Zipi sababu za mgawo wa umeme usioisha Tanzania

Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
15,010
16,615
Wanajukwaa,habari za wakati huu baada ya harakati za kutwa nzima ama za utumishi wa jamii, kujitafutia mlo wa siku ama kuzitafutia familia mahitaji ya kila siku. Ni matumaini yangu kuwa wengi wetu tuu buheri wa afya. Pia nitoe pole kwa wote wenye changamoto mbalimbali, iwe ni za kiafya, kijamii, kiuchumi na zinginezo nawaombea kwa Mungu mpate wepesi katika changamoto mnazopitia.

Baada ya kuwatakieni Kheri, ninalo jambo linanipa maswali mengi na kuninyima majibu. Wanajukwaa mtakubali kuwa mimi sii mwandishi wa hoja humu,ila kwa hili imenilazimu.

1. Bila shaka wengi wetu tumekuwa tukishuhudia kwa vipindi tofauti vya mwaka huu tatizo la umeme.

2. Tumekuwa tukielezwa sababu za upungufu kuwa ni sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa ikiwa ni pamoja na ukame wa muda mrefu na kupewa matarajio,ikiwa ni kupatikana nafuu,pindi mvua ikinyesha,pamoja na kuongeza uzalishaji umeme kwa kutumia gesi.

3. Wengi tunashuhudia kiwango kizuri cha mvua,kwa kipindi cha karibuni mwezi mmoja sasa kiasi cha kuleta maafa kwa baadhi ya maeneo.

4. Wengi tumeshuhudia kuongezeka sana kwa mgao wa umeme hata baada ya matarajio ya kupata mvua hadi kuipata mvua.

5. Uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi tunayozalisha wenyewe bila shaka unaendelea,na mitambo tunayo ile ya ubungo,na kinyerezi 1 hadi 3 kama sijakosea na pengine sijasikia iwapo kama uzalishaji umesimama kwa tatizo lolote.

6. Ni maoni yangu kuwa ni vyema tuache yale mambo ya sirikali,kama yapo matatizo yanayopelekea kujikuta katika hali ya sasa,yawekwe wazi ili kujua namna ya kutatua tatizo,kwani wahenga wanasema mficha maradhi kifo kitamuumbua.

7. Wito wangu kwa wazalendo wa kweli,mwenye kujua changamoto ilipo,tulonge/tubutue tulikomboe taifa letu.

8. Vinginevyo niseme hii ni karata tarajiwa ya wanasiasa kuelekea uchaguzi ujao,kama sivyo popote walipo wafanye kama wanajikuna tuondoke kwenye hili linalodidimiza taifa letu,uchumi wa watu wake na kulemaza kazi za uzalishaji Mali na ujenzi wa taifa kwa ujumla.

9. Ukweli utatuweka huru,ukweli utachangia maendeleo ya taifa letu.Tanzania ni yetu sote tusikubali kuona inateketea.
 
Kama ni kwa wiki hii labda hili la kuunganisha gridi ya taifa na bwawa la Mwalimu Nyerere inaweza ikawa sababu
globaltvonline_1701488502398.jpeg


Ila ki ukweli tatizo la kukatika umeme linakera
 
Labda
Maji yamezidi umeme unazalishwa mwingi. Wanakata ili kupunguza wingi wa umeme.
Hapo kama tamekuwa mengi ni kiasi cha kuyaruhusu yarudi mtoni na kuendelea na safari yake,labda uniambie mabwawa yamejaa tope na hivyo maji kuwa sii ya kutosha,na iwapo ni hivyo mbona ukatabati haufanyiki?
 
Leo imebidi watu warudie nguo za jana hakuna umeme, huku kwenye mafrig vyakula vinaoza balaa
unasema hivyo hata kwangu imebidi nguo moja niivae hivyo hivyo, just imagine saa 12 asubuhi wanakata halafu saa 5 usiku ndio wanarudisha
 
Back
Top Bottom