Zitto Kabwe mwenyekiti mpya kamati ya PAC

Zitto Kabwe mwenyekiti mpya kamati ya PAC

Hongera Kamanda Zitto Kabwe, Sasa Kazi na Uzi ni Ule Ule, Kufanya Kazi kwa Bidii na Kututumikia Sisi Wananchi.
Kila la Kheri.

Mhe Zitto Kabwe ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa kamati ya hesabu za Serikali (PAC) baada ya kumbwaga Mhe. Cheyo kwa kupata kura 13 kati ya 17.

Zitto awali alikuwa ni mwenyekiti wa POAC, kamati iliyovunjwa siku chache zilizopita na kuunganishwa na kamati ya PAC.

Binafsi nampongeza Zitto na kumtakia utendaji mzuri kwenye majukumu yake hayo mapya. Taifa linamtegemea.
 
nyabhingi kama una maelekezo ya POAC ambayo wewe na bodi ya shirika lako hamjafanyia kazi bora ukaanze utekelezaji maana kamati ya PAC sasa inashighulika na hesabu za mashirika ya umma (PSPF/TANESCO yako) na Serikali kuu (Hesabu za Wizara).

Kazi itakuwa rahisi wizara ikisema imepeleka pesa xxxxx tanesco wao wataangalia tu hesabu za Tanesco kama hizo pesa XXXXX zimefika
MKUU Ndachuwa JIBU LAKO LINA VITISHO LAKINI LIMENIELIMISHA..THANKS
 
big up zitto imani yangu kwako ni kubwa kama mlima kilimanjaro
 
Sasa ndo kifo kina karibia watakulegezea mpaka matairi
 
  • Thanks
Reactions: PhD
Bila kutilia maanani mielekeo ya kiitikadi na kifalsafa inayokinzana miongoni mwetu,taarifa hii inapaswa kumvutia yeyote anayeamini katika uwajibikaji,uadilifu,weledi na utawala bora.Hapana shaka,hatua hii itaambatana na taathira chanya katika namna tunavyoendesha shughuli za kisiasa hapa nchini.Aidha,siasa na mwelekeo wa chama cha siasa anachotoka mshindi,umepata msukumo na kani mpya ikiwa tunatambua na kuelewa nafasi na nguvu ya siasa za kibunge katika siasa za kitaifa na zile za mahali.
Kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo,kama taasisi ya kisiasa enye nia ya kweli ya kukamata dola,ushindi wa Ndugu Zitto,ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu katika chama hicho,ni ishara kuwa,upigaji kura,kwa kiasi kikubwa,ulizingatia uthabiti katika mikakati yake,umakini katika utendaji wake,na uimara na umadhubuti wa kitaasisi katika nia yake ya dhati katika usimamizi wa rasilimali za umma.Yapata mwezi mmoja uliopita,Spika Makinda,bila shaka,akiitikia maelekezo ya wapambe,wanachama na wafukutwa wa chama chake,aliamua kuivunja kamati ya PAOC kwa matarajio kuwa hatua hiyo ingefifisha nguvu na ushawishi wa Ndugu Zitto na ule wa chama chake kwa ujumla.Sasa,ni dhahiri,amethibisha,yeye mwenyewe ,kwa mara nyingine tena,jinsi isivyo kazi rahisi kupambana na kisha kuishinda NGUVU YA UMMA.
Wabunge,wengi wao wakiwa wa CCM,walioamua kutoa kura zao kwa Zitto wanastahili pongezi,kwa kuwa,pamoja na hatari ya kweli kwa chama chao kukabidhi madaraka kwa CHADEMA ifikapo mwaka 2015 kuwa dhahiri,wameamua kuitikia mahitaji,matamanio na matakwa ya wapiga kura wao ambao wengi wao wanaishi katika hali ya umaskini uliokithiri,huku wakisumbuliwa na maradhi yanayoepukika na papo hapo ujinga ukiwa umepiga kambi ya kudumu katika bongo zao.
Inaweza kudaiwa kwa uhakika kabisa kuwa,Uchaguzi wa leo,ulihusu maamuzi kati ya uwajibikaji dhidi ya uzembe;weledi dhidi ya ubabaishaji na nguvu ya hila na fitna dhidi ya Nguvu ya Umma
.
 
Hongera onyesha umahiri wako,.By the way ulisema hutagombea tena Ubunge umeshaandaa mazingira ya kulibakiza jimbo lako mikononi mwa chadema??likipotea 2015 nitakuwa wa kwanza kukulaani!!
 
Nafasi nzuri kumweka sawa katika mbio za kugombea uraisi mwaka 1015 kupitia CDM ni vizuri Babu akapumzika.
 
FortJeasus wakikusikia wanawezakusema uchaguzi urudiwe; inaelekea wabunge wa CCM hawakupewa maelekezo maalumu au hawajui kwanini POAC ilivunjwa
 
Last edited by a moderator:
Gud move dogo, kila la kheri na kazi mpya, walidhani umekwisha kumbe ndo kwanza kumekucha, waôngezee spidi ili 2015 tuwang'oe hawa vijeba
 
Huwezi kumsikia akilalamika tena na kusema majukumu ya PAC ni mengi kama alivyosikika baada ya kuvunjwa kwa POAC.

Huwezi kumsikia tena akisema hizi ni njama za serikali kudhoofisha upinzani kuimulika serikali.

Huwezi kumsikia tena akisema Spika anafanya kazi kwa maagizo ya CCM.

Huwezi kumsikia tena akisema wajumbe wa kamati ya PAC wanaendekeza uchama badala ya utaifa.

Hawa ndiyo wanaSiasa wetu na yule ndiyo spika wa bunge.
 
Sheikh Yahya aliacha vijana wa kazi wengi.Hongera kwa utabiri huu kwa ZZK.
 
Waaaaaoooooooooooooooooh.....! hadi kieleweke, VIVA CHADEMA. Huyo Cheyo naye alishalewa madaraka na kujiona kama mwana-CCM, wacha akapumzike huko Bariadi!
hahaha.....umenipa raha aisee....Hongera kwa Zitto Kabwe
 
Huwezi kumsikia akilalamika tena na kusema majukumu ya PAC ni mengi kama alivyosikika baada ya kuvunjwa kwa POAC.

Huwezi kumsikia tena akisema hizi ni njama za serikali kudhoofisha upinzani kuimulika serikali.

Huwezi kumsikia tena akisema Spika anafanya kazi kwa maagizo ya CCM.

Huwezi kumsikia tena akisema wajumbe wa kamati ya PAC wanaendekeza uchama badala ya utaifa.

Hawa ndiyo wanaSiasa wetu na yule ndiyo spika wa bunge.

Ng'wamapalala unataka kutuambia kwamba huna taarifa kuwa party caucus ya ccm ndo iliamua kumpa uenyekiti wa PAC kamanda Zitto?? usitake kuhadaa watu hapa na ngonjera zako, na tunajua ni kwanini ccm wameamua kumchagua zitto na kumtupa kapuni mwanachama wao wa mlango wa uani mzee cheyo.
 
Last edited by a moderator:
Hata sisi tunasema hongera sana mh. Filikunjombe kwa kuendelea kuwa makamu wa zitto katika kamati hiyo hiyo kwa kura hizo hizo
 
Back
Top Bottom