Zitto Kabwe: Nani anaongoza nchi yetu?

Zitto Kabwe: Nani anaongoza nchi yetu?

Zitto bhana! Uambiwe na nani sasa hali ya Rais?

Waziri mkuu kasema yuko fiti
Makamu Rais kasema rais yuko fiti

Unataka uambiwe na nani sasa?

Huu upumbavu kumbe hadi kwa wasomi upo?

Haya mambo yanashangaza san!,labda wantaka Lissu ndo atoe maelezo kuhusu maradhi ya Raisi.
 
Ukimya huu una jambo si bure tena hao!! hao!!wa jaribu yake wanaweza kummalizia! Ili wakapige hela ndefuuuu!! Faster.ili wafikie mafanikio yao vizuri ni kuondoa hicho kiwingu!! Na ndiyo wa kwanza kuturopokea kwa nguvu zotee! Tusimseme!!!

Km huyu IDEGENDA ni hatari sana kwa afya ya jiwe.ila kwa vile jiwe kazibwa machi kichawi hajui.

Hii kwao hao mafisadi waliojificha kwa mgongo wa unafiki ni fursa sana kwao. ndo watammalizia .kwanza unadhani wamuamini jiwe na jiwe hawaamini.wako km paka na panya.

Wanajua wanaweza tumbuliwa any time wakiwa mikono mitupu. Jiwe hatabiriki hii ndiyo nafasi nzuri na adimu kwenu!!

Sasa skiwa bado anajiuguza mjengeni mansion faster.hata akirudi tayari uko pazuri.
hata akikufunga wanao wanapeta utatoka lupango tu!

Angejua angeambatana na kina zitto.lisu.mbowe wale wapinzani siyo rahisi kummalizia.

Lkn hawa wanaojua dhambi zao!!! Na kamungu mtu kao kanaumwaa heee!!. Walahi akipona sijui!!!

Tatizo hata mtoto wake mwenye akili za kumshika baba yake sikio hakuna. Kwanza Nani anawajua humu?

Angalua Kikwete na ridhiwani walikuwa damdam!! Utasikia "Baba usiende huko!!! Usifanye hiki kile fanya"

Pamoja na ujanja woooote jiwe Ameshindwa kujua kikulacho kiko wapi....

.ikitokea mtu wa karibu yake akawapiga chini wasaidizi wa jiwe wote! Atapona. Hata wakumfungua macho hana...unoko uliopitiliza....
 
NANI ANAONGOZA NCHI YETU?


1. Utangulizi:

Ndugu Wananchi

Katika siku za hivi karibuni suala la afya ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli limekuwa katika mijadala katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi, katika mitandao ya kijamii na katika medani nyinginezo.

Kukithiri kwa mijadala hiyo kumesababisha hali ya wasiwasi na taharuki miongoni mwa wananchi. Hali hiyo inatia shaka zaidi na kutokuonekana hadharani kwa Rais mwenyewe kwa takriban siku 16 sasa. Aidha, ukimya wa hali ya juu miongoni mwa viongozi serikalini kumeongeza uzito wa suala hili.

Tunatambua kuwa Waziri Mkuu akiwa msikitini wilayani Njombe, alitamka kuwa amezungumza na Rais na kutaka watanzania wapuuze kauli za kuzua taharuki kuhusu afya ya Rais. Kiukweli Watanzania wanapata shida kuamini kauli hii ya Waziri Mkuu, kwani imezoeleka huko nyuma kwa Rais kuwapigia viongozi wake simu hasa wanapokuwa katika hadhira. Kwa namna tunavyojua utendaji wa Rais, kwa uvumi kuhusu afya yake ulivyoenea hiyo ndio ingekuwa njia angeitumia kumaliza uvumi na uzushi huo, haikuwa hivyo.

Imezoeleka kuwa kila siku ya Jumapili, Rais hujumuika na waumini wengine kwa ibada kanisani na mara nyingi kuzungumza na Taifa, kwa Jumapili ya Juzi tarehe 14 Machi, 2021 hali haikuwa hivyo. Hii inaongeza taharuki na kuongeza uzito wa uvumi unaoshika kasi kuhusu afya ya Rais.

