Zitto Kabwe, Hayo ndio maazimio ya Bunge ambayo Werema anakwepa kueleza utekelezaji wake

Inafurahisha sana kuona magwanda wapo bega kwa bega na Werema kwenye huu mjadala.
 
kuna na huyu
attachment.php

we binti mbona nidhamu yako ndogo hivyo
 
!
!
aache longolongo, atutajie hayo majina kabla hatujaamua kumuomba aweke na picha mahali hapa.
akiyataja within two days tutamsaidia kuweka picha za wenye majina
 
Hao hawatakuwa watoto wa vigogo; amesema watoto wa viongozi serikalini na wake zao na wao wenyewe....

si lazima wawe wa vigogo...nje ni nje ya nchi hata kongo, rwanda, kenya, uganda, somalia ni nje ya nchi
 
KWA HIYO BASI naliomba Bunge lako Tukufu liazimie:-

(i) Kwamba Bunge lako Tukufu liunde Kamati Teule kuchunguza raia wa Tanzania wenye kumiliki fedha za kigeni na mali nje ya Tanzania. Kamati Teule hiyo ifanye kazi zifuatazo:-
(a)Kuchunguza mfumo mzima wa utoroshaji wa fedha na kufichwa nje ya nchi;
(b)Kuchunguza na kupambanua mali na fedha haramu dhidi ya halali zinazomilikiwa na raia wa Tanzania katika taasisi za fedha nje Tanzania;
(c)Kuchunguza utaratibu mzima wa kugawa vitalu vya utafutaji mafuta na gesi kati ya mwaka 2003 – 2008;
(d)Kuchunguza mtiririko mzima wa utoroshaji wa fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania kupitia kampuni ya Meremeta na pia kampuni tanzu ya Triannex pty ya Afrika Kusini naDeep Green Finance Limited na kupendekeza hatua za kuchukua dhidi ya wahusika wote wautoroshaji wa fedha kwenda nje;
(e)Kuchunguza umiliki wa Watanzania kwenye kampuni zote zenye mikataba ya utafutaji wa mafuta na gesi hapa nchini na namna umiliki huo umekuwa ukibadilika yaani proceedszilizotokana na mabadiliko hayo ya umiliki na kama kodi stahili zimekuwa zikilipwakutokana na mabadiliko ya umiliki huo; na
(f)Kuchunguza kwa kina mali za Watanzania wote waliowahi kushika nafasi za UwaziriMkuu kati ya mwaka 2003 mpaka 2010, waliowahi kushika nafasi za Uwaziri wa Nishati na Madini, Uwaziri wa Ulinzi, Ukuu wa Majeshi, Ukatibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Ukatibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi, Uanesheria Mkuu wa Serikali, Ukamishna wa Nishati, Ukurugenzi Mkuu waTPDC, Uenyekiti na Ujumbe wa Bodi waTPDC katika ya mwaka 2003 mpaka 2010.

(ii)Kwamba, Serikali ilete Muswada wa Sheria Bungeni ifikapo Mkutano wa 11 wa Bunge kwamba itakuwa ni marufuku kwa Kiongozi yeyote wa Umma au mume au mke wake au
watoto wake kuwa na akaunti katika mabenki nje ya nchi isipokuwa kwa sababu maalumu na kwa kibali rasmi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

(iii)Kwamba, Serikali iwasiliane na Benki ya Dunia ili kupitia Kitengo cha Assets Recovery Unit ili mabilioni ya Fedha na mali zisizoondosheka zinazomilikiwa na Watanzania katika mabenki ya nchini Switzerland, Dubai, Mauritius na visiwa na maeneo mengine yote ambapo hufichwa fedha na mali ili kukwepa kodi na kwamba mali hizo na mabilioni hayo yaliyopatikana kiharamu yarudishwe nchini mara moja.

