Zitto azomewa Bukoba

Zitto azomewa Bukoba

Nikiwa hapa Bukoba leo nimehudhuria mkutano wa ACT Wazalendo katika uwanja wa Mashujaa. Kiongozi mkuu wa chama hicho,niko Zitto Kabwe alikuwa akihutubia.
Awali alianza kueleza sababu za kuondoka Chadema, akisema sio kosa kubadilisha jukwaa la siasa. watu walikuwa wakimpigia makofi tu.
Lakini hali ya mkutano ilibadilika na kuwa mbaya pale alipoanza kujisifu kuwa yeye ndiye aliyeagiza hesabu za Chadema zikaguliwe na CAG, kisha akaitwa msaliti na kamati kuu ya Chadema.
Hapo wananchi waliokuwa uwanjani hapo wakaanza kupiga kelele wakisema 'sio kweli, sio kweli, sio kweli".
Ilibidi Zitto abadilishe mahubiri na kuanza kueleza msimamo wa chama chake. Lakini watu wakawa hawamsikilizi tena. Wengine walisikika wakisema, "kama umekuja hapa eleza ya chama chako, ya Chadema uyaache,".
Kama hiyo haitoshi, Zitto akaanza tena majigambo akisema eti alipokuwa bungeni aliiangusha serikali mara tatu, "Hao wanaokuja kunitukana waseme wamefanya nini bungeni" alisema Zitto.
Watu waliendelea kuzomea hadi Zitto akasema, "Kama hamtaki kunisikiliza naondoka zangu,". Watu wakajibu,waliendelea kuzomea " Nendaaa...!
Hata hivyo mkutano umeisha salama.
Kwa kweli Zitto ana kazi ngumu kuijenga ACT?

Naona povu linakutoka mno. Let us use our freedom of speech properly. Unapata kiasi gani unapoleta umbea wa walevi hapa.
 
Wewe ningekuwa admin ningekutoa humu jf..
Hicho sio kikao cha chama mpaka wawepo Act peke take

Wabakuja watu mbalimbali kusikilixa Sera ya chama
kwa akili yako ndo maana hukuwa adm....
sasa kama lengo ni kusikiliza sera kwa nini usimpuuze akiongea mengine we ukazingatia sera tu
 
watu mnavyo viwanda vya uongo balaa. nawewe unatofauti gani na mafisadi. mimi nilikuwepo mbona hilo sikuliona? wewe tu ndio ulikuwa kwenye huo mkutano?. ukweli ni kwamba mkutano wa zotto leo ulifana na haijawahi pata tokea. kijana anakipawa kikubwa cha kupenda.

"zotto" ndo nani mkuu?
 
Hapa makere act tumewapuuza wanafanya siasa za udini ni kundi la watu 8 kiongozi wao ni shabani na masudi.
 
Zitto sio kumzomea, anaitaji kipigo. Wazalendo mkimuona msaliti mpigeni maana kuzomewa kazoea.
 
Je kwenye wasifu wake ana tabia ya kupokea ushauri au yake ndio anaona yako sahihi?...Hayo yote amejitakia mwenyew
Hata Profesa Baregu alisema Zitto ni mtu asiyetaka ushauri. Yeye huamini alichokisema ndo kiko sahihi. Hiyo ni ishara ya ubinafsi
 
Back
Top Bottom