Zitto Kabwe kupeleka Bungeni hoja binafsi ya kutokuwa na Imani na Rais Magufuli

Nchi ya matukio na kila tukio ni kichekesho,wenye nchi wanapiga kazi wapinzani kulala ma kutwa kucha,..Majuzi tulikua na la Saanane sasa limekufa sijui kwsharudi mara Lema sasa kimyaaa kaachwa aendelee kula msoto sijui baada ya hili la njaa litafuata lipi
 
Duh,tungekuwa na watu wajasiri kama zito nchi hii ingenyoka lakini bahati mbaya tuna mazoba tu na wengi ni wapiga debe wenye njaa!.
 
Jambo moja ni muhimu sana, Rais anapaswa kujua kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Na Katiba imetoa wajibu wa lazima kwa Serikali kulinda watu. Ndio kazi ya Serikali – kulinda wananchi pale ambapo yanatokea majanga ambayo yanazidi kimo wananchi hao.

Tunamwambia Rais kwamba, Mtanzania yeyote akifa kwa njaa kwa sababu Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake Watanzania tutapaswa kuchukua hatua, Katiba inatulazimisha kumtoa Rais madarakani ikiwa yeye na Serikali yake watashindwa kutimiza wajibu wake wa kulinda uhai wa raia wake.

Tunamkumbusha Rais kuwa yeye sio mungu mtu. Yupo chini ya Katiba na kwa idadi ya wabunge wa upinzani waliopo Bungeni, na wakiamua kusimama na wananchi na kulinda Katiba, Rais wa sasa atakuwa Rais wa kwanza wa nchi yetu kutolewa hoja ya kutokuwa na imani naye bungeni. Katiba inahitaji asilimia 20 tu ya wabunge kuwasilisha hoja hiyo bungeni.

Ninatoa wito kwa Watanzania wote nchini, bila kujali vyama vyao, kuweka rekodi ya hali ya chakula popote walipo na kuweka takwimu ya maafa yeyote yanayotokana na njaa. Mtanzania yeyote akifa kwa njaa ni lazima tuchukue jukumu la kumwajibisha Rais kwa kusema waziwazi kwamba hajatimiza wajibu wake kama Mkuu wa Serikali kulinda wananchi wake.

Tunamkumbusha Rais kwamba kwa mujibu wa ibara ya 46A ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo yeye amekula kiapo kuilinda, kuihifadhi na kuitetea, Bunge laweza kumshataki yeye Rais kwa kosa la mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais.

Wananchi wanaona lugha za ubabe, vitisho, kuonea watu, kudhihaki waliopatwa na majanga kwamba ni mambo yanayodhalilisha kiti cha Rais.

Hivyo Rais achague maneno ya kusema mbele ya wananchi wake, atumie lugha ya kujenga matumaini badala ya kujenga hofu kwenye jamii, aache kuonea watu kwa kutumia madaraka yake, na akumbuke cheo ni dhamana.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo
Kijichi - Dar es salaam
Januari 15, 2017

Mhe. Kabwe kumbe unasubiri hadi mtanzania afe?
Kama usemavyo rais na serikali yake wana wajibu wa kuwalinda watu wao na Mali zao..
Je,mpaka sasa haya yanatekelezeka?
Je,huoni huko mtaani Mali za watanzania zinapotea? Uhai wa watanzania muhimu unapotea?

Mh. Kabwe vigezo vimetimia please tunaomba utuongoze kutoa hoja ya kutokuwa na imani nae tupo nyuma yako tutakusaport.
 
Awamu hii watu watapiga makelele kwa lugha zote. Mazoea mabaya. Rais tunyooshe Baba. Heshima irudi. Hawa wapuuzi wapotelee mbali. Magufuli ndo Rais aliyesubiriwa miaka mingi tangu 1984.
 
Zito kama wewe sio mchochezi nakuwadi wa siasa za maji taka je wewe ni nani? Unapoteza muda kumchafuwa mtu ambaye hachafuliki nakuapia peleka hata leo huwo mswaada ila tambuwa mwisho utaaibika sana.
Wasiwasi wa nini kama unajua ataahibika..
 
Zitto,akili zake ni hewa, 2/3 ya wabunge kukubali anaitoa wapi akawambie malofa
 
Pumba tupu kwa kura ngapi? Firimbi tu hizo za majukwaani,fb,jf na mengine. Hamna kitu porojo tu hizo. Sawa na kutia bahari sukari iwe tamu
 
Jambo moja ni muhimu sana, Rais anapaswa kujua kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Na Katiba imetoa wajibu wa lazima kwa Serikali kulinda watu. Ndio kazi ya Serikali – kulinda wananchi pale ambapo yanatokea majanga ambayo yanazidi kimo wananchi hao.

Tunamwambia Rais kwamba, Mtanzania yeyote akifa kwa njaa kwa sababu Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake Watanzania tutapaswa kuchukua hatua, Katiba inatulazimisha kumtoa Rais madarakani ikiwa yeye na Serikali yake watashindwa kutimiza wajibu wake wa kulinda uhai wa raia wake.

