Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.

Kwa mantiki hii unanilazimisha kuamini kuwa una mgogoro Binafsi na mmoja wa uliowataja hapo juu. Kwa faida ya nani huo mgogoro? mimi sijui....


Inawezekana, swali langu kwako: kwa nini kila kukicha unaandikwa wewe tu? isitoshe sioni tatizo la mwandishi kuficha jina, kwa uzoefu wangu hii si mara ya kwanza kuona makala imeandikwa na mwandishi maalumu, labda tuseme analinda usalama wake.. Hivyo hapo penye nyekundu sidhani kama kuna ulazima wa huyo mwandishi kufanya hivyo.


Sijawahi kusema mahala popote kuwa ndani ya CHADEMA kuna udini. Ninaomba clip ya TBC iwekwe hapa jamvini na mtu anionyeshe wapi nimesem kuwa ndai ya CHADEMA kuna udinni. Tafadhali usinywe sumu unazopewa.

Hapo umenena. Kama kuna mwenye hiyo clip waungwana itasaidia kwa wale ambao hatujabahatika kuona kauli ya Mheshimiwa sana Zitto kuwa CHADEMA kuna udini..

Labda kwa kuongezea tu, Ndugu yangu Zitto jitahidi kuepuka kuwapatia watu nafasi ya kukuhukumu kwa maneno yako mwenyewe. Au kama huwezi kuvumilia basi tafuta mtu awe mshauri wako wa kisiasa ambaye atakuwa anakupa mwongozo wa nini useme na nini usiseme au ukiseme kwa kutumia maneno yapi, Siasa nayo ni sanaa wandugu. na neno likishatoka basi halirudi.

Silence can be misinterpreted but never misquoted, Even a stubborn fool is thought to be wise if he keeps silent.
 

Heri wewe umesema. Zitto siyo mustakabali wa Taifa letu.Na anayo hiari ya kujiunga na chama chochote. We are wasting time to discuss about him everyday.
 
Viongozi vijana hususan mna matatizo ya kuweka ego mbele mpaka mnaaibisha.

Hivi chama huwa hakijawafundisha namna ya kukabiliana na kuwa public figure au?
 

Nashukuru sana kwa ushauri wako. Wakati mwingine ukikaa kimya maadui zako huona kama ndio umekiri. Nimekaa kimya sana sana. Nilisimama kabisa kuja hapa nikadhani itapunguza chuki za watu. Hata hivyo haikukoma. Hata hivyo ushauri wako nimeuchukua kwa mikono miwili. Asante sana sana
 
samahani kama nimekukosea. Hizo tafsiri za uchaga ni zako. Sio zangu hata kidogo. Niwie radhi lakini. Pole
Kulikuwa na umuhimu gani wa kuandika Ansbert Ngurumo ni Secretary wa Mbowe?
Kwa nini umemtaja Komu mmiliki wa Mwanahalisi ukawaacha wengine wenye share kubwa kama Kubenea?
 

Mkuu Zitto umeandika Vizuri sana, lakini hapo kwenye nyekundu kidogo kunaonyesha kuna kitu kinafukuta kati yako na Mwenyekiti Mbowe,
Lakini mkuu pamoja na hayo yote kama ulivyosema kwenye bandiko lako, unahitaji mabadiliko makubwa ili kurudisha imani ya watu walioijenga kwako, Licha ya hayo magazeti unayoyaona yanakutuhumu, lakini pia kuna malalamishi mengi ambayo hayatokani na hayo magazeti

Nimeipenda sana hii signature yako mpya“Ukweli haupendi kupuuzwa puuzwa - TUJISAHIHISHE, Nyerere 1962.”

na mimi namalizia kwa kusema "yana mwisho"
 

Zitto ni mfano mmoja mdogo tu katika crisis ya uongozi, hata huko upinzani tulikofikiri kungetupa mbadala.

Hapa tunaongelea zaidi ya Zitto, huu ni mfano katika swala zima la uongozi Tanzania. Na kwa sababu viongozi wengine hawaji hapa, si vibaya kuwapa nafasi wale wanaokuja wajieleze vizuri.
 

Usikae kimya lakini think twice (no think three times and rethink) before you answear, BECAUSE SILENCE CAN BE INTERPRETED THAT YOU ARE GUILTY
 
2015 nitakuwa nina umri wa miaka 39. Katiba inasema kuwa Rais lazima awe na miaka 40. Hata hivyo, sio kosa kwa Mtanzania yeyote kusema anataka kuwa Rais ya Jamhuri yetu tukufu.
Sio ndiyo maana ukaomba Kikwete aongezewe muda.
 

