Zitto Kabwe mwenyekiti mpya kamati ya PAC

Zitto Kabwe mwenyekiti mpya kamati ya PAC

Ukweli utakuweka huru daima zzk,,, BADO SIJARIDHIKA NA UFUATILIAJI WAKO JUU YA TSN HILI SHIRIKA LA HABARI LA UMMA LINATUMIA KODI ZETU VIBAYA SAAAAAAAAAAAAAANA,,EBU IWE NDIYO MAIN TASK OF PAC EVEN 45% PLZ,PLZ,PLZ, KAMANDA
 
Hongera mheshimiwa Zitto, wale waliokuwa wamekata tamaa baada ya POAC kufutwa, sasa matumaini yamerudi. Tunakuaminia, kachape kazi kijana.
 
Tunakutakia kazi njema,usimamie rasilimali zetu ili tuweze kuondokana na huu wimbo wa umasikini tunaopandikizwa sisi watz wakati sio.
 
hongera kamanda zito. tunategemea mambo mazuri toka kwako for the benefit of our country and party.
 
Hongera sana zito kijana mwenzetu kwa kweli nakupongeza sana na ujue vijana wengi tunakukubali sana nakuombea kwa mungu utende mema kwa nchi yako ili vizazi vijavyo visome historia yako kama kijana shujaa na mpigania haki wa kweli.usiwazi madaraka wala usikubali wakuhadae ukapoteza heshma iliyoko kwako hivi sasa.Nina amini hata mwenyenzi mungu humbariki mtu mwenye nia njema.hakika nakuhakikishia utaweka historia kwa taifa letu.Tazama jinsi ambavyo majina ya watu kama nyerere,mandela,samora machel,kwame nkruma,indira ghandi na mengine yanavyotukuzwa japo wenyewe hawapo,kuwa mtu mwenye kukusudia kuweka historia safi kwa nchi yako kwa vizazi vijavyo .MUNGU AKUBARIKI SANA ZITO KABWE .
 
Ng'wamapalala unataka kutuambia kwamba huna taarifa kuwa party caucus ya ccm ndo iliamua kumpa uenyekiti wa PAC kamanda Zitto?? usitake kuhadaa watu hapa na ngonjera zako, na tunajua ni kwanini ccm wameamua kumchagua zitto na kumtupa kapuni mwanachama wao wa mlango wa uani mzee cheyo.
Ndiyo maana nikasema, CCM imeamua kufanya hivyo ili kuonyesha kile ambacho kilipelekea mpaka maandamo kwa baadhi ya wanaCHADEMA zilikuwa ni kelele ambazo hazina mashiko.

Kama CCM ingetaka kumtupa kwenye kapu Mh. Zitto, ingefanya hivyo bila hata kufumba mboni zake. Spika alikuwa ana uwezo wa kumpeleka Mh. Zitto hata kwenye kamati ya bunge ya UKIMWI bila hata ya kutaka kushindanisha kwenye kura na kuweka watu inaotaka PAC.
 
Hongera Zitto Kabwe, Tunajarajia matokeo ya Uchapakazi Wako kama ilivyo kawaida.
Mhe Zitto Kabwe ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa kamati ya hesabu za Serikali (PAC) baada ya kumbwaga Mhe. Cheyo kwa kupata kura 13 kati ya 17.

Zitto awali alikuwa ni mwenyekiti wa POAC, kamati iliyovunjwa siku chache zilizopita na kuunganishwa na kamati ya PAC.

Binafsi nampongeza Zitto na kumtakia utendaji mzuri kwenye majukumu yake hayo mapya. Taifa linamtegemea.
 
Ndiyo maana nikasema, CCM imeamua kufanya hivyo ili kuonyesha kile ambacho kilipelekea mpaka maandamo kwa baadhi ya wanaCHADEMA zilikuwa ni kelele ambazo hazina mashiko.

Kama CCM ingetaka kumtupa kwenye kapu Mh. Zitto, ingefanya hivyo bila hata kufumba mboni zake. Spika alikuwa ana uwezo wa kumpeleka Mh. Zitto hata kwenye kamati ya bunge ya UKIMWI bila hata ya kutaka kushindanisha kwenye kura na kuweka watu inaotaka PAC.

Spika makinda amefanya mgawanyo wa wabunge katika kamati mbalimbali kwa maelekezo ya chama chake. Na chama chake ndicho kimeamua kumpa uenyekiti wa PAC zitto kwahiyo hoja ya msigi inabaki pale pale kama nilivyokueleza hapo awali.