Tunamkumbusha Rais kuwa yeye sio mungu mtu. Yupo chini ya Katiba na kwa idadi ya wabunge wa upinzani waliopo Bungeni, na wakiamua kusimama na wananchi na kulinda Katiba, Rais wa sasa atakuwa Rais wa kwanza wa nchi yetu kutolewa hoja ya kutokuwa na imani naye bungeni. Katiba inahitaji asilimia 20 tu ya wabunge kuwasilisha hoja hiyo bungeni.

Ninatoa wito kwa Watanzania wote nchini, bila kujali vyama vyao, kuweka rekodi ya hali ya chakula popote walipo na kuweka takwimu ya maafa yeyote yanayotokana na njaa. Mtanzania yeyote akifa kwa njaa ni lazima tuchukue jukumu la kumwajibisha Rais kwa kusema waziwazi kwamba hajatimiza wajibu wake kama Mkuu wa Serikali kulinda wananchi wake.

Tunamkumbusha Rais kwamba kwa mujibu wa ibara ya 46A ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo yeye amekula kiapo kuilinda, kuihifadhi na kuitetea, Bunge laweza kumshataki yeye Rais kwa kosa la mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais.

Wananchi wanaona lugha za ubabe, vitisho, kuonea watu, kudhihaki waliopatwa na majanga kwamba ni mambo yanayodhalilisha kiti cha Rais.

Hivyo Rais achague maneno ya kusema mbele ya wananchi wake, atumie lugha ya kujenga matumaini badala ya kujenga hofu kwenye jamii, aache kuonea watu kwa kutumia madaraka yake, na akumbuke cheo ni dhamana.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo
Kijichi - Dar es salaam
Januari 15, 2017
Nadhani unahitaji kupimwa akili, umekosa jambo la kusimamia kama mwanasiasa umebaki na suala la njaa kila kukicha jambo ambalo liko ndani ya uwezo serikali, nilikuwa muumini sana wa hoja zako lkn kwa sasa tangu uwe kiongozi wa chama naona siyo zitto ninaemfaham aliyekuwa anasema nchi ina rais dhaifu. Peleka hoja lkn Magufuli hawezi kuondoka kwa hoja yako ya kitoto
 
Unaita,tangu chadema wafukuze msalit huyu ,rahana hii bado iko kichwani,
Hii lugha sijui ni abanzakinembe wa mpakani---unaita----rahana. kumbe mmeshavuka mpaka huku kumsaidia!! Jakaya leta operesheni upepo tuwapeperushe hawa
 
Zitto Kabwe ni rahisi sana kununuliwa, upo uwezekano ameshapewa chake na wapiga dili ili kuichafua serikali yetu tukufu ili ionekane haifai mbele ya jamii. Zamani watu kama hawa walikuwa hawana nafasi katika jamii hivyo hatua za haraka zilikuwa zinachukuliwa kukabiliana naye.
 
katika kitabu cha THE RIVER BETWEEN kilicho andikwa na ngugi"" ukisoma ndio utajua nchi yetu ilivyokaa muundo wake sioni haja watu kumgombez mh.zitto
 
Jambo moja ni muhimu sana, Rais anapaswa kujua kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Na Katiba imetoa wajibu wa lazima kwa Serikali kulinda watu. Ndio kazi ya Serikali – kulinda wananchi pale ambapo yanatokea majanga ambayo yanazidi kimo wananchi hao.

Tunamwambia Rais kwamba, Mtanzania yeyote akifa kwa njaa kwa sababu Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake Watanzania tutapaswa kuchukua hatua, Katiba inatulazimisha kumtoa Rais madarakani ikiwa yeye na Serikali yake watashindwa kutimiza wajibu wake wa kulinda uhai wa raia wake.

Tunamkumbusha Rais kuwa yeye sio mungu mtu. Yupo chini ya Katiba na kwa idadi ya wabunge wa upinzani waliopo Bungeni, na wakiamua kusimama na wananchi na kulinda Katiba, Rais wa sasa atakuwa Rais wa kwanza wa nchi yetu kutolewa hoja ya kutokuwa na imani naye bungeni. Katiba inahitaji asilimia 20 tu ya wabunge kuwasilisha hoja hiyo bungeni.

Ninatoa wito kwa Watanzania wote nchini, bila kujali vyama vyao, kuweka rekodi ya hali ya chakula popote walipo na kuweka takwimu ya maafa yeyote yanayotokana na njaa. Mtanzania yeyote akifa kwa njaa ni lazima tuchukue jukumu la kumwajibisha Rais kwa kusema waziwazi kwamba hajatimiza wajibu wake kama Mkuu wa Serikali kulinda wananchi wake.

Tunamkumbusha Rais kwamba kwa mujibu wa ibara ya 46A ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo yeye amekula kiapo kuilinda, kuihifadhi na kuitetea, Bunge laweza kumshataki yeye Rais kwa kosa la mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais.

Wananchi wanaona lugha za ubabe, vitisho, kuonea watu, kudhihaki waliopatwa na majanga kwamba ni mambo yanayodhalilisha kiti cha Rais.

Hivyo Rais achague maneno ya kusema mbele ya wananchi wake, atumie lugha ya kujenga matumaini badala ya kujenga hofu kwenye jamii, aache kuonea watu kwa kutumia madaraka yake, na akumbuke cheo ni dhamana.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo
Kijichi - Dar es salaam
Januari 15, 2017

sijui kama huyu mbabe atajirekebisha
 
Back
Top Bottom