Hata kauli ya Makamu wa Rais jana akiwa njiani kwenda mkoani Tanga haikukidhi haja, imeongeza mshawasha badala ya kuzima tetesi zilizoenea, imeacha maswali mengi zaidi badala ya kujibu maswali yanayoulizwa kuhusu afya ya Rais, imeibua sintofahamu zaidi badala ya kuleta utulivu kwa wananchi.

2. Tathmini Yetu:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana mamlaka makubwa na nafasi nyeti katika ustawi wa Taifa. Katiba ibara ya 33(2) inamtambua Rais kama pia Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu. Haya ni mamlaka makubwa sana. Hivyo basi, afya ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitakiwi kuwa ni jambo la kudhihakiwa ama linapouliziwa watu kuonekana wabaya.

Afya ya Rais, kwa umuhimu wake, ni jambo lililowekewa utaratibu wa kushughulika nalo inapotetereka. Tunatambua pasi na shaka kwamba Rais anaumwa, tunashangazwa na ukimya unaoendelea kutamalaki katika suala hili. Ni kwa kiasi gani ugonjwa wa Rais unasababisha ashindwe kutekeleza majukumu yake ni suala lililo katika utaratibu wazi wa kikatiba. Kwa umuhimu wake ninanukuu vipengele vifuatavyo vya Katiba:

Ibara ya 37(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, toleo la 2005 inasema, nanukuu;

“Endapo Baraza la Mawaziri litaona; kuwa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili, laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili au akili, hawezi kumudu kazi zake. Baada ya kupokea azimio kama hilo, Jaji Mkuu atateua Bodi ya Utabibu ya watu wasiopungua watatu atakaowateua kutoka miongoni mwa mabingwa wanaotambuliwa na sheria ya matabibu ya Tanzania, na Bodi hiyo itachunguza suala hilo na kumshauri Jaji Mkuu ipasavyo, naye (Jaji Mkuu) aweza baada ya kutafakari Ushahidi wa kitabibu kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba Rais,kutokana na maradhi ya mwili au ya akili hamudu kazi zake; na iwapo Jaji Mkuu hatabatilisha tamko hilo ndani ya siku saba kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi itahesabiwa kiti cha Rais ki wazi, na yaliyomo katika ibara ndogo ya (5) yatatumika.”

Aidha, Ibara ya 37 (3) ya Katiba nayo pia inatamka yafuatayo kuhusu Rais kushindwa kutekeleza majukumu yake, nanukuu;

“Endapo Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano au atashindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu nyingine yeyote, kazi na shughuli za Rais zitatekelezwa na mmojawapo wa wafuatao kwa kufuata mpangilio ufuatao, yaani –
(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yake iwazi au kama naye hayupo au ni mgonjwa; basi;
(b) Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano”.

Zaidi, Ibara ya 37 (4) inaeleza;

“Endapo Waziri Mkuu ndiye atatekeleza kazi na shughuli za Rais kutokana na sababu kwamba Makamu wa Rais hayupo basi Waziri Mkuu ataacha kutekeleza kazi na shughuli hizo endapo lolote kati ya mambo yafuatayo litatokea mwanzo –
(a) Rais atakaporejea katika Jamhuri ya Muungano au atakapopata nafuu kutokana na maradhi na kuanza kutekeleza kazi za Rais;
(b) Makamu wa Rais atakaporejea katika Jamhuri ya Muungano”.

Tumenukuu vipengele vyote hivyo vya Katiba kuonesha umuhimu na uzito unaopewa afya ya Rais katika nchi hii. Huu si wakati tena wa kukaa kimya. Huu ni wakati wa Serikali kutoa tamko rasmi la hali halisi kuhusu afya ya Rais. Tunahitaji kujua ni nani hivi sasa anayetekeleza madaraka ya Rais na kwa nyenzo ipi ya Katiba. Ukimya uliopo sasa unasababisha taharuki kubwa isiyo na tija kwa ustawi wa Taifa letu. Tunachelea kuwaza, na Mwenyezi Mungu apishie mbali, hivi leo Taifa letu likivamiwa na wasioitakia mema nchi yetu, ni nani Amiri Jeshi Mkuu? Kutuambia tu tuko salama bila kutuambia yuko wapi Amiri Jeshi Mkuu si jambo linaloleta utulivu.

3. Wito Wetu kwa Serikali:

Kwa kuzingatia uzito wa tuliyoyaeleza, tunatoa wito kwa Serikali, kwanza iwaachie watu wote waliokamatwa na Jeshi la Polisi kwa kuhoji juu ya afya ya Rais, kisha ifanye yafuatayo ili kutuliza mshawasha wa wananchi;

i. Itueleze wananchi hali halisi ya afya ya Rais, itumie pia maelezo hayo kutujibu kwa kina wananchi iwapo Rais bado anao uwezo wa kutekeleza majukumu yake au la.

ii. Iwapo Rais hana uwezo huo au afya yake imetetereka kiasi cha kutia mashaka, basi kifungu cha 37(2) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kitekelezwe ili jopo la matabibu litakaloteuliwa na Jaji Mkuu lifanye kazi yake na hali ya afya ya Rais ijulikane wazi kupitia kwa Spika.

iii. Katibu Mkuu Kiongozi atamke rasmi kuwa Makamu wa Rais amekuwa akitekeleza madaraka ya Rais Kwa mujibu wa Katiba na kwamba ni Kaimu Rais Kwa mujibu wa Itifiki zote. Hivyo basi kumtaka Makamu wa Rais atekeleze majukumu uRais Kwa mujibu wa Katiba na atumie nafasi hiyo kulieleza Taifa Hali ya Rais.

iv. Wakuu wa Mashirika ya Umma, na haswa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) watoke kuzima tetesi zinazoenea juu ya yanayoendelea katika taasisi hiyo nyeti kwa uchumi wa Nchi. Ni muhimu rekodi ya Fedha za Kigeni na Akiba ya Dhahabu zilindwe. Wakati huu wa sintofahamu ni vizuri Makamu wa Rais peke yake kama Kaimu Rais ndiye anapaswa kuidhinisha kwa kauli thabiti kinachoitwa ‘maagizo ya Rais’. Wananchi watahitaji Taarifa kuhusu Akiba hizi mara baada ya sintofahamu hii kuisha.

Vile vile Tunatoa wito Kwa Asasi za Kiraia na Bunge kuchukua hatua Kwa;

- kuitaka TLS na AZAKI nyengine za uwajibikaji wapaze Sauti zao katika Suala hili ili kulinda Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania . Itakuwa ni makosa makubwa kwa siku nyengine 16 kuacha Nchi ikiongozwa na watu ambao hawakuchaguliwa (unelected bureaucrats) Wakati Katiba yetu imezingatia mazingira yote ya mwanadamu.

- Kutoa wito kwa Waheshimiwa Wabunge watumie nafasi yao kuitaka Serikali itoe tamko kuhusu Afya ya Mhe Rais . Kwa kufanya hivyo ni kulinda kiapo chao cha kuitetea na kuuhifadhi Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

4. Hitimisho:

Afya ya Rais sio jambo linalopaswa kuwa siri, yeye ni kiongozi wa Taifa hili. Tumekuwa na marais ambao waliugua huko nyuma, Marehemu Mzee Mkapa alipougua na kukaa muda mrefu nchini Uswizi wananchi walijulishwa na taarifa za mara kwa mara zilitolewa kuhusu maendeleo ya afya yake, halikadhalika Mzee Kikwete alipofanyiwa upasuaji nchini Marekani.

Utoaji huo wa taarifa za hali ya afya ya Kiongozi wa nchi ni jambo la kawaida duniani kote, na husaidia kuondoa taharuki na wasiwasi ambao kwa bahati mbaya ndio vimetamalaki nchini kwa sasa. Ni muhimu Serikali itoe taarifa kuhusu Afya ya Rais ili kumaliza taharuki iliyopo, kwank Watanzania tunayo haki ya kujulishwa hali ya afya ya Rais.


Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Machi 16, 2021
Dar es salaam.View attachment 1726977
We mtu tangu uliporopoka eti ndege za ATC ni 2nd hand kwa kusoma tarehe kwenye vioo, sijawahi hata kukuona kama una akili timamu. Kila nikiangalia uso wako, ninachokiona ni u-maimuna zaidi ya kiwango.

Mtindo wa kupitishia makara zako huku acha mara moja! Huku tunaleta mambo ya kujaduiliwa sasa kama huna uwezo wa kujadili, get your hell out of this place!
 
CCM acheni tabia yenu ya kuficha ficha ugonjwa - ficha yote hapa duniani ruksha ila siyo maradhi - maana maradhi yana tabia ya kuumbua.