(iv)Kwamba, katika Muswada tajwa hapo juu, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aimarishiwe mamlaka ya kutoa kibali kwa Mtanzania yeyote anayetaka kufungua akaunti ya Benki nje ya nchi na kwamba kila mwaka Gavana atatangaza kwenye Gazeti la Serikali na magazeti yanayosomwa na wananchi wengi orodha ya Watanzania walioomba na walioruhusiwa kuwa na akaunti ya benki nje ya Tanzania;

(v)Kwamba, Watanzania wote wenye akaunti za fedha nje waeleze wamezipataje na TAKUKURU wachukue hatua za kisheria dhidi ya watu wote wenye kumiliki fedha na mali kinyume na mapato yao halali;

(vi)Kwamba, Serikali, katika Mkutano wa Bunge wa Kumi na Moja (11) na baada ya Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu raia wa Tanzania wenye kumiliki fedha za kigenikwenye mabenki na mali nje ya Tanzania ilete taarifa ya hatua ilizochukua ili kuziba mianya ya utoroshaji wa fedha nje ya Tanzania.

(vii)Kwamba, Serikali katika Bajeti ya mwaka 2013/2014 itaanzisha kodi maalum ‘financial transaction tax’ ya angalau asilimia 0.5 ya thamani ya ‘transaction’ ili kuweza kuwa narekodi zauhakika za fedha ndani na zinazotoka nje ya nchi.

Swali, ni kipi kimefanyika hadi sasa zaidi ya jitihada za kuligeuza suala hili kuwa naming and shaming politics?

My take huu ni mwanzo wa ZZK kujibu mapigo kwa werema na baada ya muda tutamjua nani ni mnafiki kwa watanzania kuhusu fedha haramu zilizofichwa Uswis

SOURCE kwenye fb and twitter wall yake ZZK

Haya maamuzi ya Bunge ni mazuri sana tungepata kamati yenye watu makini basi watanzania tungefahamu siri ya mchezo mzima wa utoroshaji wa fedha nje. Wasiwasi wangu uko kwenye kamati akina AG hawataweza kuja ni kitu kipya. Let's wait and see!
 
HARAMU haiwezi kuzaa HALALI,Hata mwana HIP HOP fid Q ktk moja ya nyimbo zake unaoitwa "PROPAGANDA" kuna mstari amesema nanukuu "HUPASWI KUMUAMINI MUONGO HATA KAMA AMEONGEA UKWELI".Huyu MM hana mpya.
 
lolote atakalofanya kwasasa hata liwe zuri kwangu nitaliona ni baya. msaliti hana price tag.
 
Zzk ni msomi wala hafanyi mamno kwa kukurupuka, anaelewa anachokifanya tatizo akili zenu ndogo kama Lema ndiomaana hazifikii kile anachokifanya ZZK.

Mwambie Lema ataje majina ya walio lipua bomu c ajidai dvd anayo. Sasa anataka tume ya nini!View attachment 127276
Tatizo la wananchi wengi ni kuamini kuwa wasomi ndio mwisho wa matatizo ya nchi yetu! Hiyo ni aibu, siasa hazihitaji wasomi ila tunahitaji wasomi kwenye elimu, tiba, kilimo, huduma, nk. Kama akielekeza usomi wake huko itakuwa sawa, lakini pale kwenye lile genge la wahuni ambao hupitisha maamuzi kwa ushabiki huwa haisaidii kitu.
 
Zitto acha usanii bana. Mbona unajifanya msahaulifu nmna hii? Juzi juzi tu ulikua ukipiga kelele kua unafuatilia mabilioni ya uswis?na post zako fb ambazo umekua ukituaminisha watanzania kua unafuatilia mabilion,hata kufikia hatua ya kutuhumu wanachama wenzako kua wanakuandama na unavunjwa nguvu katika ufuatiliaji kwenye mkutano wako kaliua. Leo hii ndio unajua kua kuna maazimio ya Bunge? Sasa zile mbwembwe zote zilikia za nini
 
makamanda, twendeni kwenye uzi wa mwanakjj tukajionee namna alivyomnanga mwenyekt wetu kasha tutafakari hata tusipochangia.........
 
lolote atakalofanya kwasasa hata liwe zuri kwangu nitaliona ni baya. msaliti hana price tag.

acha kukariri kamanda,msome mwanakjj 'umuone' zito, slaa na mbowe ktk uzi wake unaoelezea gogoro la chama............
 
Back
Top Bottom