Zitto Kabwe mwenyekiti mpya kamati ya PAC

Zitto Kabwe mwenyekiti mpya kamati ya PAC

Mwanachama pekee wa upinzani ninayekukubali kwakuweka maslahi ya wananchi na taifa lako mbele kuliko chama chako. Hongera kwa ushindi wako ambao naamini umeupata kwakuwa wewe ni mweledi wa kusimamia wizara na mambo ya msingi yanayohusu mustakabali wa taifa letu na watanzania.
Kazi njema mh zzk.
Maneno yanaonyesha kuficha ukweli Jakaya na Makinda wamewaambia wana CCM kwenye coccus yao bado ana mission mwenyewe anajua baada ya masalia kuumbuliwa lazima apewe wadhifa akiwa ndani yap
 
Who the Cap fit let them wear it. huyu jamaa siku akigombea urais mie kura yangu anayo kwa hakika hongera mdogo wangu Zito.



Mhe Zitto Kabwe ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa kamati ya hesabu za Serikali (PAC) baada ya kumbwaga Mhe. Cheyo kwa kupata kura 13 kati ya 17.

Zitto awali alikuwa ni mwenyekiti wa POAC, kamati iliyovunjwa siku chache zilizopita na kuunganishwa na kamati ya PAC.

Binafsi nampongeza Zitto na kumtakia utendaji mzuri kwenye majukumu yake hayo mapya. Taifa linamtegemea.
 
Mkuu mwitaMaranya maadam umesema unaangalia kwa jicho la 3 naomba nikuulize...
Slaa alipokuwa mwenyekiti wa LAAC ni CCM waliagizwa wampigie kura?
Unazungumzia Mnyika na Lema kuhamishwa kamati ina maana haujaona kwamba Mbowe kaamishwa kamati, Silinde kahamishwa kamati? Zitto kamati yake imevunjwa achilia mbali kuhamishwa.
Mbona Sugu kabaki kamati yake ile ile na hatusemi?
Spika kampelecha mxh. Natse na Philip Mturano kamati ya. LAAC, bila haya wote wawili toka chama kimoja wamesimama kugombea nafasi ya uenyekiti, matokeo yake CUF wameshinda nafasi hiyo. Hii ni aibu kubwa kwa chama kufanya mambo kama haya. Mkae vhini kujitafakari badala ya kutafuta mchawi! Zitto ni jitihada zake zimemfanya ashinde, wakati nyie mnakaa kupiga majungu na kutafuta mchawi mwenzenu anapiga kazi

nice 2 acha porojo arifu.
Kwa composition ya bunge letu tangu 1995 hadi sasa huwezi kuwa mwenyekiti wa kamati bila ridhaa ya ccm na hilo halihitaji kuwa na degree ya uchumi kulitambua.
Mimi ni mwanachadema lakini nasema huwezi kumlinganisha Silinde na Lema au Natse na Mnyika!
 
Last edited by a moderator:
Safi sana serikali na bunge kwa kufanya jambo sahihi
 
Bora nusu shari kuliko shari kamili.
Kwa kuwa,kama baadhi yetu tunavyoamni,kulikuwa na nia ya wazi ya Spika kumpokonya nafasi yake,Ndugu Zitto pamoja na chama chake ushawishi na nguvu katika siasa za kibunge na zile za kitaifa,kutokana na uamuzi wake wa kuivunja kamati ya POAC,na hivyo kuwepo ulazima wa mchakato mwingine wa kupata Mwenyekiti mpya wa kamati ya PAC ya sasa,na kwa kwa kuwa ni dhahiri kulikuwa na hatari ya kweli kwa Zitto kupoteza nafasi yake ya katika Kamati mpya ya PAC aliyokuwa akiwania, - iwapo Wabunge wa CCM wanaounda kamati ya PAC wangeamua kupiga kura kwa kuongozwa na maslahi mafinyu ya kisiasa - ,basi,kuliko Zitto kukosa nafasi hiyo,bila kujali muundo na majukumu mapya na tofauti na yale ya iliyokuwa POAC,mtu yeyote makini atafuarahia ushindi wa leo wa Zitto.[/FONT]
Mkuu ninakubaliana na maelezo yako mengine lakini kwenye hiki kipande tukubali kutokubaliana. Unapoanza kujenga hoja kwa hisia na maneno ya kuvuma, hata hoja nayo inakuwa fallacy. Kwa nini tunashindwa kuamini kile Spika alikisema kuhusiana na hilo?. Kama kweli Spika alitaka kumnyang'anya POAC, hakukuwa na sababu ya kuivunja, spika alikuwa na Uwezo wa kumhamisha tu kwenye hiyo kamati na kumpeleka hata kwenye kamati ya masuala ya Ukimwi au huduma za jamii. Na kudhihirisha kama hiyo haikuwa ni sababu, kwa sasa imewekwa kwenye kamati ya PAC na wajumbe ambao wengi ni wa CCM, wamempa kura kuwa mwenyekiti.

Mimi ninaamini kuvunjwa kwa POAC kumetokana na sababu zingine lakini siyo hii unayosema ya kutaka Mh. Zitto akose kamati ya kuisimamia kama mwenyekiti.

Tukubali kutokubaliana katika hili.
 
Duh! Chadema mna matatizo haswaa, no wonder mipango ya kumzuru kwa mambo yenu haya ya hisia mnazojitungia yanabumburuka. Inabidi ifike mahali mumkubali tu Zitto, kumsambazia habari za uongo na Mungu anawaona...

Huyo ccm na sio cdm inabidi tuwe makini na watu wanaojifanya chadema kumbe ccm wapo kwa ajiri ya kumchafua zitto inchi hii tukiacha unafiki nani asiyemkubali zitto kuanzia wabunge wote hata wa ccm mpaka wanainchi acheni unafiki
 
This's what I was waiting.....i got scared when I saw the voters list...I thought they'd be ki-CCM zaidi!!
 
Nilikuwa namkubali sana mheshimiwa Cheyo kwenye kamati yake ambayo ilikuwa ikifanya vitu kwa utulivu bila papara na jazba hope na Zitto ataendeleza mazuri ya Cheyo.
 
Zitto anatumiwa na magamba kwa kazi fulani na chadema isipoangalia huyo ndio atakayeisambaratisha kwa kuvujisha siri za chama.
 
Back
Top Bottom