Zitto Kabwe: Adui, Rafiki, Kipenzi


Ashasema hana biashara yeyete nje au ndan ya nchi hii. Hapa dar anaishi nyumba ya kupanga kule tabata. Nadhan ya NHC/NSSF.

Kuhusu magari ya kifahari na majumba kama unavosema anamiliki, alishatoa fursa kwa walio na ushahidi. kwahiyo we mwenzetu kwakua una ushahidi, uweke hapa ili kukata mzizi wa fitna. Vinginevyo, ni muendelezo wa hekaya zile zile tulizozizoea.

Hadi asilia (Natural justice) Inasema you can be judge of your own case. Kwa maana kwamba Zitto hawezi kujichunguza mwenyewe. Kwa msingi huo ametoa fursa kwa vyombo na taasisi husika kufanya kazi yao...to avoid biase as it is inherent.

We leo unatwambia kuchunguzwa na chombo kingine ni kauli za kifisadi...are you serious?? Kwahyo Tibaijuka, chenge,.Ngereja na genge lao walipaswa kujichunguza wenyewe?

Je tungepata kujua ukweli hadi leo?

Think it again
 
Uhuru wa kutoa maoni unaruhusu watu waseme kwa uhuru juu ya viongozi wao.

Zitto is a public figure, na anafanya kazi za umma. Kuna watu watamsifu na kuna watu watamtoa kasoro.

Niambie kiongozi gani ambaye anasifiwa tu?
 
March ndio hii,afanye maamuzi magumu asepe,kuna vijana wengi wamekuwa groomed,zamani nilidhani ni charismatic leader,niligundua I was wrong,hana mvuto kumfikia Salim Mwalimu ama vijana wengine waliochipukia.Aende zake his time his over.Subiri bunge la 2016 uone vijana kibao watakaoingia kupitia CHADEMA watakavyowapandisha pressure wabunge wachache wa vyama vya upinzani wakati huo [ CCM,TLP na ACT]
 
Kiukweli Zitto ni mwanamapinduzi sikuwahi penda siasa huyu jamaa ndio kanifanya nipende siasa
 

Yaani kwa matatizo yote ya akina Chenge na escrow na CCM bado akili zako zinakutuma umtaje au kumuongelea zitto!!

1. kwanza amekutawala, ndio maana at this point of time, umeingia kwenye kundi lile lile la wanaosema na hawasikilizwi jamii inakupuuza watakaokuunga mkono ni hao hao wachache

2. leta hizo document za Brela, pia useme ni wakati gani kiongozi wa umma anatakiwa kuwa na kampuni na wakati gani hatakiwi! na piga picha kubwa kwa watanzania wote, unaweza ukawa unazungumza kitu unaonekana mshamba; uongozi wa zitto ni wa kudumu??

3. nieleze kiburi cha zitto cha kuibua uchafu huo wote anaousema kila siku anautoa wapi?? ni swali ninalojiuliza kila siku

4. ulichosema unaonyesha zitto ana makosa, mbona wabunge, serikali, na wananchi wote wako kimya ( kunani?) hata maadui zake kisiasa wako kimya? na wewe thread yako itapita tu kama juzi ( dont you have an extra plan to at least go far than just writing???) unaonekana kituko na umeandika so innocently but so low! very low

tuanze kazi sasa, leta hizo document za Brela ukizipata ni PM

Then uliza kwa wataalamu wa sheria uhalali au usio uhalali unaweza ukawa unachekesha ( nimerudia hapa)

Huyu zitto anawasumbua sana
 
...............We leo unatwambia kuchunguzwa na chombo kingine ni kauli za kifisadi...are you serious?? Kwahyo Tibaijuka, chenge,.Ngereja na genge lao walipaswa kujichunguza wenyewe?

Je tungepata kujua ukweli hadi leo?

Think it again
Prof. Anna Tibaijuka, Chenge, Ngeleja na wenzao hawakutajwa wala kugunduliwa na hivyo "vyombo vya uchunguzi".
Walitajwana vyombo vya habari vyenye ujasiri.
Ndiyo maana mpaka sasa hivyo vyombo vya uchunguzi unavyovisema wewe na Zitto, havijagundua majina ya mafisadi wa Escrow kupitia Stanbik.
Think it again
 
Jakaya Mrisho Kikwete ni mtu mwenye roho nzuri sana. Lakini bwana huyu ni kiongozi mbaya sana - ana mapungufu mengi sana kiuongozi na kwahahikika hana sifa za uongozi. He lacks leadership charisma, talent, skills and qualities.

Zito Kabwe on the other hand, is the oposite of Mr Kikwete. He has leadership charisma, talent, skills and qualities - BUT he is not a good person perse'. Ana tamaa sana, ubinafsi uliopitiliza, umimi, masifa, majivuno na majigambo - sifa hizi zote (ambazo origin yake ni ukigoma) pamoja anapokuwa nazo mtu mmoja it is a leathal combination. Sifa mbaya za Zitto Kabwe zinafunika kabisa uwezo wake wa kiuongozi na ndizo zitakuja kusababisha anguko kuu la Bwana Zitto Kabwe. Mark my word!

Matatizo mengine ya Zitto

Ana pupa na papara zinazomfanya ashindwe kuelewa principal za msingi sana kwenye maisha. Principal hizo ni pamoja na ile ya Timming is everything.

Hakuna kitu muhimu kama kuelewa umuhimu wa timming especialy kwenye uongozi na siasa. Ukishindwa kuelewa hili always utakuwa unateleza kisha unaanguka. Nyerere aliwahi kujiuzulu uongozi na kumuachia Kawawa for a while ili kuweka mambo sawa - timming. Nyerere aling'atuka mwaka 1985 kwa hiyari yake kwakuelewa the essence of time.

Principal ingine ya msingi ni ukweli kuwa life is all about choices and decisions. Zitto ana tendance ya kufanya wrong choices at a right time au right choices at a wrong time - big mistake.

Katika uwanja wa polical calculations, Zitto amefeli and he will always fail because mapungufu yake ya kibinadamu yanafunika sana sana sifa zake za uongozi na kwakuwa yeye haambiliki na aamini kuwa anajua sana basi hakuna lingine la kufamnya bali kumuangalia anavyoanguka kama ajali ya train - train wreck. Ukiangalia sana matendo ya Zitto utagundua kuwa - anaamini kuwa yeye ana akili na uwezo mkubwa kiuongozi kuliko mtu yeyeto ndani ya Bunge, Chadema na Tanzania. Akiwa hajatimiza miaka 40 Zitto anaamini kuwa Tanzania nzima ni yeye tu ndio anafaa kuwa Rais na kwaongoza watanzania wengine wote - haamni vinginevyo. Pia anaamini kuwa Chadema nzima ni yeye tu ndio mwenye uwezo mkubwa kuliko kila mtu na hivyo anatakiwa kuongoza kila mtu. Kijana huyu ana upofu wa akili na maono.
 
The guy is talented...kwa anayoyafanya kwa tanzania ya sasa hakuna mwanasiasa wa upinzan anayewez kufanya....put evidence nasio siasa zile zile za kuzushiana....zitto ni mpiganaji na haitaji akili za ziada kujua hilo....ameifanyia mengi tanzania yetu...swala je hao unaowaabudu wameifanyia nin tanzania zaidi ya kuvuruga amani ya nchi....niwakat sasa wa kuamini mtu nasi chama tena....
 

HAHAH HATA FaizaFoxy amemuonesha ZITTO kama adui. Adui wa kina FaizaFoxy.
 
Last edited by a moderator:
Ni mara nyingi sana huwa nawaambia vijana masikini wenye limited resources.Ni njia mbaya sana kutumia akiba ndogo kuwekeza ktk viwanja vya matajiri ili kujenga jina halafu baadae wategemee kupata dili.

Wengi sana huishia kupata mfadhaiko mkubwa ktk maisha.Kwani huw ani shida sana kukubalika na hao ktk makundi.

Vijana hao huwa hawajui sana kuwa matajiri walifika hapo kwa kuthamini hela ndogo.Na si wepesi sana kuwapa dili(kuwekeza mali) kwa wabadhirifu.

Huwa nawashauri sana vijana kuwekeza hicho kidogo ktk mradi fulani, na huo mradi aupiganie kwa juhudi kubwa sana.Juhudi,ubinifu uwajibikaji na mafanikio ndio yatamkutanisha na hao matajiri,na utamfikisha akiwa na heshima.

Atafika kwa matajiri kumuona kuwa mtu sahihi wa kuwekeza mali kwa usalama.Zitto kajilazimisha kuingia ktk kundi la waliofanikiwa bila kujifunza Vitu fulani ambavyo vingemsaidia sana kujitathmini km kweli amefikia na kustahili alipokuwa kasimama.
 
Mtoa post unatupotosha,aliyestukia dili.hakuwa Mbowe,alikuwa ni Christopher Ole Sendeka.Ndo alisimama na kupinga pendekezo wala sio Mbowe.Baada ya Sendeka kupinga ndo Zitto akasema akili.yake imechoka
 
Juzi wakati anahojiwa na vyombo vya habari kuhusu kufukuzwa kwake uanachama wa Chadema,pamoja na mambo mengine aliyoeleza pale,moja ni hili la kujigamba kwamba namnukuu;"kazi nnazofanya mimi(zitto) siwezi kulinganishwa na mbunge yeyote yule". Kwa mtazamo wangu finyu,hili ni tusi kwa wabunge wote! Yaani mh. Zitto anafanyakazi zaidi kuliko wote!? Haya ni majigambo yaliyopitiliza.

Kuna mbunge mmoja nilikuwa naongea nae jana ambae pia ni mjumbe wa PAC anasema,zitto inahitaji roho ya chuma kumvumilia ni mtu ambae kila kitu anachofikiria yeye anataka kiwe hivyo. Me namshauri zitto,kwa vile Kitila Mkumbo kitaaluma ni mwanasaikolojia na ni rafiki yake ampe tiba ya tatizo hilo la kujiona yeye ni bora kuliko wengine. Nawasilisha!
 
Last edited by a moderator:
Mmeshamfukuza mbona bado mnaendelea kufuatilia mwacheni aendelee na maisha yake au ndo mwendelezo wa siasa za maji taka
 
Ana matatizo sana yule jamaa, sijui labda tutumie msemo wa wahenga, Akikua ataacha" Lakini ashakua tayari 39yrs si mchezo labda na useja ndio unamsumbua. Unajua umri huo kutokuwa na mke ni mapungufu makubwa sana katika kujitambua. Ebu tumuache maana wakati ukuta.
 
zitto ni adui wa wasaka tonge wa upinzani

Mimi kma mwananchi wa kawaida naona mchango wake
Hata mimi nilimpenda ila kwa sasa nasema mapema mno kuona anafaa.Kirago alicho kitupa jirani yako usikalie kwanza lazima UKIKUNGUTE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…