Zitto Kabwe: Kila Novemba kunakuwa na mgao wa Umeme ila tulikuwa hatutangaziwi kwa sababu za kibabe tu

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,957
141,948
Kiongozi mkuu wa ACT wazalendo Zitto Kabwe amesema ni hali ya kawaida mwezi November kuwa na mgao wa umeme ila tu awamu iliyopita tulikuwa hatutangaziwi lakini mgao ulikuwepo.

Zitto anasema isingekuwa rahisi kutangaza kuwa kuna mgao wa umeme awamu iliyopita kwa sababu ya kuogopa ubabe.

Ameandika Zitto Kabwe.
 
Huyu jamaa badala ya kushauri mipango mkakati hali kama hii isijirudie.

Yy anaongea kwa maana ya kutetea!?
Eti huyo ndiye Kiongozi mkuu wa chama cha upinzani hapa Tanganyika. Badala ya kuichallenge serikali kwa hoja zenye mashiko kanajipendekeza kwa serikali ya Hangaya. TZ hatuna upinzani bali wachumia tumbo tu. CCM na iendelee tu mpaka tutakapopata wapinzani wa kweli.
 
Kiongozi mkuu wa ACT wazalendo Zitto Kabwe amesema ni hali ya kawaida mwezi November kuwa na mgao wa umeme ila tu awamu iliyopita tulikuwa hatutangaziwi lakini mgao ulikuwepo.

Zitto anasema isingekuwa rahisi kutangaza kuwa kuna mgao wa umeme awamu iliyopita kwa sababu ya kuogopa ubabe.

Ameandika Zitto Kabwe.
Mataahira wataisha lini nchi hii? Kwahiyo kipindi hicho sisi tulikuwa wapi hadi tusiuone huo mgao?!
 
Hahaha huhuhu semeni tu tunataka majenereta yawe na soko
Pic%20Layer_20211113111557588.jpg
 
Zitto ni mtwana wa Makamba and Co, sioni kipya hapo

Tumwamini nani hapa?

Zitto: kila mwezi November hua kuna mgao wa umeme

Makamba: kuna maintanance ya vifaa

Mh raisi: kina cha maji kimepungua

Ukiangalia kauli ya Zitto inapita kule anakopita slave master wake!

Huyu jamaa ndio maana wenzake hawamwamini.
 
Umeme ukatike watu wasijue?
Si ndio hapo ndugu yangu ninapo shangaa hivi hawa jamaa wanatuona sisi wajinga kiasi gani yaani mgao wa umeme uwe kama hivi ilivyo sasa bado inahitaji mtu utangaziwe ndo ili ujue kuna mgao wa umeme na maji kweli!!?
Yaani kitu kinachoonekana wazi mitaani humu eti tusiyaone kisa hayatangazwi aisee hawa wanasiasa watuheshimu japo kidogo basi watanzania sio wajinga kiasi hiki.
 
Kiongozi mkuu wa ACT wazalendo Zitto Kabwe amesema ni hali ya kawaida mwezi November kuwa na mgao wa umeme ila tu awamu iliyopita tulikuwa hatutangaziwi lakini mgao ulikuwepo.

Zitto anasema isingekuwa rahisi kutangaza kuwa kuna mgao wa umeme awamu iliyopita kwa sababu ya kuogopa ubabe.

Ameandika Zitto Kabwe.
Mbona huyu huwa pro goverment sana?

Ina maana sisi raia wote ni watoto tulozaliwa mwaka jana tusijue mwenendo wa nishati ya umeme nchini kwa miaka iliyopita?

Na ngoja,baada ya kifo cha Maalim Sefu, sidhani kama kuna mtu bado anahangaika na ufuasi wa chama chenye viongozi wenye hulka za kimamluki namna hii!

Anavyoungana na wizara ya nishati kuleta utetezi wa kijingajinga, sisi raia tusemeje sasa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom