Kama mjadala umefungwa, mbona viongozi wanaendelea kutoa matamko na wanasambaza ripoti ya siri juunya zitto kabweMjadala umefungwa na tunasubiri siku ziishe haya yote unayohubiri yatapata muafaka!!!!!!!
You never step on a snake and relax on there!!!!
Character X, naomba nikuulize jambo moja tu; kama leo uchaguzi huru ungefanyika Chadema na upande wa MM, M1, M2 na M3 usiibuke kidedea, unadhani huo upande ungekubali kubaki ndani ya Chadema chini ya uongozi ule ule walioushutumu kwenye waraka na kupanga njama za siri kuuondoa madarakani?
Shujaa gani anayeogopa mapambano? Kumwambia Zitto aondoke CHADEMA ni sawa na kuomba adui ajitoe eneo la vitaNakuunga mkono kamanda huo ni ushauri wa kishujaa.
Inawezekana kabisa una hoja, ila umeiua hoja yako mwenyewe kwa kufanya uchambuzi wa upande mmoja (biased analysis) ambao bila shaka yoyote hitimisho lako litaegemea upande mmoja. Kwa nini nasema hivyo; ni kwa kuwa uchambuzi wako umeegemea katika maelezo na utetezi unaoaminika umetoka kwa mtuhumiwa Mh. Zitto Zuberi Kabwe!
Kwa haraka haraka niseme sijaona umechambua vipi tuhuma alizoelekezewa; kwa mfano kupokea pesa kutoka serikali inayoongozwa na chama pinzani, kuzigawa pesa hizo kwa baadhi ya watu ndani na nje ya chama wanaoaminika ni mamluki, kuwa na mawasiliano ya siri na taasisi nyeti za usalama mawasiliano yanayothibitisha mipango ya siri ya kukihujumu chama, n.k.
Pengine ungejaribu kuzichambua tuhuma zinazomkabili angalau nusu yake, ukaleta uchambuzi wa utetezi alioutoa kwa kila tuhuma aliyoelekezewa, kisha ukatoa hitimisho (conclusion) binafsi ningeona thread yako iko neutral kama nilivyo neutral (sina upande) katika kinachoendelea ndani ya CDM lkn sina upande katika siasa za nchi hii, bali kukweli wa moyo wangu nina upande katika maslahi mapana ya nchi yangu na watu wake.
waraka unaoutumia hauwezi kua authority ya kujengea hoja kwasababu haujathibitishwa na upande wowote kuwa kweli. Kuna kila dalili kwamba ni "hekaya" batili tu.
Hebu jaribu kujenga hoja yako kwakuonyesha evidence yoyote ya CCM kumtumia zitto.
What do you mean taifa zima? Hakuna chama cha taifa zima. Zitto is a perfect child of two worlds- ya upinzani na chama tawala the reason why anakuwa msaliti. Either he belongs to the ruling party or to the opposition. If he is in both worlds he must be a traitor. You cannot serve two masters.
Niliwahi kuona hiii.... Sijui na yenyewe ni hekaya au vipi lakini nimegundua kuwa wanasiasa ni watu wa ajabu kuliko watu wengine duniani.
Hayo uliyoandika ni tuhuma tu anazozushiwa Zitto na hazina uthibitisho wowote. Ni sawa na wewe ukaibuka na kusema Mbowe na Tundu Lissu wajiuzulu kwa vile ni mashoga na CDM haikubali viongozi mashoga, wakati huna ushahidi wowote.
Chadema ni ya zitto bila zitto hakuna chadema wakumfukuza chadema hayupo hoja zake hakuna kiongozi yoyote wa chadema anawezazipangua hoja zake.
Chadema ni ya zitto bila zitto hakuna chadema wakumfukuza chadema hayupo hoja zake hakuna kiongozi yoyote wa chadema anawezazipangua hoja zake.
Mtu ambaye unamaadili unatumiwa vipi kumzushia mtu? Halafu utegemee anayekutumia akuamini kuwa hutatumiwa na mwingine. Ndio maana sishangai kusikia waliamua kufuatilia nyendo zake.
Hapo kuomba radhi kwenye postmorten sijakuelewa, unaomba radhi maiti au? Ni dini gani inafundisha hivyo hizi za mapokeo au za asili?
Tatizo kuna vitu vinakuwa too ugly..hadi hata marafiki waamue kukupa pole n akusema masikitiko yao.Zitto kaamua fanya kila kitu too ugly.
Kwa jinsi CDM wamejitahidi kumkwepa ili amalize yote kwa akilo yake,bado aklifikisha hapa.Hakuna njia Zitto lazima atoke kabisa.Pengine wanachoweza fanya CDM na km nimelisikia ni kukata mjadala wa kumdhalilisha Zitto zaidi km sehmu ya kujali ile kumbukumbu nzuri waliyo nayo.