Zitto Kabwe: Adui, Rafiki, Kipenzi


Kaka kwa mtu anayejitambua na kujithamini atalichukua hili na kulifanyia kazi lakini kwa mtu anayejikweza hajui maana ya kujishusha mbele za watu na kutaka kuonekana kwa watu hakika huyo hajitambui na mtu kama huyo ni aheri kumwelekeza mbuzi kunywa maji kuliko kiumbe mzito kama huyo.
 
jinsi alivyo empty headed,hata hapa hatokuelewa!
 
......
Ulipotimuliwa Chadema, sikumbuka kama kuna yeyoye aliyekulilia humu kama mimi!, naomba nikukumbushe tuu
Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili ...


Pasco

Aaah....

Hata hivyo Pasco wa JF nakushukuru sana kwa msaada wa ushauri wa kitabibu wa kisaikolojia unaoutoa kwa Juliana. Juliana ni mwaafrika tena mtanzania mwenzetu. Hivyo, hatuna budi kumsaidia afya yake inapozorota...lakini akishapona tumdhibiti asilete madhara kwenye mikakati yetu ya kuboresha maisha ya watanzania na waafrika kwa ujumla.
 

Kwa Sheria zetu Za humu ndani ..mtu Ana hiari ya kuwa verified member au hoax ......usipoteze muda kujua nani ni nani humu JF ....ni Kama kutaka kuingia chumbani kwa baba yako na mama yako ...usiku !!!!!
Sheria zetu ziko wazi .....hazina tofauti na Za Intelligence ....." Ni kosa la jinai kumtangaza mtumishi au wakala ...." ....humu ndani watu wanafanya kazi kubwa kuliko hata Hiyo ya TISS ...na wao wenyewe huvuta Mpunga wa kukusanyia taarifa na kuja Huku ..,wakapata nondo Za uhakika ......so leave PASCO ..alone usitake kumjua ,.hadi Siku akiamua yeye mwenyewe kuja open ....unafanya kosa ..Sana lamkukemewa
 

Sitaki kusema kuwa wewe ni Nguin ..KILAZA ...hapana ...,ila napata mashaka Kama kila aliyejibu unamuoa hajakujibu ...count me off kwa sababu pengine Mimi sikuona content yeyote yenye MANTIKI Kama nilivoelezea awali .....Zaidi ya kuhisiwa kuwa pengine ...uko so depressed ..,na ukiacha Ndugu yetu Mwigulu ambaye kidogo amekuwa na moyo wa kibinadamu ....wengine hawajataka kuwaamini ...na kuwafanya mpate inferiority complex syndrome ....na kawaida ya Hali Hii ....ni kutafuta namna yeyote ya kupata attention kwa watu....

Nakumbuka kibwagizo cha wimbo wa ...DDC MLIMANI PARK ORCHESTRA ....( literally to tell you kuwa wengine Huku sio watoto wenzako ....)
Kisa Hiki kilimkuta Almarhum Muhidin Gurumo ...Baada ya Kurubuniwa na Kujiunga na band ya Ochestra Safari Sound " wana ndekulle " ...kwa ahadi ya Gari ..,nyumba na mengine ..Baada ya muda akagundua kuwa ahadi zilikua uwongo na akawa anajipitisha kwa bwana wa zamani ...ili arudiwe ..

Kwenye wimbo huu Cosmas Chidule akaimba...

" sio wewe peke yako wako wenzio waliondoka ...
Na bado tunapanda nao ,
UDA NA DALA DALA ...

ULISEMA MWENYEWE UMEPATA BWANA MWENYE PESA EHEEEEE....
ATAKUJENGEA NYUMBA.....
ATAKUNUNULIA GARI EEEE..
SASA UNALIA......
 
Kuna kashfa inaenda na kujirudia kuwa Bwana Zitto Zuberi Kabwe (Mwanasiasa msafi kuliko wanasiasa wote kuwahi kutokea Tanzania) ni moja ya watu walionufaika na mgao wa fedha za escrow, japo sijawahi msikia akitamka kwa ulimi wake kuwa hajapokea, ameishia kusema watu wachunguze, nitaendelea kuamini katika misingi ya mtu ni huru mpaka pale itakapothibitika kua ana makosa.

Lakini kaka yangu huyu amekuwa ni mtaalamu mzuri wa matumizi ya "fallacy" kwa waliosoma falsafa wataelewa. Zinapozuka kashfa dhidi yake, huwa anatumia A kujibu swali B.

Tundu Lissu alipomkashifu kwa kupokea pesa toka kwa Mkono na mpaka sasa ana miliki magari mawili ya Mkono, Bwana Zitto aliishia kuhamishia kashfa kwa Mh. Mbowe, na kusema haongei na kifaranga yaani Lissu, hii kwenye falsafa inaitwa appeal to mockery ab absurdo lakini pia mbinu nyengine mheshimiwa hutumia ni Argumentum ad misericordiam au kwa lughanyepesi appeal to pity (inatafsiriwa kama kuweza kushinda mjadala kwa kuvuta hisia na huruma ya walio wengi) Ilipozuka kashfa kuwa bwana Zitto Kabwe kuna ufisadi anafanya kupitia kampuni ya Gombe advisors, Bwana Zitto alijibu ameumizwa sana kwa kuwa yupo busy anamuuguza mama ( Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema Peponi aamin) ilipoibuka tena bungeni kashfa ya kupokea hela za escrow alisema tumuache mama apumzike kwa amani.

Lakini kwa kuwa vifaranga vimekuwa, na hana anayemuuguza, tunaomba sasa atujibu kwa ufasaha kwa kuwa maelezo yake ya awali yalijaa na uuguzi, kuhusu mikataba wa leka Dutigite kwa upande mmoja na NSSF na TANAPA kwa upande mwengine

Kampuni ya Leka Dutigite ina wana hisa 16, 15 kati yao ni wasanii wa kizazi kipya wenye hisa asilimia 5 kila mmoja hivyo kuwa idadi ya asilimia 75 na asilimia 25 zilizobakia zinamilikiwa na Gombe advisors. Swali huyu Gombe ni nani?

Ukienda kuangalia makabrasha ya Brela Gombe advisors inamilikiwa na watu wawili, mtu mmoja mwenye jina la kikenya mwenye asilimia 25 na Bwana Zitto kabwe ambae kwenye fomu amejijaza kama mchumi badala ya kiongozi wa Umma

Kwa hiyo kumbe NSSF na TANAPA mashirika ya Umma ambayo yanakaguliwa yasifanye ufisadi na Bwana Zitto kabwe kwa mkono wa kulia, ukija mkono wa kushoto unakuta Bwana Zitto kabwe ndo mwanahisa mkuu kwenye mikataba ya kibiashara baina ya NSSF, TANAPA na leka dutigite, japo yeye anadai hakuna mgongano wa kimaslahi.

Katika tenda moja, NSSF iliilipa Leka Dutigite shilingi milioni 120, milioni 90 kati ya hizo zilitolewa siku moja baada ya kuwekwa, siku moja kabla ya uchaguzi wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma PAC uliomfanya Bwana Zitto kuwa mwenyekiti wa kamati na kumng'oa mzee Cheyo aliyekuwa anafanya kazi kwa weledi mkubwa. Coincidence?

Na ni bahati nzuri kuwa hizo pesa zilienda kutolewa na Habib Mchange, (bank statement inaeleza hivyo) aliyefukuzwa Chadema kwa kosa la kuwa kibaraka wa Zitto na kupanga mapinduzi ndani ya Chama, leo ndio katibu mkuu wa LekaDutigite kampuni ambayo Zitto anasema hana maslahi humo, kwa nini aweke watu wake?

Sasa hapa kuna maswali yanajitokeza

1. Je NSSF na TANAPA ni mashirika ya Umma au hapana? Na je Zitto ni kiongozi wa Umma au Hapana?

2. Je Zitto anayakagua haya mashirika au hapana?

3. Je katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 sura ya 6 sehemu ya 2 Na sheria ya utumishi wa Umma inamruhusu kiongozi kama yeye kuingia mkataba na mashirika ya Umma ukiachila mbali mashirika yanayoripoti chini yake?

4. Kama Gombe advisors si kampuni ya faida, kwa nini ijimilikishe hisa asilimia 25% Za Leka Dutigite? Je si ingekuwa sahihi ingebaki kuwa mshauri tu na wasanii wakagawana asilimia 100 ya kampuni ili wanapogawana faida wagawane kwa uwiano sawa kutokana na mgawanyo wa hisa zao.

5. Kwanini aweke watu wake wa karibu kuwa ndio viongozi wa Leka Dutigite kama yeye ni mdhamini tu na mshauri wa wanamuziki?

Mimi naamini hakuna ujanja ujanja unaodumu kwa muda mrefu nchi hii kabla haujagundulika, Chama Chake kimeshamjua, ipo siku hao anaowatumia kwenye ujanja ujanja wake watamgeuke na ukweli utawekwa hadharani. lakini hadi hapo yatakoapotokea hayo, bado nasubiri siku nione Zitto Kabwe akiikosoa NSSF na TANAPA kwa kuwa mpaka sasa kila akiongea mifano mema hutolea mashirika haya mawili. Mimi ndio yule yule niliyemtabiria kufukuzwa kwenye chama siku aliyochaguliwa kuwa kiongozi wa chama
 
.... ,.hadi Siku akiamua yeye mwenyewe kuja open ....unafanya kosa ..Sana lamkukemewa
Point taken at high order seriousness !. Realy I mean it, please, edit my text in 'your post with quote' by removing a paragraph with kind of name calling as I have done in my original post.
 
Huyu ni mtu ambaye CCM wanatamani awe na nafasi ya juu ya uongozi katika chama kikuu cha upinzani

Ni sawa na kocha wa Yanga kung'ang'ania apewe jukumu la kupanga timu ya Simba kupambana na Yanga, au kocha wa Barcelona kupanga timu ya Real Madrid kwa ajili ya El Clasico.
 
Njia ya Muongo fupi tunamsubiri apande majukwaani na ACT-MWANDIGA yake aanzishe mashambulizi, atapata majibu yanayomstahili kabisa..
 
Mimi naamini hakuna ujanja ujanja unaodumu kwa muda mrefu nchi hii kabla haujagundulika,
ni kweli kabisa njia ya mwongo kama alivyo mnafiki huwa ni fupi - ni suala la muda tu. yetu subira!!
 
Niliwahi kuona thread hapa inayoeleza kuwa Kinana katika safari zake za kukiua chama chake huko mikoani alifika katika kata mojawapo wananchi bila aibu wakamtaka akanushe/au athibitishe kuwa ni lini ataacha biashara ya kuua tembo wetu kwa maslahi binafsi. Nasikia aliukimbia mkutano huo bila kujibu. Naona ZZK anajaribu kujijengea mazingira kwa wananchi ambapo siku moja watamuuliza maswali ambayo itamuwea vigumu kujibu.
 
Tunamsubiri Zitto kwa hamu apande jukwaani na ACT yake lakini awe tayari amejiandaa kisaikolojia kuleta majibu ya tuhuma zake zote za ufisadi anaohubiri kuwa anaupinga na hata fedha walizochukua na mwenzake Filikunjombe kwenye uchunguzi wa sakata la Tegeta Escrow
 
siku za zitto mbona zinahesabika ngoja aende ACT aanze kupanda majukwaaani ndo ataona
 
Ama kweli uandishi ni kazi ya watu... Hii habari isingeweza andikwa na mtu asokuwa na kipaji na utaalam wa uandishi na sijui kilitokea nini hata watu wasione umuhimu wa yale mafiga matatu - Ubarikiwe!
 
siku za zitto mbona zinahesabika ngoja aende ACT aanze kupanda majukwaaani ndo ataona
Sijawaeleweni mimi, bado mnamtaka Zitto au hampendi kuona akienda ACT? Binafsi nisichoweza kuamini ni kile kinachosemwa kwamba ZITTO siyo mchafu, hili nakataa, haya mengine ya kupanda majukwaani siwezi kumhukumu.
 
Sijawaeleweni mimi, bado mnamtaka Zitto au hampendi kuona akienda ACT? Binafsi nisichoweza kuamini ni kile kinachosemwa kwamba ZITTO siyo mchafu, hili nakataa, haya mengine ya kupanda majukwaani siwezi kumhukumu.

Mkuu Kama umekiri zitto ni mchafu well done mkuu
 
Davesto kuwa na ubinaadamu. Hakuna msiba ulio na mwisho. tumuacheni mama apumzike jamani.
 
Last edited by a moderator:
Habari ya mjini mpini wa Escrow umewaingia CCM pabaya wakakaa nchale...wakinuka nchale....wakisimama nchale ,scandal ya ufisadi inafanana na GOLDENBERG iliyoing'oa serikali ya KANU ya Kenya twende kazi ....moja wa ma actor ni Harbinder Singth Seth yule yule international mwenye mafunzo makali ya kuiangusha serikali bila kuigusa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…