Kama mfumo wote wa vyama vya upinzani ungekuwa na mtazamo kama wa Zitto, hata mimi ningejiunga na Chama cha Upinzani. Hiki kichwa ni kizuri. Hahangaikii ushindi wa CHADEMA pekee, anahangaikia ushindi wa upinzani, ambao iwapo watakuwa wengi bungeni, watakuwa ni mwiba kwa CCM. Na huu uhuni ambao CCM inawafanyia wananchi utapungua.
Zitto is a true model, I like this guy. Siyo wapinzani wengine ukiwaambia waungane wanang'aka kama nini? Hao wakiingia madarakani hawatatofautiana na CCM. Tuwapige vita watu wasiopenda umoja wa upinzani Tanzania. Binafsi nitajiunga na upinzani iwapo tu nitaona wamekubali kuungana. lakini kwa kelele hizi zisizo na mpangilio, bora tu kubaki CCM.