utekelezaji wa Sera za Mambo ya nje.Hapana!

Kukiwa na Sera imara kila jambo linaenda vizuri badala ya kutegemea kipaji cha kutembea cha Rais.Sera ni institutional Mechanism.Taasisi imara na sio watu imara wa kukata mbuga halafu wanarejea na matunda mwitu yenye sumu na kuiangamiza familia pole pole kwa miaka mingi ijayo.

Ni nini sera yetu kwa Afrika?Nini sera yetu specific kwa EU?Ni nini sera yetu kwa Middle East?Ni nini Sera Yetu kwa SADC.Ni ipi sera yetu kwa Latin America?Ni utashi na kipaji cha Rais kuweza kuweka pozi la Picha na wakuu wa nchi hizo tu?Uimara wa Rais hapa Siuoni zaidi ya kipaji chake tu cha kutembea na kuimarisha Album

Actually Rais asingekua na njia nyingine ya kuficha udhaifu wake zaidi ya kutoa uhuru wa maoni ambao ni constitutional Right.Siyo Hisani.
 
Political tolerance --- sio udhaifu ndg.... Hongera Zitto kwa kuliweka hili vizuri.

Political torelance in uhusiano gani na kushindwa kuwachukulia hatua mafisadi mf. Mapacha Watatu. umefikiri kabla ya kuandika au unasifia tu uonakane na wewe umechangia positively uzi unaomhusu Zitto. kitu ndogo namna hii unashindwa kuelewa? acvha ninyamaze tu....
 
Kikwete angekuwa Rais makini wala hayo ya uhuru yasingetokea. Kinachofanyika hapo ni kufidia udhaifu unaoonekana kwenye taasisi ya urais. A bless in disguise.

we na ben saanane hamnatofauti sana unaweza kuwa na sababu za msingi kuthibitisha unayoongea.
 
Kauli nzuri kutoka kwa mwanasiasa Zitto hasa ukizingatia alikua live kwenye radio
 
jk anaweza kubeazwa kwa upole wake na uhuru aliowapa watanzania ndiyo uhuru huo wanautumia vibaya mpaka wanatukana.lakini wakati wake ndo huo unayoyoma naamini atakapo staafu umuhimu wake mtautambua tu hata mnaombeza.
 
-Kwenye Sera za Mambo ya Nje hatuangalii matukio ya kutembelewa.Sera yetu ya Mambo ya Nje ambayo tenets zake ni za tangu enzi za Mwl.Nyerere zinatakiwa kufanyiwa overhaul.

Leo hii unashindwa kumtofautisha Rais na Waziri wa Mambo ya Nje.

Ikiwa unawezesha Marais 2 wa Mataifa makubwa ambayo yana ambitions za kuchota raslimali(Ambition za kibeberu) huku mikataba ikiwa ya Siri na huthubutu kuweka wazi ili watanzania wajue kama tumenufaika ama la,does it make you a vibrant leader? Huo ni udhaifu

Hatuwezi kujivunia kutembelewa na Mabeberu ikiwa hatujui na wala hatushirikishwi katika mikataba iliyosainiwa.Hapo wananchi tutakua tumemsaidia Chifu Mangungo.

2:Economic Diplomacy:Hadi sasa sera zetu za mambo ya nje zimeshindwa kwenda kasi na trend ya Dunia.Kenya wamelichukulua hili kwa umakini.Wizara imeshindwa ku-intergrate wizara ya Fedha na uchumi,viwanda na Biashara,Kilimo,Mali asili na Utalii na wizara ya Uwezeshaji.Tumekomalia uzururaji wa Rais kama nguzo kuu ya sera za Mambo ya nje.Tunatekeleza Sera ya Kuomba na Kushukuru

Membe ni msomi mzuri kwenye International Relations na ana uwezo lakini Rais hawezi kukwepa lawama za kuingilia Foreign Affairs.

Katika mamia ya Ziara za Rais nje ya nchi isije kuonekana kuwa ndiyo utekelezaji wa Sera za Mambo ya nje.Hapana!

Kukiwa na Sera imara kila jambo linaenda vizuri badala ya kutegemea kipaji cha kutembea cha Rais.Sera ni institutional Mechanism.Taasisi imara na sio watu imara wa kukata mbuga halafu wanarejea na matunda mwitu yenye sumu na kuiangamiza familia pole pole kwa miaka mingi ijayo.

Ni nini sera yetu kwa Afrika?Nini sera yetu specific kwa EU?Ni nini sera yetu kwa Middle East?Ni nini Sera Yetu kwa SADC.Ni ipi sera yetu kwa Latin America?Ni utashi na kipaji cha Rais kuweza kuweka pozi la Picha na wakuu wa nchi hizo tu?Uimara wa Rais hapa Siuoni zaidi ya kipaji chake tu cha kutembea na kuimarisha Album

Actually Rais asingekua na njia nyingine ya kuficha udhaifu wake zaidi ya kutoa uhuru wa maoni ambao ni constitutional Right.Siyo Hisani.

Ben saa nane tena.....!!!

kukuthibitishia Zito amekuacha mbali ni pale unapotoa maoni kwenye nyayo zake na kusema baada ya yeye kusema

common man ur better than this
 
Hata ngwair kakutwa amemeza madawa lakini kwa kuwa ameondoka atasifiwa sana,kikwete kajitahhdi kwa upeo wake.na mkumbuke m2 hawezi kufanya zaidi ya upeo wake.kuna mzuri yake,mabaya yake na udhaifu pia.
 
“Kikwete ni mkuu wa nchi aliyejaribu kwa kiasi
kikubwa kuwafanya watu kuwa huru. Kama
rais angekuwa ni mtu mwenye hasira, ni wazi
kwamba nchi ingekuwa katika machafuko
makubwa,” alibainisha Zitto.

Hivi ndugu Zitto wakati anatoa matamshi hayo sijui kama alifikiria tukio la kuogofya kama la mwanahabari David Mwangosi...
Sijui kama alifikiria vitisho wavipatavyo wale wote wanaothubutu kuweka bayana kadhia za Serikali hadharani...
Serikali ya sasa ni kama panya tu, inang'ata na kupuliza ili ionekane ni njema mbele ya wananchi wake...

Mwangosi aliuwawa na wafahidhina
 
Political tolerance --- sio udhaifu ndg.... Hongera Zitto kwa kuliweka hili vizuri.

Political tolerance ndio nini ndugu? Political tolerance iliyosheheni mauaji ya watu wasio na hatia? Yeyote anayeinuka kuwakosoa viongozi na serikali anageuka kuwa adui na anawindwa kuuawa au kuteswa na kung'olewa meno na kucha?!! Political tolerance inayotugawa watanzania kwa ubaguzi wa kidini ambao unatishia vita ya kidini Tanzania. Political tolerance tunaibiwa raslimali zetu? Political tolerance na Bunge la mipasho lisilo na tija kwa watanzania? Political tolerance na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa vilivyojaa matusi na kashfa? Hata gazeti la Kenya lililotoa kibonzo cha kukashfu Bunge halikukosea!
Anyway, President Kikwete ni mvumilivu hilo halina ubishi. Ni mtu wa watu na anayelia na waliao hilo pia halina ubishi. Angekuwa mtu wa kutaka kuitwa 'Mtukufu Rais' basi Tanzania ingejaa makaburi ya halaiki. Wengi wangenyongwa au kupotezwa katika mazingira tatanishi! Hongera Rais wetu Kikwete!
Hata hivyo tujiulize 'Nyuma ya huo uvumilivu kuna nini?'...Pengine uvumilivu wa Rais ni wa kutafuta faraja ya watanzania, maana kuna viongozi wengi wa chini yake wanamhujumu! Mara ngapi Rais amedanganywa na viongozi wa chini yake? Mara ngapi amezindua miradi bosheni??? Pia inawezekana uvumilivu wa Rais unaficha udhaifu wake! Ameshindwa kuchukua hatua dhidi ya udini ambao ni zimwi linasubiri kutuangamiza! Ameshindwa kuchukua hatua dhidi ya viongozi na watendaji wabovu na wanatia saini mikataba michafu. Ameshindwa kuchukua hatua dhidi ya viongozi hususan mawaziri wanaendekeza udini katika wizara zao! Rais ni dhaifu hilo halina ubishi! Tunae Rais lakini naogopa kusema katika kipindi cha miaka 10 ni kama TZ haina Preident na Waziri Mkuu tuliyenae ni kiongozi mwenye hulka ya huruma sana! Kuongoza nchi kunataka ubabe lakini ubabe usiopitiliza kuwa udikteta!
 
Back
Top Bottom