Zitto Kabwe mbunge makini kuliko wote TZ!

Zitto Kabwe mbunge makini kuliko wote TZ!

Status
Not open for further replies.
Zitto ni mzuri sana ila he is too ambitious, kimsingi Mnyika ni mzuri kuliko Zitto, hata mmpambanaji wetu Filikunjombe ni mzuri zaidi ya Zitto .Zitto aache kufanya kazi na magazeti kwanza ili aweze kuwekwa kwenye kundi la wabunge mahiri kabisa kwenye bunge letu
 
zitto ni mzuri sana ila he is too ambitious, kimsingi mnyika ni mzuri kuliko zitto, hata mmpambanaji wetu filikunjombe ni mzuri zaidi ya zitto .zitto aache kufanya kazi na magazeti kwanza ili aweze kuwekwa kwenye kundi la wabunge mahiri kabisa kwenye bunge letu

tatizo la mnyika ni elimu yake ndogo ndio inamcost....
 
Unajua JK na Zitto ninmarafiki??? Nahsi aliyumwa na. Rais ili iwe mbinu ya kubadili baraza!!!!!!!


A great Thinker... chezea Zitto wewe ! ndio maana Chadema kama hawamuamini amin vile...hivi ni nani anaweza kujitolea kama vile bila uoga na nchi hii ilojaa kila aina ya ufisadi ! lazima kutakuwa na kitu hapa na no wonder hata Nkono amesign !
 
tatizo la mnyika ni elimu yake ndogo ndio inamcost....
Mkuu mbona Mnyika ni mchambuzi mzuri sana wa mambo au unataka elimu gani., kwa maana kuna wabunge wengi tu wanaojiita kuwa ni madaktari yaani wanazo Phd, lakini huwezi kuwalinganisha na Mnyika kwa uelewa na hata uchambuzi wa maswala ya kitaifa na kimataifa.
 
Zitto alitumwa na JK na JK anajua kabisa uongozi wake unayumbishwa na Magamba ya CCM sasa anayatumia majembe kama wakina Zitto kutema cheche ile yeye aweze kufanya kazi. Unajua tena ule uenyekiti wa CCM na kuwa chama ndo kinaunda serikali wanambana asiende wanavyotaka wao.

Sasa amemwambia Lema azunguke Nchi nzima aiue CCM ili akija kutoka 2015 Chadema waingie ikulu halafu atawapa siri zote. na kuna kila dalili kuna agreement fulani na sisi wana Chadema kuja kumlinda.

Namnukuu Zitto kule Bungeni wakati anahitimisha ''Mawaziri msimsingizie Raisi na kumchafua kwa uzembe wenu na ubaridhifu wenu wa kushindwa kusimamia mali na pesa za walipa kodi kwa manufaa yenu binafsi i lazima muwajibike na mchukuliwe hatua stahiki''
Mwisho wa kunukuu. Hapa mpepata picha sasa kwamba JK amechoka na magamba sasa anawatumia chama makini kuiokoa nchi hii kutoka mikononi mwa wezi. JK na Zitto ni Dam Dam JK na Chadema ni Dama Dam.


:A S shade::A S shade::A S shade::A S shade::A S shade: kurunzi ya macho
 
usiseme zitto sema chadema ina wabunge makini kuliko wote Tanzania.
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, ni kama vile ndiye ‘nyota’ wa mkutano uliopita wa Bunge na hasa baada ya kuwataka wabunge kutia saini zao kwa lengo la kutaka kumpigia kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutokana na ripoti za CAG kuonyesha ufisadi unaojirudia kila mwaka miongoni mwa taasisi za umma.


Zitto ambaye ameshikilia rekodi yake ya kuwa kinara wa mikutano miwili mfululizo ya Bunge, akiibuka na pingamizi la posho kwa wabunge katika mkutano Februari, mwaka huu na sasa, akiibuka na ajenda ya ‘kumng’oa’ Waziri Mkuu, hoja zote zikipata ushabiki ndani na nje ya Bunge, amelifanya Bunge kuwa na rekodi ya kipekee lakini pia, hatua yake ya kutaka Waziri Mkuu ang’olewe inampa nguvu zaidi CAG tofauti na wengi wanavyotafsiri.

Zitto mwenyewe ameeleza: “Vyovyote itakavyokuwa, kufanikiwa au kutofanikiwa kumng’oa Waziri Mkuu, ripoti za CAG zitaheshimiwa kwa kufanyiwa kazi ili makosa ya ufisadi yasiwe yanajirudia na yakijirudia basi, siku nyingine Waziri Mkuu atang’oka, rekodi zimeshajiandika.”
Zitto alifanikiwa kukusanya saini za wabunge 73, ambao ni kutoka vyama karibu vyote vyenye wabunge bungeni, isipokuwa UDP tu.


Usalama at work,hatuna shida na hilo.Ni furaha yetu sote.
 
Mi nafikiri zitto ni cdm na hata kama anatoa hoja nzito bado anabaki ni cdm,
and ithink ni one among the leaders pale cdm alieifanya cdm iwe hapo ilipo leo.
And to my opinion ni presidential material kwa cdm miaka ijayo 2020 na kuendelea
 
Mkuu mbona Mnyika ni mchambuzi mzuri sana wa mambo au unataka elimu gani., kwa maana kuna wabunge wengi tu wanaojiita kuwa ni madaktari yaani wanazo Phd, lakini huwezi kuwalinganisha na Mnyika kwa uelewa na hata uchambuzi wa maswala ya kitaifa na kimataifa.
Hebu tuwekee cv yake hapa haraka sana ili tuijadili,tatizo vijana wengi siku wanaacha shule na kukimbilia kwenye ubunge na udiwani sababu ya posho na wengine kupata ukuu wa wilaya.
 
"mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni" zitto ana uwezo mkubwa sanawa kujenga hoja zenye mashiko na zinazosimamia katika tafiti na vielelezo halisi. katika hili tusiwe wanafiki kwa kutompa mtu kitu anachostahili.
 
Hebu tuwekee cv yake hapa haraka sana ili tuijadili,tatizo vijana wengi siku wanaacha shule na kukimbilia kwenye ubunge na udiwani sababu ya posho na wengine kupata ukuu wa wilaya.
mkuu naanza kuwa na wasiwasi na uelewa wako , wenye phd wanashindwa kujenga hoja kama hata waliomaliza darasa la saba sasa hiyo cv unayotaka inauhusiano gani na uwezo wa mbunge aliethibitishia umma uwezo usiotia shaka kama mnyika and the likes
 
Chadema ndiyo sera yao kupinga UFISADI zito cdm,hongereni MAGWANDA kwa kuwotoa jasho MAGAMBA watajiju.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom