Zitto Kabwe: Adui, Rafiki, Kipenzi

Zitto Kabwe: Adui, Rafiki, Kipenzi

harakati za Zitto na za lowasa kitu moja.
 
Last edited by a moderator:
Unajisumbua bure tu na udaku wako hapa.
Kwa taarifa yako ni kwamba hakuna mwana-ccm au mwana-chadema ambae ashawahi kumkabili Zitto kwa tuhuma uchwara km hzo akashinda.
"Sijawahi kushindwa vita yoyote ya kulinda reputation yangu"...

Hayo unaoona we leo ni maswali ashayajibu, akaenda mbali zaidi kuita vyombo vya uchunguzi na kamata za maadili zimchunguze. Juzi ngeleja aliporopoka ameitaka Sekretariat ya maadili imuite kumhoji km kutakua na tuhuma zimazomhusu na atazitolea maelezo.

Sio bure, una agenda yako ya siri.
 
Hoja marudio hii,sina tabia ya kuhukumu wala kudharau maoni ya mtu kwa vigezo vyovyote.Ila katika hili jamani tuache porojo,tuweke ukweli kwa vithibitisho kudhibitisha kashfa husika.Hizi lugha za kila siku mitandaoni sidhani kama zinaweza kuleta impacts zozote kisiasa kule field.Tumwamini nani mkweli? Anayetoa kashifa bila chembe ya ushahidi au anayetangazia umma kuwa yuko tayari kwa vyombo husika kumchunguza ili ukweli ubainike na haki itendeke.Kuhusu ZZK kwenda ACT hiyo ni haki yake kikatiba jamani,mwacheni mtoto wa watu apige siasa huko kwani huko alikokuwa hatakiwi.
 
Zitto Kabwe ni adui yao, akina nani hao? Ni rafiki yao, hao wenye uswahiba naye wapoje? Ni kipenzi chao, wasifu wa hao wanaompenda ni upi? Andiko hili linachambua kila kipengele katika muktadha mpana.

ADUI

Kunguni ni mdudu anayechukiwa sana na binadamu. Hawezi kuwa na jema hata kidogo. Huo wema wa kunguni umeanza lini? Ni mchokozi, msumbufu, mharibu starehe ya usingizi. Sisi tuliopitia maisha ya kulala na kunguni tunaelewa. Ambao hawajapitia, heri yao!

Wasifu huo ndiyo ukaibuka msemo wa “damu ya kunguni”, anayesemwa au kujisema kuwa na damu ya kunguni maana yake anachukiwa na watu. Hana jema, kila atakalofanya, litageuzwa kwa uzuri wake kisha kupewa sifa mbaya. Lengo kuu ni kwamba aonekane mbaya kila siku.

Unamsifiaje mtu mwenye damu ya kunguni mbele za watu? Kama hutachekwa, basi na wewe utachukiwa. Utawekwa kapu moja na mwenye damu ya kunguni. Almasi ya mwenye damu damu ya kunguni ni chupa, dhahabu ni shaba.
Pamoja na kazi kubwa aliyofanya, akiongoza kamati yake ya Hesabu za Serikali (PAC) kusoma, kuchambua na kutafsiri makabrasha ya ripoti ya CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali) kuhusiana na skendo ya Tegeta Escrow, na kutoa mapendekezo.

Pamoja na kuukataa usingizi, kuamua kukesha akilinda ripoti ya PAC ili kuhakikisha haichakachuliwi kwa namna yoyote ile. Pamoja na ushujaa wa kuchambua madudu katika Akaunti ya Tegeta Escrow na kuwaumbua (naming and shaming) wahusika, bado damu ya kunguni ilidhihirika kuwamo ndani ya Zitto.

Kosa lake lilikuwa kuunga mkono muundo wa pendekezo (formulation), lililotolewa na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge. Lililohusu namna ya kuishauri serikali (mamlaka ya uteuzi), kuchukua hatua za kumwajibisha Katibu Mkuu aliyesimamishwa, Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi.

Kabla ya Chenge, kila pendekezo liligonga mwamba, Spika Anne Makinda, alitaka lugha laini zaidi katika kuishauri serikali. Chenge alipotoa formulation yake, ikaungwa mkono haraka sana. Spika akaona ina nafuu kubwa. Zitto na Halima Mdee waliiunga mkono, wabunge wengi wa CCM wakashangilia.

Zitto akashauri, mapendekezo yaliyobaki ambayo yaliwagonga nyundo moja kwa moja, Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, yaandikwe kama Chenge alivyoshauri.

Spika Makinda akaona “mambo si ndiyo hayo”, akakubali, wabunge wa CCM wakagonga meza kwa fujo. Spika akawauliza wabunge, sauti ya wengi ikasikika “ndiyoooo”. Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, akashtuka, akasema hapana, “mnatuburuza.”

Msimamo wa Mbowe ukaibua zogo bungeni. Wabunge wa upinzani, hususan wale wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wakamuonaZitto msaliti. Inakuwaje anakubali pendekezo la Chenge?

Zitto alishakuwa na sifa ya usaliti. Kwamba anakisaliti chama chake (Chadema) na upinzani kwa jumla. Kitendo kile cha kuunga mkono pendekezo la Chenge, akatafsirika kama “mja asili asiyesahau asili yake”, alionekana amerudia zake za usaliti.

Chenge pia ni walewale wa damu ya kunguni, kwa hiyo hana jema. Pendekezo litolewe na Chenge? Haikuingia akilini kabisa kwa wapinzani! Kosa kubwa ni kwamba wapinzani badala ya kutathmini na kuona ubora au ubaya wa pendekezo la Chenge, wao wakamwangalia mtoa pendekezo, Chenge!

Laiti ‘msumari’ wa Zitto kwa kugandamizia pendekezo la Chenge, ungepita, leo hii Waziri Mkuu na Masele nao wangekuwa tumbo joto. Haikuwa hivyo, wapinzani walimuona Zitto anasaliti kwa sababu hawaamini katika “baniani mbaya kiatu chake dawa”, kwao Chenge ni baniani ambaye kiatu chake hakiwezi kuwa dawa, asilani, abadan!

Baada ya hapo, mitandao ya kijamii ikaingia kazini, Zitto alishambuliwa kwelikweli. Wachache waliojua ubora wa pendekezo la Chenge, walitetea kuwa Zitto alikuwa mjanja sana, mwenye akili akili za kimkakati kuunga mkono pendekezo la Chenge. Wengi hawakumwelewa, walimshambulia, walimponda.

Kama alichokisema Zitto, kingetamkwa na Tundu Lissu, hali isingekuwa mbaya kwa kiasi kile. Tatizo la Zitto ana damu ya kunguni. Alivyokuwa anatenda kazi yake kwa umahiri mkubwa, wasiomwamini walikuwa wanamfuatilia kwa umakini, wakiamini lipo eneo atateleza wamseme.

Zitto ni sawa na mchezaji mzuri asiyependwa. Kama ilivyowahi kutokea kwa Ryan Giggs, Manchester United au hata hapa Tanzania Haruna Niyonzima, Yanga, na wengineo, wakishika mpira, wanacheza vizuri sana, wanafanya mambo mengi makubwa yanayostahili pongezi lakini hawashangiliwi, ila kosa moja litasababisha azomewe kila upande. Kisa hawampendi, amewaudhi! Siku hizi Niyonzima hazomewi.

Wakati wa kuelekea kusomwa kwa ripoti ya PAC kuhusiana na Tegeta Escrow, pamoja na kuwepo kwa watu kumuunga mkono Zitto na kumtia moyo kwamba asiogope, wapo nyuma yake, wapo waliotamka bila kificho: “Zitto ni msaliti, muda utakapofika atapindisha ukweli ili kuwaokoa wachotaji wa fedha za Tegeta Escrow.”

Kwao, Zitto na waliochota fedha za Escrow ni walewale. Kwa maana hiyo walitoa angalizo huku wakimfuatilia kwa makini mithili ya macho ya mashabiki kwa mchezaji mzuri wasiyempenda anapokuwa anachanja mbuga na kupiga chenga za maudhi uwanjani, wakisubiri akosee wamzoemee. Alipounga mkono tu pendekezo la Chenge, wakazomea, wakasema “si tulisema!”

Hata baadaye, ipo hoja iliibuka kwamba katika Tegeta Escrow, Zitto alitumiwa na makundi ya CCM kwa ajili ya mnyukano wa mbio za Urais 2015. Wapo waliosema ‘alishikishwa’ kiasi kikubwa cha fedha na mzee Reginald Mengi ili kumwadabisha Muhongo kwa sababu wana bifu la vitalu vya gesi.

Hayo ni matokeo ya kuwa na damu ya kunguni, ufanya jema litageuzwa kuwa baya na ukitenda baya ndiyo kabisa. Katika mazingira kama hayo, wengi hujikuta wanayumba. Japo anajitahidi kubaki kwenye mstari, mara nyingi Zitto ameshayumbishwa na mashambulizi mpaka kujikuta anajibishana na wanaomchokonoa, au kutamka yasiyopendeza.

Zitto ni adui wa CCM, kwa maana ni mbunge mnoko. Kazi yake imeshaivua nguo serikali ya CCM mara kadhaa. Ni kiherehere, kwa sababu anafuatilia sana. Na akishafuatilia hana siri, haraka sana yataonekana mitandaoni, Twitter, Facebook na kadhalika kabla ya kufika bungeni.

Unoko wa Zitto unaosababisha asipendwe na CCM pamoja na serikali; Palipo na wizi au kashfa yoyote ile, lazima kivuli chake kitaonekana na atasema kuhusu skendo husika. Hali hiyo imesababisha aingie kwenye misukosuko mingi. Muwinda huwindwa!

Mwaka juzi, katika Bunge la Bajeti, kuelekea bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, Bodi ya Tanesco ilimsimamisha kazi, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu, William Mhando. Baada ya uamuzi huo, ikaibuka kashfa kuwa bodi ilifanya makosa ya kukiuka sheria ya manunuzi katika kununua mafuta ghafi.

Ikabainika kuwa pamoja na makosa ambayo Mhando anatajwa kuwa nayo, yapo maelezo kuwa tofauti yake na bodi, ilisababishwa na yeye kupinga ukiukwaji wa makusudi wa sheria ya manunuzi. Kwamba mshindi wa zabuni ananyimwa halafu anapewa aliyeshindwa.

Zabuni imetangazwa, makampuni kadhaa yamejitokeza kuwania tenda. Kila moja inatangaza ofa yake, baadaye baada ya kupima vigezo kampuni moja ikashinda. Ajabu iliyopewa tenda ikawa kampuni tofauti na ile iliyoshindaa. Hiyo ni kashfa, na kulikuwa na sura ya wazi kwamba rushwa ilichukua nafasi.

Zitto akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) wakati huo, akamwandikia barua Spika Makinda, kuomba kamati yake iruhusiwe na bunge kuhoji pande zote mbili, Mhando na bodi ya Tanesco.

Haraka sana picha likageuka; Ikaelezwa kuwa Zitto alihongwa na makampuni ya mafuta kwa ajili ya kumtetea Mhando. Hali ilikuwa mbaya sana mpaka akaita mkutano na waandishi wa habari kujitetea lakini haikusaidia. Ilisababisha mpaka baadhi ya wabunge kuomba uongozi wa POAC uondolewe.

Spika Makinda alipoiagiza Kamati ya Ngwilizi (Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi) kufanya uchunguzi, ikabainika Maswi na Muhongo, walisema uongo kwa lengo la kushawishi bajeti yao ipite na kuwadhibiti waliokuwa wakiipinga kwa kupitia kashfa ya ununuzi wa mauta ghafi.

Kipindi hicho, Zitto alitoka kwenye mstari, alimtumia SMS Maswi akamwambia: “Maswi sijawahi kugombana na wewe kwa kuwa nakuheshimu sana. Tuhuma ambazo wewe na waziri wako mnazitoa dhidi yangu ni uongo, uzushi na za kupikwa.

“Mwambie waziri wako na wewe binafsi, sijawahi kushindwa vita ya kulinda credibility yangu, sipendi ujinga hata kidogo, mimi nina uhuru wa kusema ninachokiamini, sina bei, tupambane tu tuone nani ataumia.”

Maswi na Muhongo walionywa na bunge wakati huo, ila baada ya matokeo ya sasa katika skendo ya Tegeta Escrow, tayari Maswi ameshasimamishwa kazi, Muhongo anaendelea kuvutiwa ‘uradi kwa tasbihi’. Swali nani ameumia? Majibu yapo wazi.

Siri moja, ukiwa mtu halisi hutafeli hata mara moja. Vita ya Maswi na Muhongo upande mmoja na Zitto upande wa pili, inanipa majibu kuwa mkweli ameendelea kuwa imara pamoja na misukosuko yote. Mzushi, pigo moja tu, leo yupo chali. Kwa hapa Zitto ni halisi zaidi.

Zitto akaichachafya serikali ya CCM; Alimtaja Waziri wa Fedha wakati huo, Mustafa Mkullo kwamba ni fisadi, kisha akalinyooshea kidole Baraza la Mawaziri kwamba lilihongwa ili kulifuta Shirika Hodhi la Rasilimali za Mashrika ya Umma (CHC) kwa sababu za kifisadi.

Mawaziri wakawa wakali, wakamtaka Zitto athibitishe, yeye aliwasilisha uthibitisho wake na kuanzia hapo ikawa kimya. Mawaziri walinywea! Haihitaji kutumia darubini kujua kuwa Zitto ni adui wa Baraza la Mawaziri kwa sababu alisema lilihongwa. Mawaziri hawawezi kumpenda. Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri ni Rais, kwa maana hiyo JK hawezi kumfurahia.

Mkullo alisema Zitto anatumika na kwamba anahongwa. Zitto akatoa uwanja huru, kila mmoja aruhusu kuchunguzwa ikibainika yeye (Zitto) amewahi kuhongwa, atajiuzulu uenyekiti wa POAC, ubunge na ataacha siasa.

Akamtaka Mkullo kutangaza kuwa tayari kuuacha uwaziri endapo itathibitika amehusika na ufisadi akiwa Waziri wa Fedha. Mkullo alinywea lakini ripoti ya CAG ya mwaka 2012, ilimng’oa Mkullo pamoja na mawaziri wengine saba.

Kabla ya kung’oka, mawaziri walikuwa wabishi, Zitto akaanzisha mchakato wa kukusanya saini 70 ili zihalalishe hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu. Mambo kabla hayajawa mabaya sana, Mkuu wa Nchi aliwaondosha mawaziri wote waliokumbwa na kashfa. Je, huyo si adui wa serikali ya CCM?

Ni Zitto aliyetimuliwa bungeni mwaka 2007 kwa sababu ya kupeleka bungeni hoja ya Buzwagi, akimtaja aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, kusaini mkataba kimagumashi, kinyume hata na agizo la Rais, aliyetaka isisainiwe mikataba mipya ya madini mpaka kwanza ile ya awali ipitiwe upya.

Zitto akaonekana mbeya, kizabizabina, aliyekusudia kuivua nguo serikali na kumharibia ulaji Karamagi, akasimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge. Hii ni kuthibitisha kuwa Zitto ni adui wa CCM na ubunge wake umekuwa mwiba kwa maovu ndani ya Serikali ya CCM.

Mwaka 2008, baada ya hotuba ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alipotangaza kujiuzulu, Zitto aliomba muongozo kwamba kwa mujibu wa Katiba, Waziri Mkuu anapojiuzulu na Baraza la Mawaziri linavunjika, kwa maana hiyo mawaziri wote hawana kazi. Mawaziri walimzomea, walimuona mnoko, anayechonga sana. Walipinga! Hawakujua wanapinga Katiba.

Ni Zitto ambaye alishawekewa sumu kwenye maziwa, akaokolewa na simu ya marehemu Amina Chifupa, aliyemwambia asiendelee kunywa, ni sumu. Akatibiwa Hospitali ya Rufaa, Bugando, Mwanza. Ni Zitto aliyenusurika kifo kwa ajali kadhaa, ikiwemo zilizotajwa kusukwa!

Ni adui wa wapinzani, maana anaonekana ni msaliti, anayetumiwa na CCM kudhoofsha upinzani nchini. Zilishatolewa ripoti kadhaa (japo hazikuwahi kuthibitishwa), zikionesha namna Zitto alivyo na ukaribu na Usalama wa Taifa pamoja na Serikali.

Taarifa kwamba Zitto ni msaliti wa upinzani, zilianza tangu mwaka 2008. Maneno hayo yameendelea kuchukua nafasi mpaka leo. Sura hiyo imemfanya Zitto kuonekana kibaraka, mamluki wa CCM. Wasambazaji wa maneno haya walifaulu, ila hawakuweza kummaliza.

Hiyo ndiyo sababu ya Zitto anapokuwa kwenye wakati muhimu zaidi kushughulikia mambo nyeti kwa taifa, badala ya kuungwa mkono kwa asilimia 100, wapinzani wanakuwa wanamtolea macho, wakivizia akosee wamzomee!
Uthubutu wake wa kutaka vyama vyote vya siasa vinavyopata ruzuku serikalini vikaguliwe na kusisitiza kwamba havijakaguliwa, uliongeza kasi ya kuonekana msaliti wa upinzani na kwa chama chake (Chadema). Akawa adui mkubwa wa wapinzani. CCM nayo ikazidi kumuona mnoko, adui, ukaguzi-ukaguzi nini?

RAFIKI

Zitto ni rafiki wanamageuzi, wanaoamini
katika fikra huru za kisiasa. Wanaopenda siasa za mawazo huria pasipo kubanwa na vyama. Hii ndiyo sababu wale wanaoonekana vimbelembele, kuongeaongea, kuzozazoza bila kukistahi chama chao cha CCM, kama Deo Filikunjombe, Kangi Lugora na wengineo, ni marafiki hasa wa Zitto.

Anne Kilango Malecela (CCM), aliwahi kuniambia kuwa anampenda na kumwamini sana Zitto kwa sababu ni mwanasiasa mwelewa asiye na katikati. Kilango: “Kama Zitto anaona kitu hakipo sawa, atasimamia hivyo mpaka mwisho.”
January Makamba aliwahi kumzungumzia Zitto: “Ni mwanasiasa ambaye sitapata shida kufanya naye kazi kwa sababu anapenda ushirikiano. Anapokuwa na hoja yake, huzungumza na wabunge wa vyama vyote bila kubagua, ndiyo maana mara nyingi hoja zake huungwa mkono na wengi.”

Kwa wanamageuzi, Zitto amekuwa kielelezo cha uswahiba naye kutokana na kumbukumbu ya alichokifanya katika skendo ya Buzwagi, saini za kumng’oa Waziri Mkuu, Tegeta Escrow na kadhalika.

Ni hao ambao wamekuwa wakijiuliza, kama Zitto ni mamluki, mbona ni yeye ambaye amekuwa mstari wa mbele kuanzisha hoja nzito za kuitikisa Serikali? Hata katika Tegeta Escrow, naye alitajwa kupokea mgawo, swali: Ni mtu gani anayeweza kula rushwa halafu akamuumbua aliyempa?

KIPENZI

Zitto ni kipenzi cha wasanii hasa wanamuziki wa kizazi kipya. Ndiye mwanasiasa ambaye jina lake linasikika kwenye nyimbo nyingi, kuliko mwingine yeyote. Vilevile watoto wa shule na vijana vyuoni, wanampenda na kumchukulia kama kioo cha maisha yao yajayo, kwa wale wanaoota kuwa wanasiasa.

Mpango wake wa kupigania haki za wasanii na kufanikisha kuzifanya kazi za sanaa kuwa biashara rasmi inayotambulika serikalini, iliongeza chachu kwa wasanii kumpenda, ingawa hata kabla, alikuwa kipenzi chao.

Haiba yake, ndiyo sababu ya wanamuziki Bwana Misosi, Ben Pol, Jay More, Roma, Kala Jeremiah na wengine wengi kumuimba katika nyimbo zao.

Mradi aliouanzisha wa Kigoma All Stars “Leka Dutigite”, kusaidia wanamuziki wa Mkoa wa Kigoma kujiunda pamoja kama kampuni na wote kuunganishwa kwenye Shirika la Hifadhi ya Jamii la NSSF, hivyo kuwezesha kupata bima ya afya, ni pointi nyingine iliyofanya wasanii wampende zaidi.

Ukiwa bungeni, utajionea jinsi watoto wanavyompenda Zitto. Wanapokwenda bungeni kwa ajili ya ziara ya kujifunza (study tour), wanapomuona Zitto huchanganyikiwa. Humkumbilia, kumkumbatia na kupiga naye picha. Wanampenda! Ni kipenzi chao!

By Luqman Maloto



Kwenye uadui umeongopa na umekuja kaa malengo ya kumsafisha.

Baada ya ya ZITTO kuunga mkono PENDEKEZO la CHENGE makinda alipitisha lile azimio, then ZITTO aka pendekeza kuwa kwa hayo mambo saba yaliyobakia nayo yaachiwe mamlaka zilizo wateua, makinda nae akauliza wabunge nayo yakapitishwa. Makinda akashtuka kaingia mtegoni kwakuwa PINDA alikuwa na mamlaka mbili zilizo mteua YAAN BUNGE NA RAISI, then makinda akataka yapitishwe mojamoja hapo ndipo wenje akashtuka nakuhoji yashapitishwa, MBOWE nae ndo akasimama nakutoa maoni na bunge likavunjika kwa siku ile na kuhairishwa.


#USI TULETEE UONGO HAPA. ZITTO aliungwa mkono na yeye alikiri na hata kesho yake maridhiano ya nje kule kabla ya kikao cha bunge kuanza alipewa support na kambi ya upinzani so what kind of hell do u want to tell us?
 
Porojo ni nizilezile za kila cku,hakuna jipya hata moja.
 
Unajisumbua bure tu na udaku wako hapa.
Kwa taarifa yako ni kwamba hakuna mwana-ccm au mwana-chadema ambae ashawahi kumkabili Zitto kwa tuhuma uchwara km hzo akashinda.
"Sijawahi kushindwa vita yoyote ya kulinda reputation yangu"...

Hayo unaoona we leo ni maswali ashayajibu, akaenda mbali zaidi kuita vyombo vya uchunguzi na kamata za maadili zimchunguze. Juzi ngeleja aliporopoka ameitaka Sekretariat ya maadili imuite kumhoji km kutakua na tuhuma zimazomhusu na atazitolea maelezo.

Sio bure, una agenda yako ya siri.
Hiyo lugha ya kutaka kuchunguzwa,au mwenye ushahidi aulete, ni lugha ya kifisadi.
Zitto ajitokeze hadharani, aeleze mambo yote hadharani, aorodheshe mali na majumba yake, atueleze biashara alizofanya mpaka akamiliki mali na nyumba hizo na kodi alizolipa.
Vinginevyo akae kimya.
Mwigulu Nchemba, rafiki yake Zitto ametueleza hapo juu kuwa daima tutawaliwe na akili kubwa, kama yeye anavyotaliwa na akili kubwa ya Wakuu wa CCM.
Inaingia akilini?
 
ukumbuke PIA yeye ndiye aliyetembea maeno mengi na Dr. Slaa kama mgombea uraisi akimpigia kampeni kuliko mbuge yeyote CDM

😀😀😀 yaani Zitto alimpigia Dk.Slaa kampeni!! Acheni utani nyie....mtu aliyepewa kuwanadi wabunge wa chadema mkoa wa Kigoma na akaishia kuwauza wagonbea wa CDM?!! Zitto aliuwauza vijana wa CDM waziwazi...
 
BY SHEILA MBAGA Sheila Mbaga is offline
Sheila Mbaga

Join Date : 27th February 2015

Default Re: Taarifa sahihi kuhusu ulinzi wa Dk. WillibrodSlaa dhidi ya upotoshwaji unaoenezwa

[h=1]Ukweli wa Mauaaji haya hapa: Membe, Gotham na Ridhiwani wahusishwa [/h]
Ni kwa kipindi chamuda mrefu kumekuwepo na kikundi kinachoratibu mauaji ya watu mbali mbali. hayatunayoyasikia kwa Dr. Slaa siyo mageni masikioni mwetu bali ni muendelezo wakile kinachoratibiwa na kundi hilo. Ni wazi kuna mipango yaliyoanza kutekelezwakwa baadhi ya wana CCM na baadhi wa wapinzani, leo hii naomba niwatelee ukweliwa haya mauaji yote na mipango ya kuuwa watu wengine....

1. Mjumbe wa NecLudewa: Huyu ndiyo alikuwa mhanga wa kwanza katika mauaji ya hivi karibuni,mjumbe huyu wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM, aliwekewa sumu katika kikao chaNEC kilichofanyika mwezi wa 11 mwaka jana katika mji wa Dodoma, bila kupepesamacho uratibu wa kumwekea sumu uliratibiwa na bwana moja anayejulikana kwa jinala Jack Gotham, ambaye ni kada wa Chama cha Mapinduzi.

2. Mjumbe wa Nec waCCM kutoka Kahama: Huyu ni mjumbe wa NEC wa chama cha mapinduzi kutoka wilayaya Kahama, ambaye ni mdogo wake waziri Marry Nagu, naye ni muanga wa kuwekewasumu, ambapo aliwekewa sumu katika kikao hicho hicho kilichoketi Dodomamwishoni mwa mwaka jana.

3. BeatriceShelukindo: Huyu ni mbunge wa Kilindi kupitia chama cha mapinduzi, na ni mjumbea halmashauri kuu ya Taifa kupitia wilaya ya kilindi, ni kwa muda mrefu sanaMama Beatrice amekuwa akiugua na kutibiwa India. Beatrice aliwekewa sumubungeni na wahusika hawahawa ambao nitawataja hapa chini. kama unakumbukaBeatrice Shelukindo alikuwa moja wa wabunge waliokuwa wakali sana kuhusu swalala Richmond ila baadaye alipogundua ukweli akaamua kuwakimbia na kusimama katikaukweli. Ni jambo la kumshukuru Mungu ya kwamba kwa sasa Beatrice yuko nchini naanaendelea vizuri baada ya juhudi kubwa za madaktari wa India kuweza kuondoasumu aliyowekewa.

4. Kapteni Komba:Komba amekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi na mjumbe wa NEC kupitia Nyasa, baadaya mazishi yake yaliyofanyika wiki iliyopita sasa ni wazi kilichomuuwakimejulikana. Komba aliwekewa sumu na hao hao wahusika sababu kubwa sikiwambili, mosi ni ahadi aliyopewa Stella Manyanya kuhusu jimbo husika na pili niwazi Komba alikuwa instrumental katika siasa za Edward Lowassa ambaye anawatoaroho huko CCM katika kinyanganyiro chao cha uchaguzi wa ndani. Ni Komba sikuchache kabla ya kuwekewa sumu alisema wazi wazi kwamba anamuunga mkono Lowassakuwa mgombea wa chama cha mapinduzi.

5. Salum Awadh: Huyualikuwa ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi, kifo chakehakikupishana na cha Komba, pamoja na sifa zote ila alikuwa na sifa moja kubwaambayo ni ujasiri, Ni Awadh aliyediriki kusema mbele ya Mkt Jakaya kwamba kamani kosa la maadili basi wagombea wote ndani ya CCM wana kosa hilo la maadili nasiyo wachache kama tunavyoaminishwa, pili ni Awadh aliyetoa hoja binasfi ndaniya kamati kuu kwamba Nape Nyauye ambaye ni mwenezi wa chama afukuzwe ndani yachama na anyanganywe kadi yake mara moja kwa sababu alishakisaliti CCM na kuwamoja wa waanzilishi wa CCJ, vile vile Awadh aliongezea hoja yake kwamba kwasasa Nape yupo kwa ajili ya kukibomoa chama badala ya kukijenga...

Bwana Awadh aliwekewasumu na ndugu Issa Gavu katika ofisi ya Kisiwandui, siku mbili kabla; nduguGavu alifanya kikao cha pamoja katika hoteli ya Serena akiwa na RidhiwaniKikwete na Jack Gotham ambaye ni consultant kwenye mradi wa vitambulisho vyaTaifa {NIDA), na ndiyo meneja kampeni wa Bernard Kamilius Membe..

Gotham mnano tarehe22.04. 2014 alienda Nchini Bulgaria kupata mafunzo ya kuuwa watu kwa njia yasumu na kisha akarudu na sumu aina ya CYNIDE ikiwa ni sumu mahsusi kwa ajili yakumaliza wale wote wanaoona ni kizingiti kwao katika kukamata dola. hii sumu nikwa ajili ya kuwamaliza wale waliovizingiti kwao ndani ya chama chao na nje yachama chao, ndiyo mana leo hii kusikia kuhusu Dr. Slaa kutaka kuuwawa ni swalaambalo ni serious na la ukweli. Katika hili la Dr. Slaa msimamizi mkubwa niMangula ambaye ni makamu mwenyekiti wa chama hicho (kama mlivoona kwenye vyombovya habari vya leo), na ni Membe aliyeenda kusini kumfata Mangula....

Mkakati huu unarudinyuma alivyouwawa kijana moja wa Kinyakyusa kisha wakasema ni ajali ya gari(stori hii ilikuwa reported kwenye vyombo mbali mbali vya habari). Kijana huyualiuwawa baada ya kutoa siri za Home Shopping Centre na Ridhiwani kutoa watuSouth Africa kwa ajili ya kumuuwa Bwana Masamaki ambaye ni kamishna wa Tax TRA.

Huu mchezo wa kuuwawatu haujaanza leo, hawa mabwana walianzisha utaratibu wa kutoa watu SouthAfrica na Kenya kwa kazi hiyo tu. wamefanya hivyo kwa Ulimboka Steven ambapowatu walitolewa Kenya na kushirikiana na Ramadhani Ighodu, wakafanya hivyo kwaAbsolom Kibanda (kama unakumbuka kati ya maadui 11 aliyowataja Membe, KIbandaalikuwa moja wao kama mwandishi)...

Mwaka 2012 RidhiwaniKikwete alichukuwa watu kutoka Kenya kwa ajili ya kufanya kazi maalumna mpakasasa watu hao bado wapo nchini ambapo wamepangishiwa nyumba mitaa ya Masakieneo maarufu kama Kilimanyege karibu na Jacks Bar.... Mauaji haya yamekiwayakisimamiwa na Membe na kuratibiwa na Ridhiwani pamoja na Gotham...

Nina uhakika kwambahaya yanafanyika bila Rais Jakaya kujua, hata hapa idara yetu hakuna wanaojuahili swala zaidi ya watu wa karibu wa Membe. Ridhiwani amekuwa akifanya hayayote na hao washirika wake hata bila baba yake kujua na hii ni kwa sababu dogokashaingizwa kwenye biashara haramu mbalimbali likiwemo na la kuuza madawa yakulevya. Kwa sasa ni wazi hawa watu wanafanya jitiada zozote zile waingiemadarakani ili kulinda dhambi zao, na wanafanya kila jambo ili washindeuchaguzi wa mwaka huu, kwa hali hiyo tutegemee mauaji mengi na makubwa kutokeakuanzia sasa.. Na kwa sasa bila kuwaficha ila nafanya haya kwa neema za Mungukuna mpango wa kuangusha helcopter ya Chadema... hawa watu wamekuwa wakipangakufanya haya mambo na kujadili hali ya siasa katika hoteli zifuatazo 1). Serena2). Protea na 3). Collesium Oysterbay...

Ila kwa wale mabibiwa umri kama wangu watakumbuka kifo cha kutatanisha cha Padre Serapius Kombaambapo Membe wakati huo alihusishwa. Komba aliuugua ugonjwa wa kufa ubongo polepole. Komba alikuwa Gombare wa seminari kuu Peramiho, mwandishi mahiri na mtualiyejaliwa upendo ila kwa unyama wa Membe na ushirika wake na Padre SebastianNepachichi walidiriki kukatisha uhai wa padre Komba... Hata hivyo kifo chabalozi wa Libya aliyeuwawa yasemekana kuna mkono mkubwa wa MEMBE..... Membe nimtu hatari sana na kama Taifa tusikubali kurudi kwenye zama za mauaji yakikatili....

Asanteni
Mtoto Sheila.....

like

Pasco, ocampo four and jme like this.
 
Kwanza si kweli kuwa nguvu ya Zitto ndio iliyojenga chama. Si kweli hata kidogo. Zitto amejengwa na chama na kufanywa maarufu na chama, kisha kiburi cha sifa kimemwingia.

Pili, inadhihirisha dhana ya usaliti. Zitto akiwa ndani ya CHADEMA, alipaswa kuainisha changamoto za chama na kujaribu kuzitatua katika timu iliyopo, na si kudhani kuwa AKILI YAKE ndio itajenga chama. Hii imedhihirika sasa. Baada ya yeye na vibaraka wenzake kama Juliana Shonza kuondoka CHADEMA, chama kimekuwa imara zaidi. Chama kimekuwa hakina migogoro kabisa. Chama kimejengeka zaidi na watu wana imani zaidi na chama.

Tatu, kama kweli uongozi wa Zitto ndicho kilichokuwa kinahitajika kukuza chama, Zitto ana nafasi katika chama chake kipya cha ACT-Tanzania. Zitto atoke CHADEMA, tuone kama ACT-Tanzania itakua kama anavyoota.

Nne, wewe kama mwana CCM ambaye una hakika kuwa Zitto ni hazina, kwa nini haushauri viongozi wa chama chako wamchukue Zitto na kumfanya kiongozi ndani ya CCM ili mumkomboe Mtanzania kwa kubadili fikra za kifisadi na za ulevi wa madaraka zilizo CCM na zenye madhara makubwa kwetu sisi kwa kuwa ndio wanaogawa rasilimali za Taifa?

Tano, unathibitisha kuwa kazi ya Zitto ndani ya CHADEMA ilikuwa kutengeneza makundi ya kumjenga yeye mwenyewe. "I have a fear of being ruled by a lesser" hii ni kauli isiyokilenga chama, ni ya kibinafsi. Ni mtu anayetafuta yeye madaraka, tena asiye na subira. Bora chama kivurugike kwa sababu ni yeye tu anayedhani anaweza. Kauli hii inadhihirisha kuwa mtu huyu anajitafuta mwenyewe.

Sita, kama ulidhani umeandika uzi huu kumjenga Zitto, hakika unazidi kumchafua.

Mwisho, jifunze kiingereza. I didn't find him, he finds me hii inadhihirisha kuwa bado unahitaji kujifunza si kiingereza tu, na mengine mengi...

huna hoja then wewe ni mjinga. kuliko unavyozani maana ubongo wako siyo huru.
 
Naomba niseme binafsi nakerwa na baadhi ya wanao jifanya wapenda maendeleo kumbe wapuuzi tu wanaotumika kila siku kuwakatisha tamaa watu wanaoonekana wasi kupambana na wala rushwa wa nchi hii.

Kwa hili sio tu maccm hata wanachadema wenzangu baadi wamekuwa wapuuzi kupita kiasi. Zitto Kabwe ni binadamu kama binadamu wengine anamapungufu kama wengine ila ni mbunge aliyejitoa kupigania watanzania Kwa vitendo na kazi anazozifanya zinaonekana kuliko hao wengine tunaowadhania.

Cha kushangaza amekuwa adui wa pande zote upinzani na chama tawala, mafisadi wameumbuliwa wanatumia mgongo wa Zitto kujisafisha ila cha kushangaza wapuuzi humu ndani mnaendelea kushadadi ambapo mnaona afadhali Ngeleja asiwajibishwe ila Zitto aaibike pasipo uhalisia.

Jamani kila tuhuma zidi ya Zitto kashazitolea ufafanuzi kufikia hatua isiwe maneno yake akasema tume ya maadili imchunguze na akikutwa tuhuma awajibishwe. sasa nyie mnataka nini?

Kila baya Zitto, hata kila anayejifunza propaganda anajifunzia Kwa Zitto. Zitto anakuwa mbaya kuliko CCM na kina Chenge kwenye tuhuma zisizo na ushahidi, huu ni upuuzi.

Ni hayo wakutukana atukane tu ila ajijue yeye hajielewi ila anayejielewa atanielewa.
 
Mti wenye matunda ... mawe!!!!!!

Na naona wengi wanataka wajifunze kuangua na kujenga hoja za kuungwa.
 
huna hoja then wewe ni mjinga. kuliko unavyozani maana ubongo wako siyo huru.
Ningependa unijibu kwa hoja na si kwa matusi.

Onyesha ujinga wangu kwa kuleta hoja kinzani na hoja zangu. Hoja hizi hapa.
Kwanza si kweli kuwa nguvu ya Zitto ndio iliyojenga chama. Si kweli hata kidogo. Zitto amejengwa na chama na kufanywa maarufu na chama, kisha kiburi cha sifa kimemwingia.

Pili, inadhihirisha dhana ya usaliti. Zitto akiwa ndani ya CHADEMA, alipaswa kuainisha changamoto za chama na kujaribu kuzitatua katika timu iliyopo, na si kudhani kuwa AKILI YAKE ndio itajenga chama. Hii imedhihirika sasa. Baada ya yeye na vibaraka wenzake kama Juliana Shonza kuondoka CHADEMA, chama kimekuwa imara zaidi. Chama kimekuwa hakina migogoro kabisa. Chama kimejengeka zaidi na watu wana imani zaidi na chama.

Tatu, kama kweli uongozi wa Zitto ndicho kilichokuwa kinahitajika kukuza chama, Zitto ana nafasi katika chama chake kipya cha ACT-Tanzania. Zitto atoke CHADEMA, aingie chama chake alichokianzisha, akijenge kwa nguvu hizo hizo anazodai kuwa amezitumia kujenga CHADEMA, tena kwa hiyo "akili KUBWA" inayompa kiburi, tuone kama ACT-Tanzania itakua kama anavyoota.

Nne, wewe kama mwana CCM ambaye una hakika kuwa Zitto ni hazina, kwa nini haushauri viongozi wa chama chako wamchukue Zitto na kumfanya kiongozi ndani ya CCM ili mumkomboe Mtanzania kwa kubadili fikra za kifisadi na za ulevi wa madaraka zilizo CCM na zenye madhara makubwa kwetu sisi kwa kuwa ndio wanaogawa rasilimali za Taifa?

Tano, unathibitisha kuwa kazi ya Zitto ndani ya CHADEMA ilikuwa kutengeneza makundi ya kumjenga yeye mwenyewe. "I have a fear of being ruled by a lesser" hii ni kauli isiyokilenga chama, ni ya kibinafsi. Ni mtu anayetafuta yeye madaraka, tena asiye na subira. Bora chama kivurugike kwa sababu ni yeye tu anayedhani anaweza. Kauli hii inadhihirisha kuwa mtu huyu anajitafuta mwenyewe.

Sita, kama ulidhani umeandika uzi huu kumjenga Zitto, hakika unazidi kumchafua.

Mwisho, jifunze kiingereza. I didn't find him, he finds me hii inadhihirisha kuwa bado unahitaji kujifunza si kiingereza tu, na mengine mengi...
 
Wewe umeshachoka? Mkuu mayange,tumeumbwa kuona na kusema.Kuchoka ni kutokwa na uhai. Ukiona tunakukera usitufuatilie
 
Last edited by a moderator:
CC
Mwalimu Kaijage "he find me, i didn't finds him" lol haya mavingereza bhana
 
Back
Top Bottom