Zitto Kabwe mwenyekiti mpya kamati ya PAC

Zitto Kabwe mwenyekiti mpya kamati ya PAC

Huyo ccm na sio cdm inabidi tuwe makini na watu wanaojifanya chadema kumbe ccm wapo kwa ajiri ya kumchafua zitto inchi hii tukiacha unafiki nani asiyemkubali zitto kuanzia wabunge wote hata wa ccm mpaka wanainchi acheni unafiki

Asante mkuu kwa kunifumbua macho
 
Kudos ZItto,

Naona leo wabaya wako wamefyata.

Napiga picha maneno ambayo wangeandika hapa pindi ungekosa hiyo nafasi.

Kwakweli inasikitisha, yani wako radhi chadema ikose mwenyekiti kabisaa kwenye kamati zote kuliko apate ZITTO
 
Mhe Zitto Kabwe ameibuka kidedea kwenye uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa kamati ya hesabu za Serikali (PAC) baada ya kumbwaga Mhe. Cheyo kwa kupata kura 13 kati ya 17.

Zitto awali alikuwa ni mwenyekiti wa POAC, kamati iliyovunjwa siku chache zilizopita na kuunganishwa na kamati ya PAC.

Binafsi nampongeza Zitto na kumtakia utendaji mzuri kwenye majukumu yake hayo mapya. Taifa linamtegemea.
Saafi sana tu!
 
Back
Top Bottom