Zitto Kabwe, Hayo ndio maazimio ya Bunge ambayo Werema anakwepa kueleza utekelezaji wake

mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,850
2,000
KWA HIYO BASI naliomba Bunge lako Tukufu liazimie:-

(i) Kwamba Bunge lako Tukufu liunde Kamati Teule kuchunguza raia wa Tanzania wenye kumiliki fedha za kigeni na mali nje ya Tanzania. Kamati Teule hiyo ifanye kazi zifuatazo:-
(a)Kuchunguza mfumo mzima wa utoroshaji wa fedha na kufichwa nje ya nchi;
(b)Kuchunguza na kupambanua mali na fedha haramu dhidi ya halali zinazomilikiwa na raia wa Tanzania katika taasisi za fedha nje Tanzania;
(c)Kuchunguza utaratibu mzima wa kugawa vitalu vya utafutaji mafuta na gesi kati ya mwaka 2003 – 2008;
(d)Kuchunguza mtiririko mzima wa utoroshaji wa fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania kupitia kampuni ya Meremeta na pia kampuni tanzu ya Triannex pty ya Afrika Kusini naDeep Green Finance Limited na kupendekeza hatua za kuchukua dhidi ya wahusika wote wautoroshaji wa fedha kwenda nje;
(e)Kuchunguza umiliki wa Watanzania kwenye kampuni zote zenye mikataba ya utafutaji wa mafuta na gesi hapa nchini na namna umiliki huo umekuwa ukibadilika yaani proceedszilizotokana na mabadiliko hayo ya umiliki na kama kodi stahili zimekuwa zikilipwakutokana na mabadiliko ya umiliki huo; na
(f)Kuchunguza kwa kina mali za Watanzania wote waliowahi kushika nafasi za UwaziriMkuu kati ya mwaka 2003 mpaka 2010, waliowahi kushika nafasi za Uwaziri wa Nishati na Madini, Uwaziri wa Ulinzi, Ukuu wa Majeshi, Ukatibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Ukatibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi, Uanesheria Mkuu wa Serikali, Ukamishna wa Nishati, Ukurugenzi Mkuu waTPDC, Uenyekiti na Ujumbe wa Bodi waTPDC katika ya mwaka 2003 mpaka 2010.

(ii)Kwamba, Serikali ilete Muswada wa Sheria Bungeni ifikapo Mkutano wa 11 wa Bunge kwamba itakuwa ni marufuku kwa Kiongozi yeyote wa Umma au mume au mke wake au
watoto wake kuwa na akaunti katika mabenki nje ya nchi isipokuwa kwa sababu maalumu na kwa kibali rasmi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;

(iii)Kwamba, Serikali iwasiliane na Benki ya Dunia ili kupitia Kitengo cha Assets Recovery Unit ili mabilioni ya Fedha na mali zisizoondosheka zinazomilikiwa na Watanzania katika mabenki ya nchini Switzerland, Dubai, Mauritius na visiwa na maeneo mengine yote ambapo hufichwa fedha na mali ili kukwepa kodi na kwamba mali hizo na mabilioni hayo yaliyopatikana kiharamu yarudishwe nchini mara moja.

(iv)Kwamba, katika Muswada tajwa hapo juu, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania aimarishiwe mamlaka ya kutoa kibali kwa Mtanzania yeyote anayetaka kufungua akaunti ya Benki nje ya nchi na kwamba kila mwaka Gavana atatangaza kwenye Gazeti la Serikali na magazeti yanayosomwa na wananchi wengi orodha ya Watanzania walioomba na walioruhusiwa kuwa na akaunti ya benki nje ya Tanzania;

(v)Kwamba, Watanzania wote wenye akaunti za fedha nje waeleze wamezipataje na TAKUKURU wachukue hatua za kisheria dhidi ya watu wote wenye kumiliki fedha na mali kinyume na mapato yao halali;

(vi)Kwamba, Serikali, katika Mkutano wa Bunge wa Kumi na Moja (11) na baada ya Taarifa ya Kamati Teule ya Bunge kuhusu raia wa Tanzania wenye kumiliki fedha za kigenikwenye mabenki na mali nje ya Tanzania ilete taarifa ya hatua ilizochukua ili kuziba mianya ya utoroshaji wa fedha nje ya Tanzania.

(vii)Kwamba, Serikali katika Bajeti ya mwaka 2013/2014 itaanzisha kodi maalum ‘financial transaction tax' ya angalau asilimia 0.5 ya thamani ya ‘transaction' ili kuweza kuwa narekodi zauhakika za fedha ndani na zinazotoka nje ya nchi.

Swali, ni kipi kimefanyika hadi sasa zaidi ya jitihada za kuligeuza suala hili kuwa naming and shaming politics?

My take huu ni mwanzo wa ZZK kujibu mapigo kwa werema na baada ya muda tutamjua nani ni mnafiki kwa watanzania kuhusu fedha haramu zilizofichwa Uswis

SOURCE kwenye fb and twitter wall yake ZZK
 

Deo Corleone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
15,718
2,000
Akitaja hayo majina mtayafanyia nini?? Hapa yatekelezwe hayo maazimio tuone kama kuna mwizi ataenda ficha hela nje.
 

AlP0L0

JF-Expert Member
Apr 23, 2011
5,073
2,000
MM ni mnafiki tu, kama si mnafiki ataje majina...

Zzk ni msomi wala hafanyi mamno kwa kukurupuka, anaelewa anachokifanya tatizo akili zenu ndogo kama Lema ndiomaana hazifikii kile anachokifanya ZZK.

Mwambie Lema ataje majina ya walio lipua bomu c ajidai dvd anayo. Sasa anataka tume ya nini! 1387267265067.jpg
 

Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,995
1,500
(v)Kwamba, Watanzania wote wenye akaunti za fedha nje waeleze wamezipataje na TAKUKURU wachukue hatua za kisheria dhidi ya watu wote wenye kumiliki fedha na mali kinyume na mapato yao halali;
Another funny eti takukuru wachukue hatua.....which takukuru?

Hizi ni sarakasi za kutafuta pa kutokea ajiulize alipojikwaa ajisahihishe ili tuanze kumwamini tena but it will take time.
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
Anazidi kunikera huyu zittomafesbuku, huku jf ni member mbona haji kujadili pamoja nasi, anadhani yeye ni wa level tofauti sio?
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,523
2,000
Ni hoja yenye mashiko kwa taifa,ila zitto aache utoto wa kuwaambia watanzania kuwa ana majina, wakati hana!
 

sifongo

JF-Expert Member
Jun 5, 2011
4,837
2,000
Mheshimiwa Zitto hembu tafuta kivuli chini ya mti usimame kwa dakika chache na kujifatakari wapi unaelekea, naona kama umepoteza mwelekeo hivi....ukishapata jibu basi uamue ama kuendelea na safari au urudi ulipotoka, waliokuambia kwamba huko uendako ni kwema na kuna neema wamekudanganya.
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,614
2,000
Akitaja hayo majina mtayafanyia nini?? Hapa yatekelezwe hayo maazimio tuone kama kuna mwizi ataenda ficha hela nje.

wakiingia kwenye kuminanane zetu kama mabina tutawashushia kipigo heavy mpaka tunawa restisha jehanam kwa bosi wao shetan.
 

sikajiji

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
586
195
mwekundu Tunahitaji wbunge wenye kuweka misingi ya kisheri itakayotulinda wavuja jasho kama ZZK.Tunahitaji nguvu ya kisheria zenye siyo kuropoka kama wavuta bangi halafu ikaaishia hapo. Na wengi wa wabunge wamekuwa ni wachumia tumbo. Heri kufa kwa kusimamia haki na maslahi ya wengi.
 
Last edited by a moderator:

Utingo

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
7,421
2,000
KWA HIYO BASI naliomba Bunge lako Tukufu liazimie:-


(ii)Kwamba, Serikali ilete Muswada wa Sheria Bungeni ifikapo Mkutano wa 11 wa Bunge kwamba itakuwa ni marufuku kwa Kiongozi yeyote wa Umma au mume au mke wake au
watoto wake kuwa na akaunti katika mabenki nje ya nchi isipokuwa kwa sababu maalumu na kwa kibali rasmi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;SOURCE kwenye fb and twitter wall yake ZZK

Hata wanafunzi wanaokwenda kusoma nje, wakibeba maboksi usiku au kusafisha glass bar usiku, wakitaka kuwa na akaunti ili kujiwekea akiba benki za huko, lazima rais aidhinishe?
 

Ben Mugashe

Verified Member
Oct 9, 2008
998
1,000
Kumbe wenye MAPESA na vijisenti Uswisi ni hawa basi tunawajua maana si hawa Watanzania wote waliowahi kushika nafasi za
UwaziriMkuu kati ya mwaka 2003 mpaka 2010 ni......
waliowahi kushika nafasi za Uwaziri wa Nishati na Madini ni.....
Uwaziri wa Ulinzi.......
Ukuu wa Majeshi.......,
Ukatibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini.......
Ukatibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi,......
Uanesheria Mkuu wa Serikali..........
, Ukamishna wa Nishati,......
Ukurugenzi Mkuu waTPDC,....
Uenyekiti na Ujumbe wa Bodi waTPDC katika ya mwaka 2003 mpaka 2010.

JAZA NAFASI Zilizoachwa wazi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom