Zitto Kabwe: Nani anaongoza nchi yetu?

Zitto Kabwe: Nani anaongoza nchi yetu?

Hii ni nchi ya ajabu sana..........

Eti mtu kuhoji tu hali ya afya ya Rais wetu kwa hivi sasa, anafunguliwa mashitaka ya jinai!

Wakati Katika ya nchi ipo wazi kabisa, katika ibara ya 18, inasema kila mwananchi anapaswa kupewa taarifa muhimu zinazohusu nchi yake
 
CCM acheni tabia yenu ya kuficha ficha ugonjwa - ficha yote hapa duniani ruksha ila siyo maradhi - maana maradhi yana tabia ya kuumbua.

Watanzania hawa wanataka kujua:-

1. Je Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo wapi?
2. Na ana hali gani kiafya?

Msipotuambia tunampango wa kwenda mahakamani kuiomba ili watanzania wote kwa pamoja tuanze kumsaka popote alipo - maana yeye ndiye tulimchagua awe kiongozi wetu sasa kwa nini mumfiche?
 
Na wewe zitto ni walewale lengo lao kuleta hali ya wasiwasi na mfarakano nchini kwa njia ya uzushi. Huu uzi wako wala haukua na ulazima ila unaendeleza tu malengo ya wapinga maendeleo. Viongozi wakuu wa nchi wameeleza rais yuko kazini ila vibaraka wanataka rais eti ajitokeza hadharani ili kuonesha sio mgonjwa. Huu ni uchokozi wa kusudi kwa dola ya wananchi kwa sababu hakuna sababu yoyote kuhisi rais ni mgonjwa. Itafika mahali wananchi tutataka wazushi na wale wenye kuwaunga mkono wachukuliwe hatua kabambe maana sheria za kuwawajibisha zipo.
 
Mkitaka kujua Rais yu wapi hakuna haja ya kutumia nguvu kubwa😂🤣😀
Ombeni ugeni mkubwa wa Rais eg India, chancellor ujerumani ama waziri mkuu wingereza au hata Baba mtakatifu aje Tanzania tuone ni protocol ipi itazingatiwa kumkaribisha Kati ya mgeni wetu pendwa noted
Najaribu kuwaza kwa sauti🤣🤣🤣😂😅😅
 
CCM acheni tabia yenu ya kuficha ficha ugonjwa - ficha yote hapa duniani ruksha ila siyo maradhi - maana maradhi yana tabia ya kuumbua.

Watanzania hawa wanataka kujua:-

1. Je Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yupo wapi?
2. Na ana hali gani kiafya?

Msipotuambia tunampango wa kwenda mahakamani kuiomba ili watanzania wote kwa pamoja tuanze kumsaka popote alipo - maana yeye ndiye tulimchagua awe kiongozi wetu sasa kwa nini mumfiche?
Rais watanzania anatakiwa kuwa wapi?
 
Back
Top Bottom