Watanzania hawa wanataka kujua:-

1. Je Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo wapi?
2. Na ana hali gani kiafya?

Msipotuambia tunampango wa kwenda mahakamani kuiomba ili watanzania wote kwa pamoja tuanze kumsaka popote alipo - maana yeye ndiye tulimchagua awe kiongozi wetu sasa kwa nini mumfiche?

Yupo Chato anafanya kilimo cha Maparachichi na Vanilla ila mje muone shamba darasa...msitusumbue Angaikeni na chama Chenu tuachien Rais Wetu apumzike.
 
So contradictory!

Zitto unasema Viongozi wa juu wako kimya, wakati huo huo unasem PM ametoa kauli, pia VP ametoa kauli. Sasa hapo issue ni ukimya wa viongozi, au huwaamini?

Pia unataka serikali itoe maelezo. Nani tena atoe maelezo ikiwa Mkuu wa shughuli za serikali ameshatoa kauli?

Usizunguke mbuyu, issue uitakayo ni rais kujitokeza hadharani.


Kwani Raisi amekuwa Doll la maonyesho kila siku kujitokeza hadharani,kama hawataki Basi wamuulize Halima Mdee na Bulaya.
 
Zitto bhana! Uambiwe na nani sasa hali ya Rais?

Waziri mkuu kasema yuko fiti
Makamu Rais kasema rais yuko fiti

Unataka uambiwe na nani sasa?

Huu upumbavu kumbe hadi kwa wasomi upo?

Sasa yuko wapi? Kaolewa kawa mwali?
 
Nina rafiki yangu amechoka kuona ukimya kuhusu hili sakata

kaniambia CONTROLA nikisikia Chuma kimetoka huko kilipokua

kikaongea neno lolote,Nitakunywaaaaa nileweee kwa furaha nitakayokua nayo

hana raha,hana amani,anatamani kujua Chuma kiko wapi anatamani tu kuisikia ile sauti

na hakika amedhamiria maana sio kwa kiapo alichoniapia,Simba akinguruma tu Yeye Ni Maji mpk kunakucha kwa raha...
 
We mtu tangu uliporopoka eti ndege za ATC ni 2nd hand kwa kusoma tarehe kwenye vioo, sijawahi hata kukuona kama una akili timamu. Kila nikiangalia uso wako, ninachokiona ni u-maimuna zaidi ya kiwango.

Mtindo wa kupitishia makara zako huku acha mara moja! Huku tunaleta mambo ya kujaduiliwa sasa kama huna uwezo wa kujadili, get your hell out of this place!
Acha mkwara basi! Watanzania wanataka kujua Rais wao yuko wapi!! Tuachane na hizo ndege kwanza! Mtuambie yuko wapi?
 
Kwani Raisi amekuwa Doll la maonyesho kila siku kujitokeza hadharani,kama hawataki Basi wamuulize Halima Mdee na Bulaya.
Zamani wakati anazindua live, anateua live, anatumbua live, anahutubia live, alikuwa Doll la hayo maonyesho? Kwani ugumu wa yeye kujitokeza hadharani kuwasalimia wafuasi wake na kuwaziba midomo wapinzani wake, uko wapi?
 
Zitto kama Kiongozi wa Chama anayo haki na jukwaa la kusema na kuhoji uwepo wa Rais. Pili, nakumbuka ACT walivyotoa habari za ukweli kuhusu afya ya Maalim Seif. Zitto anavyanzo vya uhakika Serikalini.

Hata hivyo naona suala la Akiba ya Fedha za Kigeni na Dhahabu huko BoT ndio kiini cha andiko hili. Mengine yoooote hayo ni ku-justify hoja lakini lengo ni BoT kunadaiwa Kuna mashindano ya ukwapuaji. Ahsante Zitto. Tumuombee Rais afya njema akirudi kutoka Rubondo Island mapumzikoni watazinya.

Ukishakuwa ni mwizi basi unafikiri kila umuonaye ni mwizi. Anakumbuka uenekiti wa kamati ya mahesabu ya mashirika ya umma na team yao ya 1st eleven ya enzi zile.
 
Nani anaongoza nchi? Hatutakiwi kujua and its not our business?? Ajabu sana.
Hoja zote za Zitto ni upumbavu mtupu.
Kwanza waliokamatwa sio kwa sababu ya kuhoji bali kutoa taarifu za uongo.
Pili si kweli kwamba serikali haijatoa tamko. Waziri Mkuu na Makamu wa Rais wameshatoa tamko. Tatizo hamtoridhika na kauli kinyume na matarjio yenu hususan kama hamjamuona. Au unataka kutuaminisha kwamba Dr. Abbas kauli yake ni nzito kuliko Samia!? Haya tuseme anaumwa kwa mujibu wa yeye je anajua anaumwa nini na anaumwa kiasi gani!??
Tatu hata kama Rais MGONJWA bado katiba yako imeacha mwanya mkubwa sana wa Manoeuvre kwani haisemi baada ya siku ngapi za ugonjwa ndipo mchakato uanze wa kumtoa. Yaani hata kama ni ugonjwa UNATIBIKA bado tumtoe!?
Afterall its very automatic Rais asipokuwa ofcn makamu anakaimu. Sasa haya mambo ya sijui BOT yametoka wapi ina maana uongozi hakuna hata kama ni kweli Rais anaumwa!?
Labda tuulize ACT mlifanyaje wakati Maalim Seiph anaumwa!? Nakumbuka aliwahi kulazwa miezi 3 hapo kabla ilikuwaje chamani. Alikuwa bingwa pia wa ziara za miezi nje ya nchi...

Huyu Zitto kaanza kuwa fala sana aisee
 
Huyu Kijana Zitto sijawahi mwelewa, haieleweki nini kinamsumbua. Ndiyo maana kila awapo huwaza taharuki tuu, ambazo humfuata yeye mwenyewe. Unachotakiwa kama umesikia Raisi anaumwa ni kumuombea ukimtakia mema ili apone haraka.
 
Nchi haiongozwi na matamko ya misiktini na Barabarani.
Sasa mbona nyinyi mnahoji uwepo wa Rais kwakua hamkumuona Kanisani kama kawaida yake? Kwamjibu wa hoja yako, mlitakiwa msubirie mpka pale atakapokuwa na kazi inayomlazimu kuhutubia, tena akiwa ikulu maana ndio sehemu unayoiamini kuliko huko makanisani na misikitini.
 
Unalazimisha kujibishana nami.

Sina lolote la maana ninaloweza kufaidika nalo kutokana na michango yako humu.

Kwa hiyo nenda kafilie mbali.
Sasa unanijibu ili iweje? Hao wahuni wenzenu wamechukua akili zenu zote
 
CCM acheni tabia yenu ya kuficha ficha ugonjwa - ficha yote hapa duniani ruksha ila siyo maradhi - maana maradhi yana tabia ya kuumbua.

Watanzania hawa wanataka kujua:-

1. Je Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo wapi?
2. Na ana hali gani kiafya?

Msipotuambia tunampango wa kwenda mahakamani kuiomba ili watanzania wote kwa pamoja tuanze kumsaka popote alipo - maana yeye ndiye tulimchagua awe kiongozi wetu sasa kwa nini mumfiche?
Kuna shuguli gani kubwa inayomlazimu yeye kujitokeza hadharani? Yaani uvumi muuanzishe nyinyi mitandaoni afu yeye ajitokeze Ili kuwa jibu? Nyinyi ndo mlitakiwa mlete ushahidi Ili tuamini kuwa mnachokisema ni cha ukweli.
 
Hao wahuni ndio wanawaamisha hayo sasa hivi?

Kila mtu ana haki ya kusikiliza na kuamini lolote toka kwa yeyote....

Kama unapenda kusikilizwa na kisha uaminiwe, basi jenga mazingira ya kuaminiwa...!!

Serikali hii na viongozi wake wote credibility yao ya kuaminiwa ni ZERO...

Wamejengwa ktk msingi wa propaganda, hofu, mashaka na uongo mpaka mwisho.....
Kwani ni nani aliesema Rais anaumwa? Hao waliosema anaumwa ndo wanatakiwa wathibitishe kauli zao.

Wala haihitajiki mtu kusema wala ku - prove chochote. The fate itself will soon prove everything....

Kwani atazikwa hukohuko kama The former BoT Governer Mr Daudi Balali...?

No sooner or later, The Casket (Jeneza) will prove it all....!!
 
Back
Top Bottom