-Kwenye Sera za Mambo ya Nje hatuangalii matukio ya kutembelewa.Sera yetu ya Mambo ya Nje ambayo tenets zake ni za tangu enzi za Mwl.Nyerere zinatakiwa kufanyiwa overhaul.
Leo hii unashindwa kumtofautisha Rais na Waziri wa Mambo ya Nje.
Ikiwa unawezesha Marais 2 wa Mataifa makubwa ambayo yana ambitions za kuchota raslimali(Ambition za kibeberu) huku mikataba ikiwa ya Siri na huthubutu kuweka wazi ili watanzania wajue kama tumenufaika ama la,does it make you a vibrant leader? Huo ni udhaifu
Hatuwezi kujivunia kutembelewa na Mabeberu ikiwa hatujui na wala hatushirikishwi katika mikataba iliyosainiwa.Hapo wananchi tutakua tumemsaidia Chifu Mangungo.
2:Economic Diplomacy:Hadi sasa sera zetu za mambo ya nje zimeshindwa kwenda kasi na trend ya Dunia.Kenya wamelichukulua hili kwa umakini.Wizara imeshindwa ku-intergrate wizara ya Fedha na uchumi,viwanda na Biashara,Kilimo,Mali asili na Utalii na wizara ya Uwezeshaji.Tumekomalia uzururaji wa Rais kama nguzo kuu ya sera za Mambo ya nje.Tunatekeleza Sera ya Kuomba na Kushukuru
Membe ni msomi mzuri kwenye International Relations na ana uwezo lakini Rais hawezi kukwepa lawama za kuingilia Foreign Affairs.
Katika mamia ya Ziara za Rais nje ya nchi isije kuonekana kuwa ndiyo utekelezaji wa Sera za Mambo ya nje.Hapana!
Kukiwa na Sera imara kila jambo linaenda vizuri badala ya kutegemea kipaji cha kutembea cha Rais.Sera ni institutional Mechanism.Taasisi imara na sio watu imara wa kukata mbuga halafu wanarejea na matunda mwitu yenye sumu na kuiangamiza familia pole pole kwa miaka mingi ijayo.
Ni nini sera yetu kwa Afrika?Nini sera yetu specific kwa EU?Ni nini sera yetu kwa Middle East?Ni nini Sera Yetu kwa SADC.Ni ipi sera yetu kwa Latin America?Ni utashi na kipaji cha Rais kuweza kuweka pozi la Picha na wakuu wa nchi hizo tu?Uimara wa Rais hapa Siuoni zaidi ya kipaji chake tu cha kutembea na kuimarisha Album
Actually Rais asingekua na njia nyingine ya kuficha udhaifu wake zaidi ya kutoa uhuru wa maoni ambao ni constitutional Right.Siyo Hisani.