Zitto Kabwe, Hayo ndio maazimio ya Bunge ambayo Werema anakwepa kueleza utekelezaji wake

Kifupi keshawataja kwa majina yao kilichobakia ni serikali kujiridhisha na kuwachukulia hatua.
 
kama imeshindikana kuunda tume kuchunguguza watu walivyouwawa na bomu watawezaje kuunda tume kuchunguza fedha, fedha na mauaji kipi kinaogopesha zaidi?, serikali ya ccm ni sikio la kufa
 
Wachaga utawajua tu,zito msomi na anajua anachokisema,namshangaa sana lema(chakula cha watu)kujifanya mzalendo wa chadema wakati mnafiki tu anatafuta umaarufu kila chama kapita na kaparaganya na kukiacha na leo atasema nini ili tumuone mkweli??zito upo juu sema tu wala usiogope hao kina lema(chakula cha watu)mwache awataje waliolipuwa bomu.
 
mwekundu Kuunda kamatii wakati Zitto amejitapa ana majina ni kutumia vibaya raslimali za watanzania.

Kama majina anayo ataje, kamati ni kupoteza hoja ya msingi na kutufinyanga kifiira watanzania!
 
Last edited by a moderator:
SOURCE kwenye fb and twitter wall yake ZZK

Mzee wa Twira na ma-facebook tumekusoma.
Ila sisi tunajua ULIAPA mbele ya mwanasheria mkuu kwamba hujui chochote kuhusu Madola ya uswisi - na debate imeshafungwa sababu wewe ni MUONGO!!

Hizi point ulizokuja nazo leo ulitakiwa uzimwage Bungeni kama utetezi wakati suala lako linajadiliwa sasa humo kwenye Facebook unataka wananchi wakuone huruma kwamba hukudanganya na LIST ya watuhumiwa bado unayo!!
 
mwekundu maneno mengi ya nini Zito taja majina, vinginevyo unathibitisha unafiki wako.
 
Last edited by a moderator:
Ataje nini acheni chuki nani asiejua km chenge ana vijisenti visiwa vya jessy hata hilo hamulioni? Acheni chuki na zitto dogo anatisha km kweli bunge linania ya mabadiliko wafuate huo ushauri wake chezea zitto
 
KWA HIYO BASI naliomba
Bunge lako Tukufu liazimie:- ...

(vii)Kwamba, Serikali katika Bajeti ya mwaka 2013/2014 itaanzisha kodi
maalum ‘financial transaction tax' ya angalau asilimia 0.5 ya thamani ya ‘transaction' ili kuweza kuwa narekodi zauhakika za fedha ndani na
zinazotoka nje ya nchi.

Swali, ni kipi kimefanyika hadi sasa zaidi ya jitihada za kuligeuza suala hili kuwa naming and shaming politics?

Nionavyo mimi hili azimio la saba ni kama limeshafanyiwa kazi. Sasa kuna kodi ya asilimia 0.15 ya thamani ya fedha inayokwenda nje ya nchi
 
Hata wanafunzi wanaokwenda kusoma nje, wakibeba maboksi usiku au kusafisha glass bar usiku, wakitaka kuwa na akaunti ili kujiwekea akiba benki za huko, lazima rais aidhinishe?

Hao hawatakuwa watoto wa vigogo; amesema watoto wa viongozi serikalini na wake zao na wao wenyewe....
 
Maneno meeengi ya nini,sisi tunataka majina ya hao watu,hizo story hata huko ccm wanaziimbaga kitambo tu'
 
