Massare asema SGR imechukua maeneo ya Watu, Serikali itende haki, iache dhulma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,979
12,298
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 15, Kikao cha 6, leo Aprili 15, 2024.

Ripoti 21 za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), za ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka 2022/2023 zimewasilishwa bungeni.

Kukabidhi ripoti hizo kunakuja baada ya CAG, Charles Kichere kuikabidhi kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Machi 28, 2024 Ikulu, Chamwino jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa ratiba ya shughuli za leo Jumatatu Aprili 15,2024 iliyotolewa na Bunge, ripoti zilizokabidhiwa ni ukaguzi wa taarifa za fedha za Serikali kuu kwa mwaka wa fedha, ukaguzi wa taarifa za fedha za mamlaka za Serikali za mitaa na ukaguzi wa taarifa za fedha za miradi ya maendeleo.

Massare: SGR imechukua maeneo ya Watu, Serikali itende haki, iache dhulma
Mbunge wa Manyoni Magharibi, Yahaya Omary Massare akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu ametoa mapendekezo kuwa Wananchi walioathiriwa kwa maeneo yao kuchukuliwa kupisha Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) Wilayani Itigi Mkoani Singida walipwe kwa haki na katika kiwango kinachoendana na thamani ya ardhi iliyochukuliwa

Mbunge Neema Mwandabila: Kikokotoo hakina tatizo, wanapewa fedha za kutosha

Mbunge wa Viti Maalum, Neema Gerald Mwandabila amesema suala la Kikokotoo limekuwa na kelele nyingi kiasi cha Wananchi wengi kuhisi Serikali inawadhulumu jambo ambalo anaamini si kweli na kuwa kinachokosekana ni elimu juu ya kikokotoo hicho cha kustaafu
 
Mbunge aliyechangia swala kikokotoo hapo nina mashaka kwenye ufahamu wangu iwapo amepangwa aseme hivyo au ni utashi wake umemtuma. Hivi kweli kikotoo kilivyokaa ni cha kuwa na ujasiri wa kukitetea!!??. Ile ni dhuluma ya wazi sema tu ukisema useme sana ni machozi ya samaki kwenye maji
 
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 15, Kikao cha 6, leo Aprili 15, 2024.

Ripoti 21 za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), za ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka 2022/2023 zimewasilishwa bungeni.

Kukabidhi ripoti hizo kunakuja baada ya CAG, Charles Kichere kuikabidhi kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Machi 28, 2024 Ikulu, Chamwino jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa ratiba ya shughuli za leo Jumatatu Aprili 15,2024 iliyotolewa na Bunge, ripoti zilizokabidhiwa ni ukaguzi wa taarifa za fedha za Serikali kuu kwa mwaka wa fedha, ukaguzi wa taarifa za fedha za mamlaka za Serikali za mitaa na ukaguzi wa taarifa za fedha za miradi ya maendeleo.

Massare: SGR imechukua maeneo ya Watu, Serikali itende haki, iache dhulma
Mbunge wa Manyoni Magharibi, Yahaya Omary Massare akichangia Hotuba ya Waziri Mkuu ametoa mapendekezo kuwa Wananchi walioathiriwa kwa maeneo yao kuchukuliwa kupisha Mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) Wilayani Itigi Mkoani Singida walipwe kwa haki na katika kiwango kinachoendana na thamani ya ardhi iliyochukuliwa

Mbunge Neema Mwandabila: Kikokotoo hakina tatizo, wanapewa fedha za kutosha

Mbunge wa Viti Maalum, Neema Gerald Mwandabila amesema suala la Kikokotoo limekuwa na kelele nyingi kiasi cha Wananchi wengi kuhisi Serikali inawadhulumu jambo ambalo anaamini si kweli na kuwa kinachokosekana ni elimu juu ya kikokotoo hicho cha kustaafu

Mbunge neema wa viti maalumu ni tapeli
 
Back
Top Bottom