Wamefanya hivyo kwa nia moja tu ambayo iko wazi siku zote, wanajaribu kumtumia kufanikisha mipango yao ya siri ambayo sasahivi si siri tena.
 
Mhe Zitto Kabwe ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa kamati ya hesabu za Serikali (PAC) baada ya kumbwaga Mhe. Cheyo kwa kupata kura 13 kati ya 17.

Zitto awali alikuwa ni mwenyekiti wa POAC, kamati iliyovunjwa siku chache zilizopita na kuunganishwa na kamati ya PAC.

Binafsi nampongeza Zitto na kumtakia utendaji mzuri kwenye majukumu yake hayo mapya. Taifa linamtegemea.

Huwa sitaki kabisa kuweka mategemeo ya Taifa kwa mtu mmoja. Tumpe Hongera lakini pia akumbushwe kwamba u-kigeugeu kama aliojaribu kuonyesha pale Tanesco, Nooooo!

Hizi kamati pia nina mashaka nazo sana! Yabidi warudishe mtindo wa kuingiza wataalamu toka nje ya Bunge maana naona kama Bunge linajaribu kuwa na utaalamu wa kila kitu wakati tuonavyo, hali yao kichwani wengi ni mbaya na hawako tayari kuazima washauri.
 
Huwezi kumsikia akilalamika tena na kusema majukumu ya PAC ni mengi kama alivyosikika baada ya kuvunjwa kwa POAC.

Huwezi kumsikia tena akisema hizi ni njama za serikali kudhoofisha upinzani kuimulika serikali.

Huwezi kumsikia tena akisema Spika anafanya kazi kwa maagizo ya CCM.

Huwezi kumsikia tena akisema wajumbe wa kamati ya PAC wanaendekeza uchama badala ya utaifa.
Hawa ndiyo wanaSiasa wetu na yule ndiyo spika wa bunge.

Siasa ni ''the art of the possible/realpolitik''.
Mkuu,moja ya tafsiri ya dhana ''siasa'' ni ''the art ot the possible'' ama ''realpolitik''.Kwa sababu hiyo,basi,madai yako,ingawa yanaweza, kwa haraka haraka,kuonekana yana chembe za usahihi,mara moja,yanapoteza maana na uzito.Siasa,kama sanaa ya yale yawezekanayo, mara nyingi,humaanisha matokeo yanayopatikana baada ya mpambano kati ya kanuni,misingi,itikadi,tunu,falsafa,imani,kwa upade mmoja na uhalisia unaotokana na minyumbuliko na mabadiliko ya kimazingira katika uwanja wa kisiasa kwa upande mwingine.Kwa maneno mengine,dhana ya ''realpolitik''/the art of the possible,huweza kumaanisha ''pragmatism''.Kwa mfano,chama cha kisiasa kinachoingia katika uchaguzi huku kikinuia kupata wabunge 350 na kisha baada ya matokeo kupata Wabunge 190,idadi ya chini,kadiri ya matarajio/malengo kilichojiwekea,hufikia uamuzi wa kukubaliana na uhalisia,kwa kuwa, hiyo ndiyo idadi ya nafasi kilichoweza kuzipata kwa mujibu wa kura -tukichukulia mchakato wa uchaguzi ulikuwa ni huru na haki-.Kuukataa ukweli kuwa lengo la kupata wabunge 350 halikuweza kufikiwa, ni jaribio la kukigeuza kile kilichoshindikana kiwezekane.Busara na hekima kwa pamoja,vinaelekeza ulazima wa kukubali matokeo yaliyopatina.
Bora nusu shari kuliko shari kamili.
Kwa kuwa,kama baadhi yetu tunavyoamni,kulikuwa na nia ya wazi ya Spika kumpokonya nafasi yake,Ndugu Zitto pamoja na chama chake ushawishi na nguvu katika siasa za kibunge na zile za kitaifa,kutokana na uamuzi wake wa kuivunja kamati ya POAC,na hivyo kuwepo ulazima wa mchakato mwingine wa kupata Mwenyekiti mpya wa kamati ya PAC ya sasa,na kwa kwa kuwa ni dhahiri kulikuwa na hatari ya kweli kwa Zitto kupoteza nafasi yake ya katika Kamati mpya ya PAC aliyokuwa akiwania, - iwapo Wabunge wa CCM wanaounda kamati ya PAC wangeamua kupiga kura kwa kuongozwa na maslahi mafinyu ya kisiasa - ,basi,kuliko Zitto kukosa nafasi hiyo,bila kujali muundo na majukumu mapya na tofauti na yale ya iliyokuwa POAC,mtu yeyote makini atafuarahia ushindi wa leo wa Zitto.
Mwisho kabisa, dhana ya siasa yenye maana ya ''the art of the possible'' aghalabu huendana na compromises na sacrifices za hapa na pale,hali inayohusisha ulazima na utayari wa ''kutoa'' na ''kupokea''.Ni wazi,kuwa,Ndugu Zitto,kama mwakilishi wa wananchi, hakuwa na uwezo wa kukataa uamuzi wa Spika kuvunja POAC lakini amekuwa tayari kukubali na kupokea nafasi aliyopata kama mwenyekiti mpya wa PAC.Mwanasiasa mwerevu huridhika kupata kile kinachwezekana kwa kuzingatia minyukano ya kisiasa,mivutano iliyopo katika mifumo ya kisiasa ambazo aghalabu huongozwa na tofauti za kiitikadi,kifalsafa,kiimani,kimalengo na kimwelekeo.Kwa hiyo,ni dhahiri kusingekuwa na sababu ya kupoteza muda kuendelea kutafuta kile kisichowezekana.

