Zitto Kabwe: Samahani Rais Mwinyi lakini kwenye hili umekosea

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,558
Na Zitto Kabwe

MAONI: Suala moja lililoibuliwa katika mikutano ya hadhara ya chama cha ACT Wazalendo inayoendelea katika visiwa vya Unguja na Pemba ni uendeshaji (ground handling) wa ‘Terminal 3’ katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar.

Katika mkutano uliofanyika Nungwi Februari 26, 2023, Kaskazini Unguja, niliwaeleza wananchi kwamba kutokana na maamuzi ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege ya Zanzibar (ZAA) ya kutoa ukiritimba kwa kampuni moja ya uendeshaji wa viwanja vya ndege, zaidi ya Wazanzibari 200 wako hatarini kupoteza ajira zao.

Nilieleza kuwa ZAA imevunja sheria za Zanzibar na za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazokataza ukiritimba wa kampuni moja kuendesha shughuli za viwanja vya ndege.

Siku mbili baada ya mkutano huo wa Nungwi, Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi alijitokeza kujibu suala hili.

Akizungumza na waandishi wa habari mnamo Februari 28, 2023, katika Ikulu ya Mnazi Mmoja, Rais Mwinyi alisema “madai” yetu ACT-Wazalendo hayana ushahidi wowote na kwamba yana lengo la kuwapotosha wananchi.

Kiongozi huyo alisema kwamba uamuzi wa Serikali yake kuipa ukiritimba kampuni ya Dubai ya Dnata kuendesha ‘Terminal 3’ kumeisaidia Serikali kukusanya mapato mengi zaidi, kitu ambacho ameshangaa kwamba ACT-Wazalendo hatukisemei.

Bahati mbaya sana, Mheshimiwa Rais Mwinyi hajaeleza hoja za msingi zilizoibuliwa katika mkutano ule na kuhusu suala lenyewe la uendeshaji wa ‘Terminal 3’ katika Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume.

“Uungwana unataka uweke maslahi yako wazi [wakati unatetea jambo fulani],” alisema Dk Mwinyi. “Kama una maslahi [kwenye jambo hilo,] uyaseme. Hao wanaowataka wao [ACT Wazalendo,] wana maslahi gani? Upo uhusiano kati ya hizo kampuni na viongozi [wa ACT Wazalendo]. Mbona hawasemi? Kwa hiyo, hapa hawaitetei Serikali na nchi, wanatetea maslahi binafsi.”

Makala haya mafupi yana shabaha ya kueleza msingi wa hoja hii na kwa nini tulitaka Taasisi ya Uchunguzi wa Rushwa Zanzibar (ZAECCA) ifanye uchunguzi wa mkataba wa uendeshaji wa Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume.

PIA SOMA:
- Rais Mwinyi awachana ACT Wazalendo kwa ufisadi

Credit: The Chanzo
 
Na Zitto Kabwe

MAONI: Suala moja lililoibuliwa katika mikutano ya hadhara ya chama cha ACT Wazalendo inayoendelea katika visiwa vya Unguja na Pemba ni uendeshaji (ground handling) wa ‘Terminal 3’ katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar

Credit: The Chanzo
Kuna vitu haviko sawa! Jibuni hoja za mwinyi acha longolongo
 
Naona siku hizi inatangulia samahani kwanza kabla ya ukosoaji.

Safi sana hii.

"Samahani NEC, tunaomba kuyakataa matokeo ya urais."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom