Mkwawa
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 1,334
- 1,464
ZZK amewataja walioficha fedha nje, kasema mawaziri wakuu 2003 - 2010 hapa alikuwa Sumayi, Lowassa, Pinda. Mawaziri wa nishati na madini toka 2003 - 2010 , makatibu wakuu wa nishati na madini, makamishna wa nishati na madini itabidi nimuulize Kafumu yeye ana ngapi, wakuu wa majeshi, 2003 -2010 waziri wa ulinzi .
Tuwe wakweli hapa, ni wazi anachokisema ZZK kina maana kubwa sana ya kuzuia mianya ya utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na upatikanaji wa fedha haramu na kuzificha. Ila its too political kuliko reality. Je kwanini alisema ana majina kumbe ana vyeo vya wezi. Je kwanini uchunguzi huu anataka ubakie kwa wale wenye vyeo tu wakati BAE ilishirikisha hata wafanyabiashara uchwara.
Je watanzania wanaoishi nje, kufanya kazi, biashara na wana account zilizonona nao wapo kundi gani la kuchunguzwa. Wapo wafanyabiashara wenye account nje ili kurahisha ubadilishaji fedha hasa za kigeni sio wizi wala kukwepa kodi, na wengine ni wizi na kukwepa kodi.
Mpaka sasa sheria za nchi zinasemaje kuhusu mtanzania kuwa na account nje ya nchi. Vita hii itakuwa ngumu sana, kwani wnaotakiwa kuchunguzwa ni wale Prof Kapuya alisema ndio serikali hakuna wa kuwagusa. Hatuwezi kuchunguzi kupitia mfumo wa serikali wa sasa tukapata majibu. Kama EPA ilitiwa kapuni au Meremeta imekuwa donda ndugu, kwa serikali hii hakuna jibu hapa.
ZZK ilimpasa ashirikiane na chama chake ambacho yeye ameamua kukisambaratisha ili kupata majibu ya haya ila kwa solo siioni mbali.