Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 8,942
- 6,860
Si unajua kisa cha cholera kumvunja ngamia mgongo. Tukiwa wakweli, chaguzi za 2019 na 2020 zilipitiliza kwa brazenness. Kabla ya hapo palikuwa na modicum ya kiaibu. Their brazenness ndio unawafanya washindwe kutoa matokeo ya kila kituo mpaka leo. Walimgusa kipofu wakati wa kula. In all honesty, unaweza kuamini kabisa kuwa wagombea wote wa Chadema hawajui kujaza fomu? Na kuwa nchi nzima ni wabunge wawili tu wa upinzani ndio wameshinda? Watu walitiwa ndani dakika chache kabla ya deadline ya kurudisha fomu ili mgombea wao apite bila kupingwa! Wasimamizi walijifungia au walihama ofisi ili wasipokee fomu za wapinzani halafu voila, wanajitokeza kumtangaza mgombea wa CCM kuwa mshindi! Na hayo ni sehemu tu.Lakini Fundi…CHADEMA hao mbona wameshiriki chaguzi nyingi tu chini ya hii hii tume ambayo wameisusia sasa?
Kama hii tume ya sasa si huru, ina maana tume za 2015, 2010, na 2000 zilikuwa huru?
Watu mpaka leo wanasota magerezani kwa sababu tu walimshabikia mpinzani. Na wengine baada ya kusota muda mrefu wameachiwa bila hata aliyewashitaki kujisumbua kuwasilisha ushahidi!
Anaeshangaza ni yule anayeamini kuwa waliofanya yote hayo watamruhusu ashinde kirahisi. Kwa kifupi hamna Tume iliyokuwa huru lakini hii ya sasa imezidi. Badala ya kuweka kidole kwenye mzani wameukalia kabisa.
Amandla...