Asemavyo Zitto kuhusu Prof Muhongo. Ampa changamoto hizi

Asemavyo Zitto kuhusu Prof Muhongo. Ampa changamoto hizi

matumbo

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2011
Posts
7,224
Reaction score
3,960
Prof. Sospeter Muhongo alikuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati wa sakata la ‪#‎TegetaEscrow‬. Kamati ya Bunge ilipendekeza na Bunge kuazimia kuwa Muhongo avuliwe madaraka yake ya Uwaziri. Prof. Muhongo alijiuzulu. Akafanyiwa uchunguzi na Kamishna wa Maadili kutamka kuwa hakukutwa na kosa la kimaadili. Unajengaje hoja kuwa hana haki ya kuteuliwa kuwa Waziri? Keshaadhibiwa kwa kosa la awali, kwa kujiuzulu. Sheria ipi inasema hana haki ya kuteuliwa tena?

Niliongoza Kamati ya PAC. Nina uhakika Waziri muhongo kwenye sakata lile alishauriwa vibaya na kujikuta anatetea ubadhirifu. Lile ni funzo kubwa kwake na ninavyomuona sasa hatarudia tena makosa yale.

Kuna mambo ya msingi lazima afanye sasa

1) Azuie kuanzia sasa malipo ya 'capacity charges' kwa kampuni ya kitapeli ya IPTL na atumie sheria kutwaa mitambo ya IPTL na kumilikisha TANESCO.

2) Amtake Waziri wa Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kumkamata mara moja anayejiita mmiliki wa IPTL na afunguliwe mashtaka ya utapeli, wizi wa udanganyifu na uhujumu uchumi; huyo mmiliki na washirika wake ambao ni raia wa Tanzania.

3) Amtake Gavana wa Benki Kuu na FIU kuichukulia hatua za kisheria Benki ya Stanbic ikiwemo kupiga faini ya kurejesha fedha zote zilizokua kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Hizo ndio hoja za msingi na sio uteuzi wa Prof. Muhongo. Mwenye ushahidi dhidi ya Muhongo si aende Mahakamani?

Tuache siasa za porojo porojo..

=======

Chanzo: Ukurasa wake (Zitto Kabwe) wa mtandao wa Facebook
 
Muhongo - Kuna kijana mmoja yuko upinzani ni mlafi sana wa rushwa...

Muhongo - Nashukuru chama chake wamemfukuza....

Mchange - Muhongo alijiuzuru with confidence...

ACT ni chama cha watu wenye msongo wa mawazo...
 
Muhongo - Kuna kijana mmoja yuko upinzani ni mlafi sana wa rushwa...

Muhongo - Nashukuru chama chake wamemfukuza....

Mchange - Muhongo alijiuzuru with confidence...

ACT ni chama cha watu wenye msongo wa mawazo...
tUNDU LISU-uFISADI SIYO AGENDA MUHIMU YA WATANZANIA
TUNDULISU-KUTEULIWA KWA MUHONGO NIDHARAU KWA BUNGE
ZITTO-LAZIMA NIWE MKITI WA MASHIRIKA YA UMMA HIVYO LAZIMA NISHIRIKIANE NA WALIO WENGI.
ZITTO-KITU KINACHOONGEWA NA WANASIASA KWA UKELI NI JINA LAO TU
 
Amshauri na hili: ajifunze unyenyekevu kwenye kazi za umma; ameona nguvu zake! Na Zitto akayafanyie kazi bungeni haya aliyomshauri Muhongo.

matumbo
 
Last edited by a moderator:
Hiki ndiyo kinachonifanya nimkubali sana Mh. Zitto. Kwenye ukweli huwa anaongea ukweli japo wakati mwingine huwa nahisi anatumiwa na hawa wafanyabiashara wezi wanaojiita wazawa.
 
hiki ndiyo kinachonifanya nimkubali sana mh. Zitto. Kwenye ukweli huwa anaongea ukweli japo wakati mwingine huwa nahisi anatumiwa na hawa wafanyabiashara wezi wanaojiita wazawa.

anatafutwa kuungwa mkono na ccm kwenye kamati.akikoswa tu au kupata ndo mtamjua zitto ni nani? Anajua kikwete ameondoka hivyo lazima aajenge njia ya kuaminika serikalini
 
anatafutwa kuungwa mkono na ccm kwenye kamati.akikoswa tu au kupata ndo mtamjua zitto ni nani? Anajua kikwete ameondoka hivyo lazima aajenge njia ya kuaminika serikalini

Inawezekana mkuu.

Huyu jamaa miaka hii ya karibuni siasa zake nimeshindwa kuzielewa kabisa. Leo atasema hivi, kesho vile. Siyo mtu wa kuaminika.
 
Huu ndio msimu wa ZZK kujikomba sana kwa watawala...
Fahamu zake zote zimeshamtoka pale alipo..
Kisa... uenyekiti wa PAC.
 
Inawezekana mkuu.

Huyu jamaa miaka hii ya karibuni siasa zake nimeshindwa kuzielewa kabisa. Leo atasema hivi, kesho vile. Siyo mtu wa kuaminika.
Ni mfumo wa siasa za CHADEMA, na ndio sababu wamediriki kukana kauli zao wenyewe
 
Ina maana PAC ilikurupuka?
Ina maana Bunge lilifikia maazimio husika bila ya kujiridhisha?

Zitto alibadilika bungeni wakati wa mjadala husika na kuhamia upande wa pili wa hoja. This is Self defense mechanism at work. It is also a a pre -emptive strike kuelekea bunge lijalo, kwa maelekezo ya chama kilichomsaidia ubunge (CCM). Kitila Mkumbo alishaweka wazi kupitia gazeti la Raiamwema kwamba lengo kuu la ACT ni kupambana na upinzani (Chadema), sio chama tawala. Hizo ndio siasa za upinzani wanazotaka CCM. Ndio maana chama hiki kikahakikisha kwamba kinamsaidia Zitto arudi bungeni. Bila ya juhudi za CCM Kigoma (Zikiongozwa na Kikwete), kumzima Kafulila na kumpaisha Zitto, huyu mtu asingerudi bungeni.

Huu ni mwanzo tu, tutarajie burudani zaidi kutoka kwa Zitto.
 
Inawezekana mkuu.

Huyu jamaa miaka hii ya karibuni siasa zake nimeshindwa kuzielewa kabisa. Leo atasema hivi, kesho vile. Siyo mtu wa kuaminika.
Dunia ina maajabuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Back
Top Bottom