Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
 
Kweli hukusema CHADEMA kuna udini but kulisema nchi hii ina uchaguzi wa kidini.. Je ni agenda ya chama chako? ni kweli?

Selous,
Mbona mmeamua tu kumzika Zitto alive? Mara mseme amesema Chadema kuna Udini, mara hakusema ila alisema nchi ina chaguzi za kidini. Kama Zitto hakusema Chadema kuna udini na amesengiziwa, basi aombwe radhi kwanza then mlete lawama nyingine.
Jamani, Zitto naye ni binaadamu na ana feelings, mtasababisha aandike mambo ndivyo sivyo ili mpate sababu zaidi ya kumlaumu. Na hii ndio sababu viongozi wengine hawaji JF.
 

I beg to differ mkuu; kuna mambo ambayo ukisema yanakuwa more destructive kuliko faida yanazoleta..... Well Zitto tunayempenda ni Zitto Mpambanaji Zitto Mpinzani, Knowing What happens behind the scenes kwenye Chama hakutamsaidia Mtanzania yeyote, unless if what happens ni ufisadi then itabidi ajitahidi kusolve hayo mambo behind the scenes ikishindikana basi kuna alternative za kwenda ambako mambo yako sawa. Sababu kinachofanyika sasa ni kama kuibomoa boti ambayo wote wamepanda, its very likely kwamba wote watazama
 
Samahani kama ntakuwa nimewachanganya ila mawazo yangu ni kama ifuatavyo!
Ili chama kiweze kukua na kufahamika kwa kila mtu hata ambaye hependi siasa ingawa siasa ndio zinaongoza nji, lazima wawepo watu kama akina Zitto Kabwe Zitto ambao watakuwa wanaonesha na kuja na mawazo tofauti katika jamii. Hii itawafanya watanzania kuendelea kufatilia kinachoendelea katika chama hicho...Matokeo yake jina la chama linakuwa kubwa kwa sababu kitazungumzwa katika mijadala mbalimbali. Kwa hiyo kitendo cha Mh. Mbunge wangu, maana na mimi ni wa Kigoma Kaskazini kuonekana kama ndumilakuwili ni jitihada za kukitangaza chama kwa watanzania.
Kwa hiyo mimi binafsi sioni kama ni kosa kwa Mh Zitto kuleta changamoto kadhaa ndani ya CHADEMA. Hata hivyo migogoro ndiyo huimarisha chama maana ni kipimo kwaq viongozi wa juu kuweza kuonesha uwezo wao wa kutatua matatizo hayo, hivyo kujijengea jina na hadhi katika jamii husika.
Asanteni lakini musimuandame sana Mbunge wangu Zitto....Ameufanya mkoa wa Kigoma kuwa kwenye ramani ya Siasa.....
 
Kuna mwana JF alileta habari kwamba Zitto Kabwe amevuliwa uwanachama. Nimefuatilia na nimepata habari kama ifuatavyo.

Kikao kilichokuwa kimeendelea Zitto alitakiwa kujiuzulu nafasi zote za Uongozi ndani ya chama. Kama vile naibu katibu mkuu, Naibu kiongozi kambi ya upinzani bungeni na vingine vyote kama vipo. Anatakiwa kubakia kama mbunge na mwana chama wa kawaida kama alivyo mzee Sugu.

Kutakuwa na kikao kingine tarehe 9 hivyo bwana Zitto anao muda wa kufikiria mpaka hiyo tarehe kama achape mwendo au vipi.

Source ni gazeti moja lisilo la mafisadi hivyo am not sure kama watazirusha kesho au la.

Kuweni wapole nitaendelea kuwafahamisha.
 
Basi ungengoja mpaka uwe na uhakika kwa ishu nyeti kama hiyo; yaani unawashwa hata huwezi kusubiri? Patience and truth are virtues we must uphold
 
Mh jina lako lanitishia shala na hizo habari
 
Zitto is not my cup of tea at all, this kind of narcissistic behavior he has shown so far is not healthy for the party and opposition in general.
 
Nimeamini we malaria Sugu Una matatizo!!! si uhamie kwa michuzi
 
Malaria Sugu anafurahia habari anazoambiwa na SHETANI na anaamini ni za kweli.
mkimwona mwambieni namtumia rambirambi
 
Chadema ni taasisi ina hazina kubwa achana na vibraka wamvue madaraka abaki kama alivyo tuone janja yake akisema ovyo tena tupilia mbali lazima ajifunze discipline na asiwe mlopokaji wa hovyohovyo.
 
Chadema haina haja ya kuogopa chochote kama inasimamia kweli na haki.
 

Mkuu,
Tunashukuru kwa taarifa...endelea kufuatilia utupashe zaidi.

OMBI: Ndugu yangu, unaonaje kuhusu user name yako?
Mi huwa inanitisha kidogo...ingekuwa shwari sana ungeibadili.
 
Mungu akibariki CDM Ikamuondosha huyu Zitto itakuwa mwake tuu....yaani historia ya zitto ndani ya chadema huwa naifananisha na Historia ya Ballotelli alivyokuwa Inter....Kiburi, Haambiliki....mchochea utengano...mjivuni...Kinyonga..na anafanya vyote hivyo kwa sababu anajijua yeye ni muhimu......
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…