Zitto Kabwe autaka Urais

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema dhamira yake kubwa ya kuwa kwenye ulingo wa siasa ni kuwa Rais wa Tanzania atakayeibadilisha nchi pale ilipo na kupiga hatua kubwa kimaendeleo.

Zitto alitoa kauli hiyo jana Dar es Salaam alipohojiwa katika kipindi cha Super Breakfast kinachorushwa na Kituo cha Redio cha East Africa ingawa hakutaja kama atagombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu ujao wa 2025.

Alisema dhamira yake kuu kama mwanasiasa ni kuona siku moja anakuwa Rais wa Tanzania kupitia mifumo halali ya kiuchaguzi na kwamba ukaribu wake na baadhi ya mawaziri wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), una lengo la kupanga safu ya uongozi kwa ajili ya uchaguzi wa 2025.

"Tunajenga chama ili siku moja kije kushika dola na kila mwanasiasa dhamira yake kuu ni kushika nafasi ya juu kabisa ya kisiasa inayotokana na mifumo ya kisiasa na nafasi hiyo ni urais na mimi ninautaka urais," alisema Zitto.

Aliongeza kuwa kwa sasa yeye ni kiongozi mwenye jukumu la kuhakikisha chama chake kinapiga hatua ya kimaendeleo, ikiwamo kuongeza wanachama kusimamia sera za chama na kuhakikisha anakabidhi majukumu hayo kwa kiongozi atakayekuja badala yake.

"Mwezi wa tatu (Machi) mwakani mimi nitang’atuka katika uongozi wa chama, nitakuwa nimeshatumia mihula miwili ya uongozi kwenye nafasi hiyo, nitawaachia wenzangu watakaochaguliwa kuongoza lakini dhamira yangu ya siku moja kuwa Rais wa Tanzania itabaki pale pale," alisisitiza Zitto.

MIKUTANO YA HADHARA
Akizungumzia nafasi ya vyama vya siasa baada ya kuondolewa kwa zuio la mikutano lililodumu kwa takriban miaka saba, Zitto alisema mfumo wa demokrasia ulirudishwa nyuma kwa miaka 30 wakati kulipokuwa na chama kimoja na kwamba sasa vyama vya siasa vina kazi ya kujijenga upya katika maeneo mbalimbali nchini.

Zitto alisema moja ya vitu walivyopigania kwenye kikosi kazi ni kuwapo Katiba Mpya, jambo ambalo kwa sasa limezungumzwa na karibu kila chama.

Alisema kuwa wakiwa kwenye kikosi kazi, walitaka mikutano ya hadhara iruhusiwe, mchakato wa Katiba Mpya ufanyike ikiwa ni pamoja na uandishi wa sheria mpya ya vyama vya siasa na ya uchaguzi.

Alieleza kuwa baadhi ya watu wanaosema Katiba haileti chakula, ni watu wa kupuuzwa kwa kuwa kila kinachofanyika nchini kinahusisha katiba, hivyo kuiepuka ni jambo lisilowezekana.

NIPASHE
 
Ajifunze kwa mama mgwira, hawajawahi kupata kura zaidi ya elfu tisini nchi nzima.
 
Ninataka Zitto agombee urais I'll ajionee mwenyewe Hali ilivyo, maana akiwa CHADEMA alikuwa akitishia anautaka urais ili tu kuleta sintofahamu.
 
Hata Dovutwa na Rungwe wanataka urais, hawana tofauti na Zitto.
Ndugu yangu acha kabisa kumfananisha Mzee Rungwe na vitu vya ajabu ajabu (mfano wa Zitto, Dovutwa, Lupumba nk), Mzee Rungwe ni level nyingine kabisa ya kisiasa.

Yule mzee wakati anagombea urais alikuwa yuko real na sera zake, aliomba tumpe urais ili ahakikishe tunapiga msosi fresh watanzania wote, from there mengine yangefuata.
 
Ndugu yangu acha kabisa kumfananisha Mzee Rungwe na vitu vya ajabu ajabu (mfano wa Zitto, Dovutwa, Lupumba nk), Mzee Rungwe ni level nyingine kabisa ya kisiasa.

Yule mzee wakati anagombea urais alikuwa yuko real na sera zake, aliomba tumpe urais ili ahakikishe tunapiga msosi fresh watanzania wote, from there mengine yangefuata.
wasitupoteze kwenye reli,mzee rungwe sera ni kuhakikisha ubwabwa uko available bila kokoro watu washibe.
hatujamsikiliza angalia sasa kinachotukumba:D
 
Dah huyu mwamba nikimkumbuka enzi zake. Siku hizi hawashi kiukweli, amekumbana na "tragedy miscalculations" katika siasa zake. Siasa bwana😁
 
Back
Top Bottom