Kila la kheri mkuu, hongera pia Mungu akujalie afya njema ili uweze kutekeleza wajibu wako bila wasiwasi binafsi nakukubali we ni jembe la ukweli!
 
Spika makinda amefanya mgawanyo wa wabunge katika kamati mbalimbali kwa maelekezo ya chama chake. Na chama chake ndicho kimeamua kumpa uenyekiti wa PAC zitto kwahiyo hoja ya msigi inabaki pale pale kama nilivyokueleza hapo awali.

Wamefanya hivyo kwa nia moja tu ambayo iko wazi siku zote, wanajaribu kumtumia kufanikisha mipango yao ya siri ambayo sasahivi si siri tena.
Mkuu Mwita Maranya wewe kweli ni nguli wa siasa za Tanzania, halafu kwa jinsi Mkurya alivyobarikiwa ubishi, The package is complete. Hukosi hata kidogo pa kutokea.

Sasa kama CHADEMA walilijua hilo, kulikuwa kuna umaana gani wa kushadadia wakati Mh. Zitto anapiga kelele 'kunyang'anywa' POAC huku wakimtuhumu Mzee Mapesa kutaka kupewa PAC kama kibaraka wa CCM. Hawakujua kama Mh. Zitto anaweza kuwa pia kibaraka kama Mzee Mapesa au ndiyo political blindness ndani ya chama.
 
Last edited by a moderator:
Maelekezo toka CCM partycocus! Mana wangemwaga jamaa wananchi tungeichukia zaidi CCM coz tungeamini CHADEMA kaonewa! HONGERA Z. Z. Kabwe.

Hayo ni maelekezo toka kwa baba MwanaAsha hakuna cha party caucus wala nini!! He did it last time and he has instructed them this time again.
 
Spika makinda amefanya mgawanyo wa wabunge katika kamati mbalimbali kwa maelekezo ya chama chake. Na chama chake ndicho kimeamua kumpa uenyekiti wa PAC zitto kwahiyo hoja ya msigi inabaki pale pale kama nilivyokueleza hapo awali.

Wamefanya hivyo kwa nia moja tu ambayo iko wazi siku zote, wanajaribu kumtumia kufanikisha mipango yao ya siri ambayo sasahivi si siri tena.

Duh! Chadema mna matatizo haswaa, no wonder mipango ya kumzuru kwa mambo yenu haya ya hisia mnazojitungia yanabumburuka. Inabidi ifike mahali mumkubali tu Zitto, kumsambazia habari za uongo na Mungu anawaona...
 
Huwa sitaki kabisa kuweka mategemeo ya Taifa kwa mtu mmoja. Tumpe Hongera lakini pia akumbushwe kwamba u-kigeugeu kama aliojaribu kuonyesha pale Tanesco, Nooooo!

Hizi kamati pia nina mashaka nazo sana! Yabidi warudishe mtindo wa kuingiza wataalamu toka nje ya Bunge maana naona kama Bunge linajaribu kuwa na utaalamu wa kila kitu wakati tuonavyo, hali yao kichwani wengi ni mbaya na hawako tayari kuazima washauri.
Mkuu jifunze kuheshimu maoni ya watu nawe kutoa yako unavyoona inafaa
 
Back
Top Bottom