Ninachofahamu fika ni kuwa wahalifu waliungana kumkomoa Muhongo. Wapo waliomchukia Muhongo kutokana na kuwazibia ulaji (Mkono et al), wapo waliomchukia Muhongo kwa kuwazuia wasihodhi utajiri wa mali asilia ambayo ni kwa manufaa ya wote (Mengi et al), wapo waliotaka kumkomoa Muhongo kwa kuwaeleza ukweli wao juu ya uwezo na uelewa wao mdogo kuhusu sekta ya madini na gas (Zito, Olesendeka et al.), na pia wapo waliofanya kazi ya kumwondoa Muhongo katika nafasi yake ili biashara zao ziweze kuendelea vizuri (Zito, Olesendeka et al.), wapo waliofanya kazi ya kumwondoa Muhongo kwaajili ya faida za kisiasa (wengi wa wabunge wa upinzani), wapo waliofanya kwa nia ya kumkomoa Kikwete (baadhi ya wabunge wa CCM), na wapo waliofanya jitihada ya kumwondoa Muhongo ili wapate nafasi za uwaziri (Filikunjombe et al.), mwisho kabisa tupo tulioshabikia bila kuwa na msingi wowote ule.
Ukiona una nchi ambayo waovu wanaweza kuungana kutimiza malengo yao na wakafanikiwa kuwa na viongozi wanaowataka, kuwaondoa viongozi wasiowataka; na umma ukachezeshwa mchakamchaka kuunga mkono matakwa binafsi ya waovu, Taifa la namna hiyo lipo kwenye hatari ya kushindwa kabisa kulinda maslahi ya walio wengi, na watu wengi hawawezi kuwa tumaini la uhakika kuwa siku moja maslahi yao yatakuwa mbele kuliko ya watu wachache.
Hela yoyote ambayo inatolewa kwa Mwenyekiti wa PAC au mjumbe kutoka Mashirika ya umma, inatafsiriwa kuwa ni rushwa mpaka pale kutakapotolewa maelezo ya kina kwa nini hiyo pesa ilitolewa, na je Zito ali-declaire kuwa amepokea hela kutoka kwenye taasisi ambayo anaisimamia? La sivyo, bila shaka yoyote Zito na taasisi iliyotoa, wote wana hatia.