Zitto Kabwe mbunge makini kuliko wote TZ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto Kabwe mbunge makini kuliko wote TZ!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KIM KARDASH, Apr 28, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto, ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, ni kama vile ndiye ‘nyota' wa mkutano uliopita wa Bunge na hasa baada ya kuwataka wabunge kutia saini zao kwa lengo la kutaka kumpigia kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutokana na ripoti za CAG kuonyesha ufisadi unaojirudia kila mwaka miongoni mwa taasisi za umma.


  Zitto ambaye ameshikilia rekodi yake ya kuwa kinara wa mikutano miwili mfululizo ya Bunge, akiibuka na pingamizi la posho kwa wabunge katika mkutano Februari, mwaka huu na sasa, akiibuka na ajenda ya ‘kumng'oa' Waziri Mkuu, hoja zote zikipata ushabiki ndani na nje ya Bunge, amelifanya Bunge kuwa na rekodi ya kipekee lakini pia, hatua yake ya kutaka Waziri Mkuu ang'olewe inampa nguvu zaidi CAG tofauti na wengi wanavyotafsiri.

  Zitto mwenyewe ameeleza: "Vyovyote itakavyokuwa, kufanikiwa au kutofanikiwa kumng'oa Waziri Mkuu, ripoti za CAG zitaheshimiwa kwa kufanyiwa kazi ili makosa ya ufisadi yasiwe yanajirudia na yakijirudia basi, siku nyingine Waziri Mkuu atang'oka, rekodi zimeshajiandika."
  Zitto alifanikiwa kukusanya saini za wabunge 73, ambao ni kutoka vyama karibu vyote vyenye wabunge bungeni, isipokuwa UDP tu.
   
 2. M

  Malolella JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 367
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Joh Cheyo hajitambui na hatambui nafac yake.
   
 3. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Unajua JK na Zitto ninmarafiki??? Nahsi aliyumwa na. Rais ili iwe mbinu ya kubadili baraza!!!!!!!
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Umekuja na thread ili utuchonganishe Kati ya CDM na zitto huwezi Pambaf!!!!!!! Ni makini ndio maana yupo CDM Chama makini kwi kwi! Kwi! Kwi! Kwi
   
 5. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2012
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  sawa! mpigie makofi mara tatu....
   
 6. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Zitto alitumwa na JK na JK anajua kabisa uongozi wake unayumbishwa na Magamba ya CCM sasa anayatumia majembe kama wakina Zitto kutema cheche ile yeye aweze kufanya kazi. Unajua tena ule uenyekiti wa CCM na kuwa chama ndo kinaunda serikali wanambana asiende wanavyotaka wao.

  Sasa amemwambia Lema azunguke Nchi nzima aiue CCM ili akija kutoka 2015 Chadema waingie ikulu halafu atawapa siri zote. na kuna kila dalili kuna agreement fulani na sisi wana Chadema kuja kumlinda.

  Namnukuu Zitto kule Bungeni wakati anahitimisha ''Mawaziri msimsingizie Raisi na kumchafua kwa uzembe wenu na ubaridhifu wenu wa kushindwa kusimamia mali na pesa za walipa kodi kwa manufaa yenu binafsi i lazima muwajibike na mchukuliwe hatua stahiki''
  Mwisho wa kunukuu. Hapa mpepata picha sasa kwamba JK amechoka na magamba sasa anawatumia chama makini kuiokoa nchi hii kutoka mikononi mwa wezi. JK na Zitto ni Dam Dam JK na Chadema ni Dama Dam.
   
 7. M

  Mkira JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2012
  Joined: May 10, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Anajua mwisho wake ni 2015 nintabiri UDP haitakuwa na mbunge kuanzia mwaka 2015 na vyama design yake SAU etc vitafutwa kutokana na kutokidhi matakwa, KATIBA MPYA INATAKIWA PIA IE NA KIPENGELE CHA KUFUTA VYAMA VISVYO NA WABUNGE ILI KUPUNGUZA UTITIRI WA VYAMA VINAKUWA KAMA MALIA YA MWENYEKITI KUALIWA NA RASI KUTEMEBELEA NCHI FULANI
   
 8. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,132
  Likes Received: 10,479
  Trophy Points: 280
  eh! eh...aisee
   
 9. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Tusubiri tuone,naona haya mahusiano ya mh.zitto na mh.dr.jk yanazungumziwa sana,yamkini dhamira ipo lakini vema kujipa muda ili kuona.mungu ataweka bayana maana hakuna siri ya wawili.
   
 10. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Mkuu ukusema Zitto ndiye makini kuliko wote TZ vipi Mnyika? Unajua mapendekezo yake madogo yamesaidia kulinusuru taifa kuingia katika deni kubwa? Tunataka kuanza mradi hatuna fesibility study, designs n.k vyote vile vimesababishwa na mh. Mnyika. Mi nadhani kila mbunge ana nafasi yake ndio maana wote wanfanya kazi vizuri labda useme zitto ameng'ara zaidi katika bunge hili.
   
 11. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  na ndiyo maana aliwaambia wakome kumsingizia au kumhusisha Rais katika wizi wao. I get the point. Na ninahisi Rais anapigia chapuo Rais kijana ajae kwa Maana ya Zitto ili aje amlinde na madudu yake. Sidhani kama atafanikiwa kwa hili. Watu wako macho sana siku hizi.
   
 12. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #12
  Apr 28, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  John Mnyika ni makini kuliko huyo gamba zitto, vp Lissu aliyeanzisha hoja ya kumng,oa waziri mkuu halafu Zitto akaidandia..acha kuleta mambo ya Bongofleva kwenye mustakabali wa nchi...
   
 13. b

  buyegiboseba JF-Expert Member

  #13
  Apr 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zito anajua sana kutumia nafasi finyu,Ni vema,tatizo ni pale anapohusishwa na magamba,binafsi CDM yeyote mwenye virusi vya magamba hatafanikiwa kuwa Rais wa nchi hii,Mungu lazima amkatilie mbali,Nchi hii tunaenda kwenye ukurasa mpya kabisa,ya kale yote lazima yapite yaje mapya
   
 14. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #14
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zitto hawez kuwa makin kuliko Mnyika na wengine, Zitto kwa habar zilizopo anataka kuoa kwa JK
   
 15. k

  kansiana Member

  #15
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Isaya 41:6 - Wakasaidiana, kila mtu na mwenzake, kila mtu akamwambia ndugu yake; Uwe na moyo mkuu. 7 Seremala akamtia moyo mfua dhahabu, na yeye alainishaye kwa nyundo akamhimiza yule apigaye fuawe, akiisifu kazi ya kuunga, akisema, Ni kazi njema; naye akaikaza kwa misumari isitikisike.

  Hivi ndivyo kiumbe kinachoitwa mwanadamu kinavyofanya kazi no one is complete exclusively!
   
 16. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #16
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,081
  Likes Received: 6,544
  Trophy Points: 280
  Hawezi kufungua mdomo bado anategemea kuendelea kulipiwa mkopo wake wa benk ya nyumba kutoka kodi zetu.
   
 17. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #17
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Cheyo kaonyesha kabisa nafasi ya ubunge wake ni kama fadhila toka kwa magamba!!!!!

  Hana analolijua zaidi ya ndiyo mzee na ndiyo maana chama chake hakina mbunge zaidi ya yeye na kaiua zaidi kwa kugoma kusign vote of no confidence.
   
 18. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #18
  Apr 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Cheyo kaonyesha kabisa nafasi ya ubunge wake ni kama fadhila toka kwa magamba!!!!!

  Hana analolijua zaidi ya ndiyo mzee na ndiyo maana chama chake hakina mbunge zaidi ya yeye na kaiua zaidi kwa kugoma kusign vote of no confidence.
   
 19. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #19
  Apr 28, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Mkuu raha ya mbio ni kumalizia sio kuanza,hivi mwanasiasa gani asiyetaka sifa ya kuiangusha serikali ya mpinzani wake mpaka aanzishe hoja aishie njiani mwenzake ndio aidake na kuipatia sifa?basi huyo sio mwanasiasa
   
 20. M

  Molemo JF-Expert Member

  #20
  Apr 28, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Muhuni yuleyule analeta thread zake za kihuni za uchonganishi.Stupid at work!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...