Percival Salama
Senior Member
- Feb 3, 2010
- 118
- 7
Mimi ni mmoja wa watu tunaoamini katika uwezo wa zitto kabwe kisiasa, lakini napata shida sana na upepo wa mwenendo wake tangu kuuibuka kwa richmond. ana uwezo wa kujenga hoja makini, lakini tangu kashfa hiyo kauli zake zimekuwa tata. CHADEMA imetuambia watanzania kuwa JK ameingia madarakani kwa kuchakachua kura. Kitendo cha mgawanyiko kwa minajili ya mitazamo na kuiita hiyo ni demokrasia ni kuwachanganya watanzania. TUNATOA WITO KWA DK SLAA NA CHADEMA kudhihirishia umma wa watanzania UCHAKACHUAJI wa CCM kwenye kura za URAIS vinginevyo Madai yenu yatapoteza haki ya kuaminiwa. THE RIGHT MAN ALWAYS STANDS ALONE.Zitto Kabwe ameeleza kuwa ni kweli walipiga kura na kukubaliana watoke wakati Rais akizungumza, lakini wao walipinga na ndiyo maana aliamua bora asiingie ndani ya Bunge, amesema kuwa yeye kama Zitto na wenzake aliona ni bora kutoingia kuliko kuingia na kutoka wakati Rais ambaye ndiye alama ya Bunge na Amiri jeshi mkuu akiongeaa.
Kwa vile kutoka ulikuwa msimamo wa chama, basi yeye na wenzake wamekosea na hilo ni swala la Chama kwani wanaweza kuadhibiwa na chama kwa vile kura za kukubaliana kutoka ilishinda.
Zitto alisema kuwa wanasubiria hatma yake katika chama na kusema kuwa hiyo ndiyo gharama ya Demokrasia. Ila amekanusha kuwa jambo hilo lisifikiliwe ni mgawanyiko bali mtazamo tofauti wa mawazo.
Source: TBC 1 News Bulletin
Nadhani Zitto aanchojaribu ni kuwafundisha nyie mashabiki wa CHADEMA kwamba msiwe watumwa wa mawazo, mitazamo na miongozo ya wachache. Kwa nini awe mtumwa wa mawazo ya Mbowe na Dr Slaa wakati yeye msomi na mwenye exposure ya siasa ya kimataifa.. Nyie lazima mkubwali kile kitendo kilikua cha kitoto na kilidhihirisha kutokua nna malengo ya muda mrefu ya chama.
Zitto Kabwe ameeleza kuwa ni kweli walipiga kura na kukubaliana watoke wakati Rais akizungumza, lakini wao walipinga na ndiyo maana aliamua bora asiingie ndani ya Bunge, amesema kuwa yeye kama Zitto na wenzake aliona ni bora kutoingia kuliko kuingia na kutoka wakati Rais ambaye ndiye alama ya Bunge na Amiri jeshi mkuu akiongeaa.
Kwa vile kutoka ulikuwa msimamo wa chama, basi yeye na wenzake wamekosea na hilo ni swala la Chama kwani wanaweza kuadhibiwa na chama kwa vile kura za kukubaliana kutoka ilishinda.
Zitto alisema kuwa wanasubiria hatma yake katika chama na kusema kuwa hiyo ndiyo gharama ya Demokrasia. Ila amekanusha kuwa jambo hilo lisifikiliwe ni mgawanyiko bali mtazamo tofauti wa mawazo.
Source: TBC 1 News Bulletin
Amri jesh mkuu ambae alishinda kwa wizi wa kura. Zitto, hoja ya kitoto. Sema nyingine.
Huna sababu ya kuwachukia. Kuna watu vichwa vinafanya kazi. Wanamptisha waziri mkuu na wanaomba serikali inayoongozwa na mtu wasiyemtambua asikilize madai yao!!!!! Kuna haja ya kufikiria upya strategies za namna hii. Zitto anatambua wazi kuwa strategy hii ni fake maana February watakuwa bungeni na wanahitaji kujadili hotuba ya Rais. Wakisusa kwa CCM ni mteremko tu maana hata utendaji wa serikali hawataujadili na kwa kifupi CCM watapeta zaidi. Nadhani aliyeshauri strategy hii alisahau kuangalia mbeleni. Mnakumbuka kura za maruhani Zenji? CHADEMA wanayaweza haya?
Hivi hapa pana siri gani?walipanga watoke nje na wametoka na wengine mkaanzisha chokochoko kwamba wale ambao hawakwenda bungeni na kutoka nje yaani hawakuingia kabisa bungeni ni wasaliti kwa bahati Zitto ni mmojawapo na ndiyo ameenda kujisafisha na kueleza kinagaubaga.mpaka mtakapoacha kila analolifanya Mh.Zitto kuwa ni issue nafikiri naye hataacha kuwashangaza kwani anaelewa gharama ya vijineno vyenu kwa wapiga kura wake.Hilo jina unalotumia haliendani na wewe kabisa,
Hebu elewa hivi
Watu hawamlaumu Zitto kupingana na wenzie, hiyo ni demokrasia na ndio maana Chadema waliitisha kura
WATU WANAMLAUMU ZITTO KUKIMBILIA KWENYE VYOMBO VYA HABARI NA KUROPOKA SIRI ZA CHAMA, KWANI ZITTO ALIKUWA PEKEYAKE ALIYEPINGA?, MBONA WENGINE HAWAKWENDA KWENYE VYOMBO VYA HABARI? YEYE NI NANI? NI MSEMAJI WA CHAMA?
Mwekeni pembeni letu jicho na masikio..............................!Nadhani wewe una matatizo makubwa. Hii sio habari ya kuandika, usidhani ni Kigoma tu wanachagua watu na sio Chama, kama unadhani ndivyo basi umekosea sana. Zito kama angekuwa na akili kama unavyosema angeliingia bungeni na kukaa kumsikiliza mshikaji wake JK. Kitendo cha yeye kutokufika bungeni ni unafiki wa hali ya juu na kiuongozi ni usaliti. Ingekuwa Chadema ni chama cha kijeshi, angeshapigwa risasi siku nyingi
Zito in all aspects ni mvurugaji wa chama, kuna mambo anafanya ambayo sidhani kama yanamsaidia. Lakini kiongozi makini ni yule mwenye msimamo na asiyekubali kuyumbishwa, sioni kama hilo analo Zito. Kuna kipindi alisema hatogombea tena ubunge, mara atachangua jimbo la kugombea, mara akagombea, mara niko shule. He can not be trusted. Wakati kampeni za uchaguzi zinaendelea, alitangaza kugombea uraisi 2015 very strange, bila kujua outcome ya uchaguzi huu. Zito alishaweka kichwani kuwa Dr Slaa hatoshinda, na ndio maana haoni kama kilio cha Chadema kina maana.
Hili na kupiga kura ndani ya chama sidhani kama alipashwa kulileta mitaani, anajikosha kwa watu, na anataka kugombea uraisi 2015, kweli, kwa mazingira haya haya, au anadhani bila pressure mambo yatakuwa tofauti, loh, amekosa weledi wa kutambua hii hali yote
Kwa wanaokumbuka kilichoivuruga NCCR ni kila mmoja kati ya Mbatia, Marando na Mrema, Selasini kuwa wasemaji wa Chama. Zito hakupaswa kukimbilia kwenye vyombo ya habari na kuteta kilichofanyika katika vikao vyao vya ndani. Huko ni kukosa kuheshimu mamlaka husika ndani ya chama na nadhani Chadema wanapaswa kumchukulia hatua kali. Hujamsikia mjumbe wa kamati kuu ya ccm akienda kwenye mtanzania daima na kueleza kilichotokea ndani ya kamati kuu kumuengua Sitta.
Nakubaliana na wanaosema kuwa Zito ni wa kumuangalia sana, he is cheap and he can easily be seduced. He has tried several times kupingana na mwenyekiti wake, na nadhani ana bifu na Mbowe. I think the best way watanzania watamheshimu ni kwa yeye kuondoka Chadema kwa amani kama hakubaliana na mwenyekiti wake na viongozi wenzake, kuliko kukivuruga chama. Asingojee kupewa adhabu, kwa kuwa ndicho anasubiri kifanyike, Chadema, dont waste time na huyu mtoto, wala hakuna haja ya kumchukulia hatua, kwani mtakuwa mmefanya kile anachokitaka, cha msingi ni kumsideline, kwa kuwa hawezi kutunza siri za chama, basi awekwe pembeni tu, this time is critical na sidhani kama kuna muda wa kupoteza na huyu mlimbwende Zito
Umenena watu wanasahau kwamba CCM Imefika hapo ilipofika kwasababu ya ukandamizwaji wa hoja na mitazamo tofauti,Sasa hiki chama kinasema mbadala lakini watu wakileta fikra mbadala wanaitwa wasaliti..............!Tanzania yetu wengi ni walewale na hata Hawa Chadema wakipewa Dola nafikiri mwendo utakuwa mdundo kama kopi ya CCM.si jamvini pekee ndugu. ni tatizo letu watanzania! TUNATAKA TUNACHOKITAKA NA HATUTAKI TUSICHOKITAKA, mara nyingi tunashindwa KUKUBALIANA KUTOKUBALIANA. Huku tukiimba kwamba tunajenga demokrasia. Sidhani kama tunaweza kujenga Demokrasi bila kukubali kupingana, bila kuwa wawazi, kwanini iwe siri? Iwe siri ili iweje? Zito Kabwe amefanya kitu sahihi kabisa na ninamuunga mkono kwa hilo. Alipata kujibu alipohojiwa "...Maslahi ya taifa kwanza!" Ndicho alichoangalia. Je kwanini ahukumiwe kwa hilo? Chadema si baba wala mama yake.
Kufanywa au kutofanywa wajinga inategemea mtu amnaelewaje na anatafsiri viti taratibu na sheria zinazosimamia eneo husika. Naamini mdogo wangu Zitto ana akili timamu na anafanya jambo bila kukurupuka kama unavyodhani. Demokrasia ni pamoja na kujua jinsi ya kuwa mwana dipromasia pia. Kijana huyu anajua kusoma nyakati...... big up ZITTO!!
Tatizo jamani sisi wana jf tuking'ang'ania jambo hatutaki kushindwa,zito ameweka wazi yaliyojili ktk mchakato mzima wa kupiga kura,ameonyesha kuwa kunakosa lilifanyika na wanasubili maamuzi ya chama dume
nampongeza zito,siasa ipo hivyo,ikiona umekosa unasema na ukiona huna kosa unasema
tuendelee kuwaunga mkono wapambanaji na ipo siku tutakuwa pale na sio hapa tulipo sasa
mapinduziiiiii daimaaaa
Yeye alihujumu chama kigoma kivipi?Si aliwaeleza kitendo cha kumuita mtu sisimizi na ambaye angekuwa asset baadae si vyema mlisema aende tu,aliwasihi sana kutoa adhabu mbadala kama mnaona Kafulila amekosea mkaona mnayaweza.Sasa mnamlaumu Zitto kwa lipi?Uongozi umevuna walichopanda kigoma period!ZITTO KABWE ni mnafiki, na anaependa kuweka maslahi yake mbele wala sio ya chadema. yeye ndie aliihujumu CDM huko Kigoma mpaka ikakosa wabunge wengi. ni mtu anaependa sana kujitanua yeye kama yeye huku akijiona ni Mungu mtu pale chadema.
Anapenda sana makundi,fitna na chuki zisizo na msaada kwa CDM. ushauri wangu zitto hamia CCM ili ujiweke wazi usikae cdm huku unahujumu chama hiyo ni usaliti nao ni dhambi kubwa kwa mungu.
Kufanywa au kutofanywa wajinga inategemea mtu amnaelewaje na anatafsiri viti taratibu na sheria zinazosimamia eneo husika. Naamini mdogo wangu Zitto ana akili timamu na anafanya jambo bila kukurupuka kama unavyodhani. Demokrasia ni pamoja na kujua jinsi ya kuwa mwana dipromasia pia. Kijana huyu anajua kusoma nyakati...... big up ZITTO!!