Prof. Muhongo afunguka mikataba ya madini, kutokuwapo kwake bungeni kipindi cha Bunge la bajeti

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,408
2,000
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amesema hahusiki na mikataba ya yote ya madini.

Muhongo alitoa maelezo hayo jana, ikiwa si siku moja baada ya Nipashe kuripoti kutoonekana kwake bungeni bila ruhusa ya Spika.

Aidha, Prof. Muhongo alidokeza Nipashe chanzo cha kutokuwapo kwake katika chombo hicho cha kutunga sheria kwa wiki tano sasa.

Gazeti hili jana liliripoti kuhusu kutoonekana bungeni kwa mbunge huyo wa Musoma Vijijini (CCM) bila ruhusa ya Spika tangu uteuzi wake katika baraza la mawaziri utenguliwe wiki tano zilizopita.

Katika ripoti hiyo ya jana, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alisema ofisi yake haina taarifa za mtaalamu huyo wa kimataifa wa Jiolojia na haijui aliko tangu alipoachishwa nafasi ya uwaziri, muda mfupi baada ya Rais John Magufuli kukabidhiwa ripoti ya Kamati ya kwanza ya uchunguzi wa mchanga wa dhahabu (Makinikia) Mei 24, mwaka huu.

Hata hivyo jana asubuhi Prof. Muhongo kupitia simu yake ya mkononi ambayo kwa siku tofauti amekuwa akipigiwa bila kupokea, alituma ujumbe mfupi wa maandishi kwa Nipashe akikana kuhusika na mkataba wowote wa madini na kutolea ufafanuzi kutokuwapo kwake bungeni kipindi hiki muhimu cha Bunge la bajeti.

Katika maelezo yake Prof. Muhongo alisema hahudhurii vikao vya Bunge kwa kuwa yuko mapumziko.

Aliongeza kuwa kipindi hiki hataki malumbano na hahusiki na mikataba mibovu ya madini ambayo kwa sasa 'imeteka' vinywa vya watanzania wengi wakiwamo wabunge.

"Muhongo yuko mapumzikoni. Hataki malumbano na hahusiki na mikataba yote hiyo", aliandika.

Nipashe ilipotaka kujua mahali ambapo Prof. Muhongo ameamua kupatumia kupumzika, msomi huyo alijibu kwa ufupi " It is my private life''(ni maisha yangu binafsi).

Nipashe pia ilitaka kujua kauli ya Prof. Muhongo kuhusu kutenguliwa kwa uwaziri wake na sababu za kuamua kwenda mapumzikoni kipindi hiki ambacho Bunge linajadili bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao wa fedha.

Hata hivyo, msomi huyo hakuwa tayari kueleza kwa kina. Katika majibu yake Prof. Muhongo aliandika: " Tuheshimu taratibu za malezi, utamaduni, uzoefu na tabia ya kila mmoja wetu".

Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah aliiambia Nipashe juzi kuwa ofisi yake haina taarifa za Muhongo jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Chanzo: Nipashe
 

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,097
2,000
Sawa prof. Muhongo!
Bora ungebaki kufundisha chuo kuliko huku unadhalilika namna hii
 

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,158
2,000
Prof kweli hakusaini huyo mikataba...
watu wanahoji kwa nini kama yeye kwa kujua kwamba kuna malalamiko ya madini na mchanga miaka yote...
angalau kufanya initiative yoyote kujiridhisha kwa upande wake au kupitia wataalamu wake siku zote amekuwa waziri...
 

Terrible Teen

JF-Expert Member
May 1, 2017
565
1,000
Profesa Muhongo is highly confused , JPM kamtenda vibaya. Kwenye Vikao vya baraza la mawaziri he was the most outspoken minister mwenye kuaminiwa zaidi na JPM. It came by surprise kutumbuliwa.Itachukua muda kwa muhobgo kurudi normal.
 

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,171
2,000
Sijui ni kwanini naona Prof kama ni innocent? Siasa ni kazi ya ajabu sana, niliwahi kusikia kwamba ukiwa kiongozi unayefanya kazi karibu na Rais unaweza ukapata changamoto ya kufanya maamuzi kiasi kwamba ukiagizwa jambo na mkuu wako ukisema 'YES' ni hatari, ukisema 'NO' ni hatari, 'USIPOJIBU' ni hatari na 'UKIJIUZURU' ni hatari pia.
 

pecial

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
638
500
profesa ana hasira asee, achana na siasa prof nenda kaendelee na taaluma yako bhana ya kufundisha huku wasomi hakuwafai
 

Menyainganyi

JF-Expert Member
Mar 12, 2013
1,172
2,000
Profesa Muhongo is highly confused , JPM kamtenda vibaya. Kwenye Vikao vya baraza la mawaziri he was the most outspoken minister mwenye kuaminiwa zaidi na JPM. It came by surprise kutumbuliwa.Itachukua muda kwa muhobgo kurudi normal.
Professor Mwakyembe nae anafuata nyayo . . , soon atashangaa jinsi atakavyotupwa nje . . Hata Prof Kabudi, ajiangalie sana . .
Hawa ma Professor wanatumika tuu kama Toilet papers na wanasiasa wa ccm . .

Tazama Prof Kabudi anavyojiandaa kufanya kazi ya kishetani kwa kuandaa muswada wa Sheria kudhibiti Wanasheria na Mahakama Huru . .
Ajabu, baada ya muda sheria hizo hizo wanazopitisha leo, ndio zitakazowavunjia heshima ccm na hao ma Prof wachumia tumbo . .

cc. Paskali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom