Kuntakinte
JF-Expert Member
- May 26, 2007
- 702
- 28
:: CHADEMA sasa waanza kumchimba
:: Chacha amshauri ajiuzulu, yeye agoma
:: Asema hajausaliti upinzani, hatishiki
:: Leo anamaliza adhabu ya kufukuzwa
na godfrey dilunga
Ina maana wananchi ni wa CCM au wa CHADEMA? Mhe. Chacha bado sijamuelewa maana kuteuliwa na Rais lazima kuna sababu za msingi au umeonekana ufanisi na upeo wa mtu as Individual kwenye kupanga na Kujenga Hoja sasa iweje waseme amewasaliti? Au alitaka awe yeye kwenye Kamati. Kwani katiba ya CHADEMA inasemaje kuhusu wajumbe hawatakiwi kushiriki kwenye mambo ya Kujenga nchi?
:: Chacha amshauri ajiuzulu, yeye agoma
:: Asema hajausaliti upinzani, hatishiki
:: Leo anamaliza adhabu ya kufukuzwa
na godfrey dilunga
HATUA ya Rais Jakaya Kikwete kumteua Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Kabwe Zitto, kuingia katika Kamati ya Kuchunguza Mikataba ya Madini inaelekea imezusha mgogoro wa ndani katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Hatua hiyo imetokana na Mbunge wa Tarime (CHADEMA), Chacha Wangwe, kutamka hadharani kuwa Zitto anapaswa kujiuzulu kutoka kwenye Kamati hiyo iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete, hali inayopingana na fikra za Zitto.
Zitto anapaswa kujiuzulu si zaidi ya saa 24 kuanzia leo. Kukubali uteuzi ni sawa na kuusaliti upinzani nchini, Chacha alikaririwa akimwambia mmoja wa wabunge mjini Dodoma jana.
Mbali na kauli hiyo, gazeti moja la kila siku jana lilimkariri Wangwe, hivi: Alisema anapinga suala hilo kwa madai kwamba, kuundwa kwa kamati hiyo kumelenga kudhoofisha hoja ya msingi ya wapinzani ya kutaka sheria ya madini ifutwe kabla ya kwenda katika hatua ya pili ya kujadili mikataba. Kizingiti kikubwa ni sheria, ndiyo haijakaa vizuri. Hivyo kilichotakiwa ni sheria kufutwa kwanza halafu ndiyo tuzungumze mikataba mipya.
Mwandishi Wetu alipowasiliana naye mjini Dodoma jana, Wangwe alisema amsubiri kidogo amalize kikao cha Kamati na hadi tunakwenda mitamboni ilikuwa hajapatikana na simu yake ya mkononi muda wote ilikuwa imezimwa.
Kwa upande wake Zitto, aliliambia Mtanzania kuwa hajausaliti upinzani na wala kuteuliwa kwake katika kamati hii hakupingani na dhana yoyote kwani imebeba malengo yanayowiana na dhamira ya kambi ya upinzani na kwamba hatajiengua kutoka katika kamati hiyo.
Kauli hiyo ya Zitto inapingana na ile iliyotolewa na Wangwe. Wangwe na Zitto wote ni wabunge kutoka CHADEMA na Zitto ni bosi wake Wangwe kwani ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho. Hata hivyo, Wangwe ni mmoja kati ya viongozi wenye nguvu kubwa ya ushawishi ndani ya CHADEMA.
Zitto alisema si busara kwake kujiondoa katika kamati hiyo kwa kuwa malengo yake yanarandana na ya kambi ya upinzani.
Akifafanua Zitto alisema baadhi ya hadidu za rejea za Kamati ya Madini iliyoundwa na Rais Kikwete, zinarandana na baadhi ya vipengele vya Azimio la Songea, ambalo lilitangazwa na upinzani mjini Songea, Septemba 10, mwaka huu.
Alisema azimio hilo linahimiza kuundwa kwa kamati ya madini pamoja na kufanyika kwa marekebisho ya sheria za; madini, kodi ya mapato ya mwaka 2004 na sheria ya uwekezaji.
Si kweli kwamba kambi ya upinzani ilitaka kufutwa kwa sheria ya madini, matakwa yake ni kufanyiwa marekebisho ya sheria hiyo pamoja na sheria nyingine, alisema Zitto.
Alisema vipengele hivyo ni sehemu ya hadidu za rejea za kamati ya madini iliyoundwa na Rais Kikwete.
Rais Kikwete alitangaza dhamira ya kuunda Kamati ya Madini wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Nane wa Chama Cha Mapinduzi mjini Dodoma, hivi karibuni.
Alitimiza dhamira yake hiyo juzi kwa kuwateua Mwenyekiti wa Kamati, Jaji Mark Bomani, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige na Mbunge wa Kyela Dk. Harrison Mwakyembe.
Wengine ni Peter Machunde kutoka Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), David Tarimo kutoka Kampuni ya Uhakiki wa Hesabu ya PriceWaterCoopers, Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa katika Wizara ya Nishati na Madini, Maria Kejo na Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange.
Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni Kamishna wa Sera katika Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha na Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Makazi katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Edward Kihundwa.
Kamati hiyo bado haijaanza kazi ingawa imepewa kipindi cha miezi mitatu kukamilisha kazi na kukabidhi ripoti kwa Rais Kikwete.
Ina maana wananchi ni wa CCM au wa CHADEMA? Mhe. Chacha bado sijamuelewa maana kuteuliwa na Rais lazima kuna sababu za msingi au umeonekana ufanisi na upeo wa mtu as Individual kwenye kupanga na Kujenga Hoja sasa iweje waseme amewasaliti? Au alitaka awe yeye kwenye Kamati. Kwani katiba ya CHADEMA inasemaje kuhusu wajumbe hawatakiwi kushiriki kwenye mambo ya Kujenga nchi?