kwa hiyo basi naliomba bunge lako tukufu liazimie:-

(i) kwamba bunge lako tukufu liunde kamati teule kuchunguza raia wa tanzania wenye kumiliki fedha za kigeni na mali nje ya tanzania. Kamati teule hiyo ifanye kazi zifuatazo:-
(a)kuchunguza mfumo mzima wa utoroshaji wa fedha na kufichwa nje ya nchi;
(b)kuchunguza na kupambanua mali na fedha haramu dhidi ya halali zinazomilikiwa na raia wa tanzania katika taasisi za fedha nje tanzania;
(c)kuchunguza utaratibu mzima wa kugawa vitalu vya utafutaji mafuta na gesi kati ya mwaka 2003 – 2008;
(d)kuchunguza mtiririko mzima wa utoroshaji wa fedha kutoka benki kuu ya tanzania kupitia kampuni ya meremeta na pia kampuni tanzu ya triannex pty ya afrika kusini nadeep green finance limited na kupendekeza hatua za kuchukua dhidi ya wahusika wote wautoroshaji wa fedha kwenda nje;
(e)kuchunguza umiliki wa watanzania kwenye kampuni zote zenye mikataba ya utafutaji wa mafuta na gesi hapa nchini na namna umiliki huo umekuwa ukibadilika yaani proceedszilizotokana na mabadiliko hayo ya umiliki na kama kodi stahili zimekuwa zikilipwakutokana na mabadiliko ya umiliki huo; na
(f)kuchunguza kwa kina mali za watanzania wote waliowahi kushika nafasi za uwazirimkuu kati ya mwaka 2003 mpaka 2010, waliowahi kushika nafasi za uwaziri wa nishati na madini, uwaziri wa ulinzi, ukuu wa majeshi, ukatibu mkuu wa wizara ya nishati na madini, ukatibu mkuu wa wizara ya ulinzi, uanesheria mkuu wa serikali, ukamishna wa nishati, ukurugenzi mkuu watpdc, uenyekiti na ujumbe wa bodi watpdc katika ya mwaka 2003 mpaka 2010.

(ii)kwamba, serikali ilete muswada wa sheria bungeni ifikapo mkutano wa 11 wa bunge kwamba itakuwa ni marufuku kwa kiongozi yeyote wa umma au mume au mke wake au
watoto wake kuwa na akaunti katika mabenki nje ya nchi isipokuwa kwa sababu maalumu na kwa kibali rasmi kutoka kwa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania;

(iii)kwamba, serikali iwasiliane na benki ya dunia ili kupitia kitengo cha assets recovery unit ili mabilioni ya fedha na mali zisizoondosheka zinazomilikiwa na watanzania katika mabenki ya nchini switzerland, dubai, mauritius na visiwa na maeneo mengine yote ambapo hufichwa fedha na mali ili kukwepa kodi na kwamba mali hizo na mabilioni hayo yaliyopatikana kiharamu yarudishwe nchini mara moja.

(iv)kwamba, katika muswada tajwa hapo juu, gavana wa benki kuu ya tanzania aimarishiwe mamlaka ya kutoa kibali kwa mtanzania yeyote anayetaka kufungua akaunti ya benki nje ya nchi na kwamba kila mwaka gavana atatangaza kwenye gazeti la serikali na magazeti yanayosomwa na wananchi wengi orodha ya watanzania walioomba na walioruhusiwa kuwa na akaunti ya benki nje ya tanzania;

(v)kwamba, watanzania wote wenye akaunti za fedha nje waeleze wamezipataje na takukuru wachukue hatua za kisheria dhidi ya watu wote wenye kumiliki fedha na mali kinyume na mapato yao halali;

(vi)kwamba, serikali, katika mkutano wa bunge wa kumi na moja (11) na baada ya taarifa ya kamati teule ya bunge kuhusu raia wa tanzania wenye kumiliki fedha za kigenikwenye mabenki na mali nje ya tanzania ilete taarifa ya hatua ilizochukua ili kuziba mianya ya utoroshaji wa fedha nje ya tanzania.

(vii)kwamba, serikali katika bajeti ya mwaka 2013/2014 itaanzisha kodi maalum ‘financial transaction tax' ya angalau asilimia 0.5 ya thamani ya ‘transaction' ili kuweza kuwa narekodi zauhakika za fedha ndani na zinazotoka nje ya nchi.

Swali, ni kipi kimefanyika hadi sasa zaidi ya jitihada za kuligeuza suala hili kuwa naming and shaming politics?

hili tuliite azimio la kigoma
 
Back
Top Bottom