Chakochangu
JF-Expert Member
- Mar 21, 2011
- 2,668
- 2,174
Mkuu kuna watu hawaelewi tunaongelea nini wao wanadhani ni ubishani wa nani zaidi?
Hakuna jambo baya kama wewe ni mtumishi wa umma na unayeheshimiwa na jamii na unaona unafanya yakupasayo kwa mujibu wa sheria na kanuni halafu unafedheheshwa hadharani na mtu mmoja mwenye madaraka lakini kwa vile hapingwi basi wewe na wenzako mnabaki kusononeka tuu.
Kwanza tabia hiyo inawapunguzia weledi na hamu ya kutumikia taifa kwa nguvu zote,, inakuwa kama mnatumikia adhabu na sio kutumikia nchi.
Mimi kuna kitu fulani nakisubiri kwa hamu kubwa.
Kuna kitu au jambo lisilotarajiwa kwa watu wengi litatokea katika Bunge letu ,
kama sio katika kikao hiki basi ni katika vikao viwili vijavyo either cha APRIL au kile cha bajeti JUNI /JULAI.
Na vilevile katika Baraza la Mawaziri ni hivyo hivyo.
Muda utatuambia.