mwita ke mwita
JF-Expert Member
- Aug 13, 2010
- 8,058
- 3,755
muhongo ni jembe sana mi namkubali majigambo yake, le prefeseri
Kama CCM watakuwa wa kuendelea kuongoza nchi, basi na waache porojo nyingi na wamsimamishe Prof. Muhongo. Huyu muhemishimiwa yuko makini (smart) sana katika utendaji na katika kupangilia mikakati.
Kama ulisikiliza hotuba yake ya kutangaza nia, tukio ambalo halikuwa na makuu, kwa watu makini watakubaliana na yeye kuwa nchi yoyote duniani haiwezi endelea bila tafiti. Hili ni suala ambalo viongozi ama wanasiasa wengi wamekuwa wakilipa uzito mdogo sana na kujikita zaidi kwenye mambo ambayo ni ya kufunika kombe (cosmetic), ambayo mara nyingi yanakuwa sio endelevu
Muhongo siyo kiongozi hawezi uongozi sense akufundishe. Sisi with wa Mtwara hatumpendi hata kidogo. Hivi mnajua kuwa gesi yote anyotambia huyo prof ipo Mtwara na Lindi sisi tunasema hafai. Iketokea akawa raisi lazima umwagaji wa damu utatokea
hamjamaliza tu shughuli ya kutanganza nia huko?? naona nyie mmeamua kuja kimila zaidi!! haya bana!! Mgetembelea pia IKULU ya Chief Lungusha pale Sikonge kupata baraka zaidi.Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Tabora)
Nampa muhongo kura amesema ataniletea bomba la gas na maji ya bomba hadi huku ukerewa nansio
Napiga picha za maboma na tembe kufungwa mabomba ya gesi wakati maji yamekuwepo tangu kuumbwa kwa dunia lakini serikali imeshindwa kupeleka mabomba ya maji kwenye kila nyumba! Siasa ni balaa maana prof. haoni aibu kusema uongo hadharani kisa madaraka.Muhongo katumia falsafa ya kusadikika. Kila nyumba kuunganishwa na bomba la gesi?????!!!! Labda tusemee tu kwa pamoja NDIYO MZEE!!!!
muhongo ni jembe sana mi namkubali majigambo yake, le prefeseri
ZZITO umejuaje kuwamhaiwezekani? yeye kama mtalamu anaaminimhivyo subili ashidwe hacha majungu.
Jamaa anawadharau sana watz eti kwa vile muda mwingi ameishi na kusoma ujerumani. Alifikia hata kuongea kijerumani cha kuokoteza, tunaokijua tulikuwa tunamsikiliza tu kwani hakukuwa na nafasi ya kuuliza maswali
ZZITO umejuaje kuwamhaiwezekani? yeye kama mtalamu anaaminimhivyo subili ashidwe hacha majungu.
Subili ashidwe hacha majungu = Subiri ashindwe acha majungu (Siamini kama ni typing error kwa maneno yote hayo utakuwa unatatizo kubwa mzee,ndio mana ni rahisi kwako kukubali ya Muhongo kwamba atasambaza bomba la gesi na maji kila nyumba ya Mtanzania)ZZITO umejuaje kuwamhaiwezekani? yeye kama mtalamu anaaminimhivyo subili ashidwe hacha majungu.
Nasikia ni mmanyema wa kariakoo, je, kimanyema anakijua? Kizaramo anakijua? Kiingereza anakijua? Au anadhani akijua Kijerumani hadhi inapanda? HKuna watu tumezaliwa huko na bado hatuzungumzi lugha hiyo! Yeye ni ulimbukeni tu, ambayo ni mbaya ktk umri wake.
Huyu ni mtu ambaye binafsi sijawahi kumuona kuwa ana matumizi ya maana. Zipo kazi ambazo naweza nikampa lakini siyo siasa aliyoingia. Sitegemei apange la maana kwa mwananchi. Sijui mwaka huu atakuwa na dili gani maana posho ya kuachia majimbo hataipata.