Hata kuja na kuandika hapa haiwezi kupunguza chuki kwa sababu ukiandika unaongezea na taarifa nyengine ambazo ni za kichochezi.


As long as hujui unapaswa kuongea nini mbele ya watu hizo chuki haziwezi kumalizika.
 
Hata kuja na kuandika hapa haiwezi kupunguza chuki kwa sababu ukiandika unaongezea na taarifa nyengine ambazo ni za kichochezi.


As long as hujui unapaswa kuongea nini mbele ya watu hizo chuki haziwezi kumalizika.

I beg to differ, suala sio kwamba aache kuja hapa, bali ajibu majibu diplomatically na asiongee jambo ambalo linaweza kukiumiza chama chake
 
I beg to differ, suala sio kwamba aache kuja hapa, bali ajibu majibu diplomatically na asiongee jambo ambalo linaweza kukiumiza chama chake

Nisome vizuri. Sijamkataza kuja hapa kuandika.

Yeye anasema 'alinyamaza kimya' lakini chuki zikaendelea ndio akaamua aje ajieleze.

Sasa kama kujieleza kwenyewe ndo kwa namna hii ya leo, chuki haziwezi kuondoka kamwe. Manake kaanzisha jengine jipya leo, kuwa ndani ya chama kuna mtu au watu wanamhujumu.

SMH
 
Sio ndiyo maana ukaomba Kikwete aongezewe muda.


Sijawahi kuomba Kikwete aongezewe muda. Tanzania Daima waliandika habari hiyo kwa lengo maalumu na nililalamika rasmi kwa Mhariri mtendaji. Unaona sasa unanihukumu kwa habari iliyotungwa? Ndio maana nimetaja Tanzania Daima na Mhariri wake maana hii ni scheme ya muda mrefu na nimelalamika sana kimya kimya. Hata suala la mimi kutangaza nitagombea 2015 liliandikwa na Tanzania Daima peke yake tena kati kati ya kampeni. Hakuan aliyejiuliza ni kwa nini gazeti linalomilikiwa na Kiongozi wa CHADEMA linaweza kuandika kitu kama kile katikati ya kampeni.
 
Wana Jf hii mada ifungwe, Zitto amejibu kwa ufasaha bila kuwa na jazba pamoja na madongo yote, at least nimeona jinsi kiongozi anavyotakiwa kuwa.
 
Kulikuwa na umuhimu gani wa kuandika Ansbert Ngurumo ni Secretary wa Mbowe?
Kwa nini umemtaja Komu mmiliki wa Mwanahalisi ukawaacha wengine wenye share kubwa kama Kubenea?

MwanaHalisi linamilikiwa na watu wawili wenye hisa sawa. Hakuna mwenye hisa nyingi kumzidi mwenzie kati ya Komu na Kubenea. Vile vile Komu na Kubenea wameoa nyumba moja. Kwenye MwanaHalisi Komu na Kubenea ndio wamiliki pekee. Kama wewe unajua wamiliki wengine tuambie.
 


Nakuomba tu kwenye hiyo katiba mpya kuweke kifungu kitakacho fafanua matumizi ya TISS na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kwa manufaa ya taifa sio kwa kulinda manufaa ya viongozi na maslahi yao na hasa pale inapokuwa maslahi ya kiongozi ndio maslahi ya mafisadi na familia yake si ya wananchi wala nchi yao.
 
Wana Jf hii mada ifungwe, Zitto amejibu kwa ufasaha bila kuwa na jazba pamoja na madongo yote, at least nimeona jinsi kiongozi anavyotakiwa kuwa.
Mada ifungwe kwa kuwa ina jadili mgogoro wa chadema?Ingekuwa inahusu wana ccm hapa ungekuwa unapiga zumari!acheni hizo wanachadema acha mjadala uendelee!
 

Huwezi kutegemea ufanye makosa kisha usiandikwe kwa sababu tu gazeti linamilikiwa na mwenyekiti wa chama

Na kama unaona kuna tatizo kwenye hilo ulitakiwa uwasiliane na mwenyekiti wa chama na mjadiliane mpaka mpate suluhu. Kama msimamo wake ni hasi kwako, kwa faida ya chama unatakiwa umezee tu ufe kisabuni.

Hii ya kuja kuweka malalamiko ya kuonyesha kuwa kuna mvurugiko kwenye chama is not a good look kwako wala chama chako.
 
Mada ifungwe kwa kuwa ina jadili mgogoro wa chadema?Ingekuwa inahusu wana ccm hapa ungekuwa unapiga zumari!acheni hizo wanachadema acha mjadala uendelee!

Brother, hakuna mgogoro CHADEMA!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…