Acheni kudanganya umma. Zitto siku zote amekuwa akiamini katika ushirikiano wa wapinzani. Hata kabla ya uchaguzi wa 2005 yeye alikuwa mstari wa mbele kutika mikakati ya ushirikiano ambayo kama si umimi wa baadhi ya watu basi CUF, NCCR na CHADEMA wangeliweza kushirikiana na kusimamisha mgombea mmoja katika urais na kuachiana majimbo mengi tu.
Omar,
Watu gani hao? Na ubinafsi upi huo? Mimi ninachokumbuka ni maandishi ya Zitto mwenyewe humu JF kuwa NCCR ni chama kilichokufa na kwamba chama hicho mwaka 2005 kilifadhiliwa na mafisadi kwa fedha za EPA. Kwa hiyo hadithi ya kuwa Zitto alitaka ushirikiano na NCCR ndio naisikia kwako.
Pia Zitto wakati wote amekuwa karibu na wanasiasa wengine hata wale wa CCM ambao hata kama alikuwa hakubaliani nao lakini pia haamini katika siasa za uadui. Waulize viongozi wa vyama vingine vya upinzani ni nani wanamuona muumini wa dhati wa ushirikiano ndani ya CHADEMA na watakutajia Zitto.
Omar, Zitto kuwa karibu na Mrema na Mbatia akashindwa kuwa karibu na Mbowe sio sifa wala sio ishara ya kutanguliza utaifa. Ndio maana watu wanashangaa kwamba baada ya matukio ya Tarime yaliyofanywa na Mrema na Mbatia, na matukio ya Mrema dhidi ya Mutungirehi Zitto akawa mwanasiasa pekee wa CHADEMA aliyekwenda Mkutano Mkuu wa TLP na kuchangia dola mia. Siku ambayo kulikuwa na mkutano wa CHADEMA hakuuchangia wala kuhudhuria pamoja na kuombwa. Maneno kama haya yanapotolewa na wewe ambaye umetajwa humu na Zitto mwenyewe kuwa ni msaidizi wa Salim na umetajwa kuwa ni msaidizi wa Zitto ni vyema ukatueleza zaidi
Ndio maana sishangai unavyosifia Zitto kuingiliana na wanasiasa wa vyama vingine ikiwemo CCM. Kama msaidizi wake ni msaidizi pia wa Dr Salim wa CCM si jambo la ajabu. Lakini wapo wanajiuliza pia mbona kila Zitto anapoulizwa role models wake hutaja orodha ndefu ya wazee wa CCM? Hivi wazee kama Mtei, Makani nk wa CHADEMA hawaoni kuwa na maana yoyote?
Hata wakati bado hajajitoa katika kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA moja ya ajenda yake kubwa aliyokuwa akitaja hata katika vyombo vya habari ni kujenga mazingira mazuri ya ushirikiano wa dhati wa vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi ujao.
Kwa hiyo kwake mazingira ni CHADEMA kushirikiana na NCCR na TLP? Hebu tueleze vizuri faida ya huo mkakati, na kwanini mkakati huo haukuanzia Tarime, Busanda na Biharamulo? Vyama hivyo vimejiandaaje kwenda 2010 ili iwe sababu ya CHADEMA kuviachia majimbo kama ambavyo huo mkakati ulioita wa Zitto na ajenda uliyoitaja inavyosema?
Tatizo katika upinzani bado wengi wao wamegubikwa na umimi, usisi, falsafa pinga na kujidanganya kuwa wanaweza pekee yao wakati realities says otherwise.
Wapo hata wanaofikia kudefine muingiliano wa Zitto na wanasiasa wa vyama vingine kuwa ni usaliti na sio mkakati chanya.
Tafuteni majungu mengine lakini katika hili Zitto ameonyesha muono mpana wa suala zima la maendeleo ya demokrasia nchini mwenu katika mtazamo wa mbali kuliko wanasiasa wengine.
Wapinzani gani hao wamegubikwa na umimi? wataje kwa majina na umimi wao ili tuujadili. Lakini usiandike hoja za kuchokoza zenye kumuingiza Zitto kwenye malumbano humu
omarilyas