Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,232
- 113,610
Kwa hiyo umeamua kuuchuna kabisa kuhusu vyombo vya habari binafsi wakati wa Nyerere...?
Jamani wandugu acheni kutumia vibaya elimu kiasi hicho...Mnaposema Zitto hana elimu ya madini mna maana gani hapa?..
Hivi nyie nyote mloona kasoro ktk mikataba hii mmesomea madini? ama nyote ni wanasheria?.
Duh! mimi naona karibu hata bunge letu litahitaji watu wenye shahada ya sheria ili kutunga sheria nikifuata mtazamo wenu kwani yaonyesha wazi mnaamini kuwa huwezi kufahamu uzito na athari ya kitu bila kuwa na elimu yake. Yaani hata njaa inahitaji elimu ya upishi wa chakula uweze ku solve tatizo la njaa bila kujua kwamba njaa kinachotakiwa ni mahesabu ya kiwango cha shibe sio degree ya upishi.
Jamani haya si ndio maswala tunayosema huhitaji kuwa mwana sayansi! - ama.
Damn!
Mhe. Zitto akizungumza Bungeni kutoa hoja ya kuundwa kamati teule ya BungeMheshimiwa Spika, utata huu ambao umegubika sekta hii ya madini unaweza kufafanuliwa na Bunge lako Tukufu kupitia Kamati Teule. Kamati Teule ya Bunge ichunguze upitiaji wa mikataba hii na kuona kama kuna vitendo vyovyote vya uvunjaji wa sheria za nchi na kupotea kwa mapato ya Serikali na ufisadi.
Mheshimiwa Spika, suala hili ni suala la kitaifa. Halina hata chembe ya itikadi za kivyama. Naamini Wabunge wataamua kwa maslahi ya Taifa letu. Uundwaji wa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza mapitio ya mikataba ya madini na mazingira ya kusainiwa kwa mkataba mpya wa Buzwagi utatoa msaada mkubwa kwa azma ya Rais wetu, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete ya kuona rasilimali za madini zinafaidisha nchi yetu.
Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja.
Magreat Wa wakati huo..HIV wapo?Kitila,
Nakubaliana na wewe juu ya hili na sio wakati wote ni wa kupinga kila kitu, inabidi chama cha upinzani wakati mwingine kiwe tayari kushirikiana na serikali kwa faida ya nchi.
Kwenye hili la kamati ni afadhali kuwa ndani na ku influence maamuzi ya kamati na hivyo sheria ya madini kwa faida ya nchi kuliko kuwa nje.
Pamoja na kusema hayo, Wangwe naye ana right ya kupinga na hata siku moja kupinga kwake kusichukuliwe kama amechukia kwasababu hayumo kwenye kamati.
Siasa ni ngumu sana na wakati mwingine inabidi kuachana na misimamo mikali na kuchukua msimamo wa kati ili kupata ufumbuzi wa tatizo.