KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,139
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, ni kama vile ndiye ‘nyota' wa mkutano uliopita wa Bunge na hasa baada ya kuwataka wabunge kutia saini zao kwa lengo la kutaka kumpigia kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutokana na ripoti za CAG kuonyesha ufisadi unaojirudia kila mwaka miongoni mwa taasisi za umma.
Zitto ambaye ameshikilia rekodi yake ya kuwa kinara wa mikutano miwili mfululizo ya Bunge, akiibuka na pingamizi la posho kwa wabunge katika mkutano Februari, mwaka huu na sasa, akiibuka na ajenda ya ‘kumng'oa' Waziri Mkuu, hoja zote zikipata ushabiki ndani na nje ya Bunge, amelifanya Bunge kuwa na rekodi ya kipekee lakini pia, hatua yake ya kutaka Waziri Mkuu ang'olewe inampa nguvu zaidi CAG tofauti na wengi wanavyotafsiri.
Zitto mwenyewe ameeleza: "Vyovyote itakavyokuwa, kufanikiwa au kutofanikiwa kumng'oa Waziri Mkuu, ripoti za CAG zitaheshimiwa kwa kufanyiwa kazi ili makosa ya ufisadi yasiwe yanajirudia na yakijirudia basi, siku nyingine Waziri Mkuu atang'oka, rekodi zimeshajiandika."
Zitto alifanikiwa kukusanya saini za wabunge 73, ambao ni kutoka vyama karibu vyote vyenye wabunge bungeni, isipokuwa UDP tu.